Aliyeona ndiye anayeweza kushuhudia kweli HD 1080p

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 7 ก.ย. 2024
  • Katika kipindi hiki;
    Maelezo ya aya 7-8 (tofauti katika upangaji wa aya)
    Maelezo ya aya kwa aya 6-12
    Ufafanuzi ya maana
    1Yohana 5:6-12
    Ushuhuda kuhusu Mwana wa Mungu
    6 Huyu ndiye alikuja kwa maji na damu, yaani, Yesu Kristo. Hakuja kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. 7 Kwa maana wako watatu washuhudiao. Roho, Maji na Damu; hawa watatu wanakubaliana katika umoja. 9 Kama tunaukubali ushuhuda wa wanadamu, basi ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi, kwa kuwa huu ndio ushuhuda wa Mungu kwamba amemshuhudia Mwanawe. 10 Kila mtu amwaminiye Mwana wa Mungu anao huu ushuhuda moyoni mwake. Kila mtu asiyemwamini Mungu amemfanya yeye kuwa mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda Mungu alioutoa kuhusu Mwanawe. 11 Huu ndio ushuhuda: kwamba Mungu ametupa uzima wa milele, nao huo uzima umo katika Mwanawe. 12 Aliye naye Mwana wa Mungu anao uzima, yeye asiye na Mwana wa Mungu hana uzima.
    Tatizo ya aya ya 7-8
    Katika aya ya 7-8 kuna nyiongeza ambayo haipo katika miswada ya mwanzo inasema [ mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho Mtakatifu. Hawa watatu ni umoja. 8Pia wako mashahidi watatu duniani]
    Maneno haya yanapatikana kwa mara ya kwanza 385, miswada yote yanayotangulia hapo haina hiyo sentensi. Inaaminika kwamba kwanza iliwekwa kama note ya kuonyesha utatu halafu mtu akaingiza katika mswada. Utatu unapatikana sehemu zingine kwa hiyo si kwamba inaleta kitu ambayo si kweli lakini inaonekana Yohana hakuiweka mwenyewe alipoandika waraka wake.
    Na mpangilio ya aya kidogo zinapangwa tofauti katika baadhi ya tafsiri za kiswahili.
    1Yohana 5:6
    Yesu Kristo alifunuliwa kama mwana wa Mungu kwa kupitia ubatizo wake, na kwa kutoa damu yake msalabani
    Maji na damu inaweza kuwa na kusudi mbili ya maana
    Kifo chake msalabani pale alipo chomwa mkuki na damu na maji ilitoka (wakati damu na maji katika mwili inatoka kama kioevu mbili mtu kwa uhakika amekufa na Yohana mwenyewe alishuhudia hiyo ka macho yake.
    Maana ya pili ni ubatizo na kifo chake msalabani.
    Na Roho pia aliye mkwelipia anashuhudia (Yoh 15:26, 16:13-15) ndiyo maana anaitwa Roho wa kweli.
    Roho ndiyo anayofunua kwa muumini ukweli wa Kristo.
    Roho wa kweli LAZIMA anakubaliana na ukweli wa Mungu.
    1Yohana 5:7-8
    Matatu yanayotajwa katika (6) Roho, Maji na damu yote ni shahidi ya ukweli wa Kristo
    Kuhusu yeye ni nani
    Kuhusu kazi aliyokuja kuifanya
    Kuhusu ushindi wake
    (Nyongeza ya 7-8 nimeshaipitia)
    1Yohana 5:9
    Hapo tu inasema ushahidi wa Mungu ni kuu kuliko ya wanadamu
    Katika sheria ya kiyahudi ushahidi ilihitaji mashahidi 2-3 ku ridhisha. Hapo Mungu anatoa 3 Roho, Damu na Maji.
    Katika Injili ya Yohana 5:31-47 inafafanuliwa zaidi na maneno ya Yesu mwenyewe.
    1Yohana 5:10
    Wanao mwamini Yesu mwana wa Mungu wanahisi mioyoni mwao kwamba ushuhuda huo ni wa kweli.
    Hiyo inafanyika kwa sababu Roho wa Mungu anakaa ndani yao na kuwapa amani katika hilo (Warumi 8:16, Gal 4:6)
    Ambao hawamwamini wanamfanya kuwa mwongo, kutokumwamini Yesu kama mwana wa Mungu ni kumkataa Mungu kama aliye mkweli. = inapinga ukweli wa Mungu, inampinga Kristo.
    Kwa sababu wanakataa kuamini ushahidi ambao Mungu ametoa kuhusu mwana wake.
    1Yohana 5:11
    Mungu ametupa maisha ya milele na maisha ya milele yanapatikana kupitia Kristo, (Yoh 1:4, 14:6, 2Tim 1:10)
    Bila imani sahihi juu ya Kristo hakuna maisha ya milel kwa Mungu.
    Wanao mkataa Yesu wanabaki katika kifo. (Efeso 4:18)
    1Yoh 5:12
    Mwenye kuwa naye Mwana anayo uhai, mwenye kumkosa hana uhai
    Wanadamu hawana uhai kwa nguvu yao wenyewe, wanapewa huai kutoka kwa mwana wa Mungu
    Mwana wa Mungu hana sehemu ambapo anaitoa huo uhai bali anayo uhai ndani yake yeye ni chemchemi ya uhai, hiyo ni sifa ya kimungu.
    Hakuna kiumbe kilichoumbwa ambaye anayo chemchemi kama hiyo.
    Sasa wenye kuwa naye huyo mwana kuishi ndani yao (wamepokea wokovu) wanao huo uhai wa milele, na uhai huo wanao hata sasa.
    Ufafanuzi;
    Tangu wakati wa kanisa la kwanza kumekuwepo makundi yanayo kataa kwamba Yesu alikuwa Mungu
    Wengine walikataa kukubali kwamba alikuwa mwanadamu
    Yohana anasema katika maandiko yake kwamba alikuwa naye alimtambua na anafahamu wkamba ailkuwa mwanadamu (Yoh 1:1-5, 1Yoh 4:2)
    Hali kadhalika maandiko yanatuambia kwamba yeye ni mwana wa Mungu = Mungu (Mathayo 3:16-17, Marko 15:39, Warumi 1:3-4
    Wanao kubali na kuamini ukweli wa ushuhuda wa Kristo wanakubali kwamba Mungu ni wa kweli na wanapata wokovu
    Wanaokataa ukweli unaoletwa na maandiko ya Mungu wanakataa ukweli wa Mungu na kumwita mwongo, wanakataa kupokea ukweli wa Mungu na wanabaki katika giza ambayo ni ukosefu wa uhai wa Mungu.

ความคิดเห็น • 4