Walioshamiri: Khadija Ali, Mtangazaji Wa KBC Radio Taifa Nchini Kenya Anayevuma Tangu 1974

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 11 ก.ย. 2024
  • Khadija Ali Mohammed anatajika kuwa miongoni mwa magwiji wa utangazaji wa redio nchini Kenya akiwa amehudumu katika shirika la kitaifa la utagazaji la KBC kitengo cha redio. Bi. Khadija Ali alijiunga na KBC kama muigizaji mwaka 1974 ambako alihudumu kwa takriban miaka 9 kabla ya kuajiriwa kama mtangazaji wa KBC Radio Taifa.
    Mama huyu wa watoto watano alizaliwa eneo la Mji Wa Kale (Old Town) kaunti ya Mombasa na kuhamia jijini Nairobi akiwa mtoto mchanga. Licha ya kutomaliza masomo yake ya shule ya upili, maono aliyokuwa nayo pamoja na mapenzi ya utangazaji zilimpelekea kuandama ndoto yake ya uwanahabari. Bidii yake na talanta aliyokuwa nayo ilimpa fursa ya kuendeleza masomo yake ya utangazaji nchini Ujerumani pamoja na kushinda tuzo kadhaa.
    Sauti yake nyororo na mbwembwe alizonazo anapokuwa kazini zinalainisha nyoyo za mashabiki wengi na kuwafanya kuganda pembeni mwa redio zao wakati wa kipindi chake cha nyimbo za taarabu. Kando na utangazaji, Khadija Ali ni mtayarishi wa vipindi na mtunzi wa mashairi.

ความคิดเห็น • 7

  • @thelivingwordchannel9027
    @thelivingwordchannel9027 4 หลายเดือนก่อน

    Huyu mama alikuwa akitangaza vizuri sana

  • @shamimnoor4824
    @shamimnoor4824 10 ปีที่แล้ว +4

    poleni sana tena sana kwa kufiwa mwimbaji maarufu

  • @shifaaal-baity4503
    @shifaaal-baity4503 5 ปีที่แล้ว +2

    Mungu ampe uzima bi khadija Ali

  • @user-td9lq1rg8v
    @user-td9lq1rg8v 3 หลายเดือนก่อน

    Kwao ni huku lamu mpeketoni mama yao mama kandogo pia majirani wetu

  • @hedzupvisuals1272
    @hedzupvisuals1272 2 ปีที่แล้ว

    nilisoma na wattoto wake watatu

  • @LilKindy
    @LilKindy 3 ปีที่แล้ว +1

    mbna namuona mwanaisha mahali hapo

    • @AhmedJumaBhalo
      @AhmedJumaBhalo  3 ปีที่แล้ว +1

      Una macho makali boss wangu. Ndiye pamoja na marehemu Ahmed Darwesh. Wote walikua wanafunzi wa mama Khadija Ali.