EWURA YAFUNGIA VITUO SABA VYA MAFUTA "TUNAKOELEKEA TUTAFUTA LESENI"

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 14 ต.ค. 2024
  • Ikiwa imesalia wiki moja kuelekea kutangazwa kwa bei elekezi ya mafuta nchini kwa mwezi Octoba mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kufungwa kwa vituo saba ya mafuta kwa kipindi cha miezi sita kwa kukiuka sheria ikiwemo kuficha Mafuta
    Taarifa ya EWURA imetolewa na Titus Kaguo Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo amesema katika kipindi cha mwezi Julai na Agosti vilifungiwa vituo vitano na mwezi septemba vimefungiwa vituo viwili ambapo mamlaka hiyo ilitoa fursa ya siku 21 kwa kampuni zilizofungiwa kuwasilisha utetezi kuanzia septemba 18,2023.
    “hii biashara inahusisha usalama wa nchi tukisema mafuta hayapo utaona mihimili inasimama na tunakoelekea tutafuta leseni lakini uchunguzi bado unaendelea na Jana(29/09/2023) bodi ya wakurugenzi ilijiridhisha kuwa kuna vituo vingine vimeingia viliingia kwenye mkumbo huo wa kuhodhi mafuta bila kuuza na bodi ya wakurugenzi imeagiza hivyo vituo hivyo vifungwe kwa musa wa miezi sita”

ความคิดเห็น • 11