KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA FRIDAY PRAYERS - THE SCHOOL OF HEALING 15/ 11/ 2024

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 14 พ.ย. 2024
  • KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA FRIDAY PRAYERS - THE SCHOOL OF HEALING 15/ 11/ 2024
    MAFUNGO YA SIKU 40 - SIKU YA 12
    UJUMBE WA LEO: ''WEKEZA KWENYE UWEZO WAKO"
    "INVEST IN YOUR CAPABILITY"
    NENO KUU : Waamuzi 6 : 14
    ENENDA KA UWEZO WAKO HUU
    UJUMBE WA LEO : "NENDA KAJICHONGE"
    Waamuzi 11 : 1 - 11
    1 Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha.
    2 Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine.
    3 Ndipo Yeftha akawakimbia hao nduguze, akakaa katika nchi ya Tobu; na watu mabaradhuli walikwenda na kutangamana na Yeftha, wakatoka kwenda pamoja naye.
    4 Ikawa baadaye, wana wa Amoni wakapigana na Israeli.
    5 Ikatukia, hapo wana wa Amoni walipopigana na Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumtwaa huyo Yeftha katika ile nchi ya Tobu;
    6 wakamwambia Yeftha, Njoo wewe uwe kichwa chetu, ili tupate kupigana na wana wa Amoni.
    7 Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa wakati mlio katika taabu?
    8 Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, Kwa ajili ya hayo sasa tumegeuka kukuelekea wewe tena, ili uende pamoja nasi na kupigana na wana wa Amoni, nawe utakuwa kichwa chetu juu ya wenyeji wote wa Gileadi.
    9 Basi Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi Kwamba mwanirejeza kwetu tena ili kupigana na wana wa Amoni, naye Bwana akiwatoa mbele yangu, je! Mimi nitakuwa kichwa chenu?
    10 Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, Yeye Bwana atakuwa shahidi kati yetu; hakika yetu tutafanya sawasawa na neno lako.
    11 Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kichwa, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya Bwana huko Mispa.
    AGENDA ZA MAOMBI
    1. TOBA NA REHEMA
    2. KUOMBAEA HAIBA YAKO
    3. KUOMBEA MIPANGO YA MUDA MFUPI NA
    MUDA MREFU.
    4. MAOMBI YA UPONYAJI NA KUFUNGULIWA
    Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
    Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
    Simu: +255 713 553 443
    TH-cam: Kijitonyama Lutheran church
    Barua Pepe: Kijitonyamalutheran@gmail.com

ความคิดเห็น •