CCM YAMKATAA NAPE KISA KAULI YA USHINDI "NJE YA BOKSI" MWENYEWE ATOA UFAFANUZI

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 25 ส.ค. 2024
  • Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema video inayosambaa ikimuonyesha akisema kuna mbinu nyingi za CCM kushinda uchaguzi ikiwamo zisizo halali imepotoshwa na hakuwa na maana iliyotafsiriwa na watu wengi.
    “Nimeona mjadala wa video hii. inapotoshwa kwa kukata vipande watakavyo wapotoshaji. Msingi wa mjadala huu ulikuwa utani wa hoja ya zamani ya “goli la mkono”.. uliorushwa wakati naongea ndio maana kuna kicheko kabla. Haikuwa serious version. Mimi muumini wa uchaguzi huru na haki. Vizuri tuendelee kushindana kwa hoja,”ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa X leo Jumanne Julai 16, 2024.
    Nape ameibuka kuelezea hoja hiyo ikiwa ni saa chache tangu Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla leo, aseme kauli hiyo haitokani na msimamo wa chama hicho.
    “Kuna kiongozi nimemsikia huko mitandaoni anasema eti ushindi wa uchaguzi hautokani na kura za kwenye boksi, mimi nataka nimwambia hiyo kauli isitazamwe kuwa inatokana na CCM,” amesema.
    Nnauye aliyewahi kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, alitoa kauli hiyo jana Julai 15, 2024 usiku alipotembelea soko la Kashai mkoani Kagera na kuzungumza na wananchi.
    Muktadha wa kauli hiyo ilikuwa ni kuwahakikishia ushindi wa Mbunge wa Bukoba Mjini, Stephen Byabato katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Nnauye ambaye kwa sasa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alitoa kauli hiyo.
    “Unajua nyie sikilizeni, matokeo ya kura sio lazima yawe ya kwenye boksi, inategemea nani anahesabu na kutangaza. Na kuna mbinu nyingi kuna halali, nusu halali na kuna haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi tu mkishamaliza unamwambia Mwenyezi Mungu nisamehe pale nilipokosea,” alisema.

ความคิดเห็น • 94

  • @georgempogomi7329
    @georgempogomi7329 หลายเดือนก่อน +6

    Mungu tisaidie haya majambazi uyaondoe yote kwa nguvu zako wizi wa kura na Kodi zetu

  • @mlyamalitv1789
    @mlyamalitv1789 หลายเดือนก่อน +6

    Kama kura wanaweza kuiba sembuse pesa za UMMA Hii nchi tunashida ona wanavyojikanyaga.

  • @user-xu3zm2wl3g
    @user-xu3zm2wl3g หลายเดือนก่อน +5

    Mwenyekiti wa CCM na rais asipomuondoa nape ktk Baraza la mawaziri umma utaamini hiyo ni kauli ya Baraza la mawazir

  • @ayobow56
    @ayobow56 หลายเดือนก่อน +4

    Bora yeye amesema ukweli nape nampongeza kwa kusema ukweli

  • @HUSENIISSA-d8k
    @HUSENIISSA-d8k 29 วันที่ผ่านมา

    Mungu tusaidie kuondoa madhwalim hawa

  • @nkorankoranigwa4058
    @nkorankoranigwa4058 หลายเดือนก่อน +2

    Shida Sana aise....hapa maendeleo hayawezi patikana

  • @user-vt9pl1bz6x
    @user-vt9pl1bz6x หลายเดือนก่อน

    Ningumu kuamika maneno ya nape ya ighalimu CCM

  • @ramadhanmahongole9293
    @ramadhanmahongole9293 หลายเดือนก่อน +1

    Ccm haina dhamila njema ktk chaguzi za haki na haiamini demokrasia ingekuwa inaamini ingeruhusi mchakato wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi lkn mpk sasa vyama inaingia kwenye uchaguzi hakuna tume huru wala katiba mpya kwa maana hiyo aliyo sema nape nauye ya kuiba uchaguzi ni msimamo wa ccm

  • @marianamontoedi1318
    @marianamontoedi1318 29 วันที่ผ่านมา

    Utamfundisha kuiba kura duuu bongo 😂😂😂😂😂

  • @omaryissa1821
    @omaryissa1821 หลายเดือนก่อน

    Imeongea ukweli

  • @TrinaRoman345
    @TrinaRoman345 หลายเดือนก่อน +1

    Sio urais tu nje ya Box hata uwaziri nje ya box inawezekana 😅😅😅

  • @Kwelihukuwekahuru
    @Kwelihukuwekahuru หลายเดือนก่อน +2

    Lakini Watanzania tu wajinga jamani wanashangilia uovu

  • @shaban6644
    @shaban6644 หลายเดือนก่อน +1

    Tuchunge Sana Kauli Zetu,

  • @user-cj2iq1qv6n
    @user-cj2iq1qv6n หลายเดือนก่อน

    UONGO CCM AWANA UWEZO WAKUSHINDA UCHAGUZI WOWOTE BILA KUSAIDIWA NA POLISI TUME YA UCHAGUZI WANAJESHI NA USALAMA WA TAIFA MSIDANGANYE WATU NYINYI WADANGANYENI WATOTO WALIOZALIWA MWAKA 2000

  • @user-le6jm2tf5y
    @user-le6jm2tf5y หลายเดือนก่อน +1

    Uzur hakuna anaeishi milele bas fresh

  • @MagrethKatondo-qs9oz
    @MagrethKatondo-qs9oz หลายเดือนก่อน

    Mmmmhhh ee mungu utuhurumie dhambi ya kukusudie. Lihurumie taifa letu. Tuondolee dhambi.

  • @michaelchombo8956
    @michaelchombo8956 หลายเดือนก่อน

    C.c.m halina dedemocrasia

  • @JamesRichard-q2h
    @JamesRichard-q2h หลายเดือนก่อน

    Nape ni mkweli kafukuzwa kwa kusema ukweli ndiyo yanayoendelea huko ccm

  • @johngibson3089
    @johngibson3089 หลายเดือนก่อน

    Pia Bw Nape ni vema tu ukakumbuka MUNGU sio katibu wala mwenyekiti wa CCM. Usilitaje jina lake ktk upumbavu huo

  • @user-hn7uv4yg2q
    @user-hn7uv4yg2q หลายเดือนก่อน

    pombe sio chai 😢

  • @mohdnasser3620
    @mohdnasser3620 หลายเดือนก่อน

    Mungu anawaona sijuwi atawapokea vp

  • @user-pf6yw7vh1p
    @user-pf6yw7vh1p หลายเดือนก่อน

    Huyu itakua mlevi ndio ttzo lake 1:09

  • @ndinzeissa4778
    @ndinzeissa4778 หลายเดือนก่อน

    Huyu nape.aliwahi.kusema wanaitakanccm yao walio.izowea naakafanikiwa eatu.huwa.eanayatunza maneno yenu naona mlifanmkiwa na.mkaludisha kwrli kabisa.ccm mlio izowra ila zamazama hii ni ya vijana sio nyie wezeerev

  • @SuperMukama
    @SuperMukama หลายเดือนก่อน

    Kazi ni kazi na uswahiba ni uswahiba, Yule aliyeacha kumteua alifanya hivyo kwa sababu iweje waje wengine wamteue ? Huyu si mara ya kwanza kusema hivyo tena hadharani .Ndiyo faida ya kumpa kiongozi mbovu cheo.

  • @barakamanga5502
    @barakamanga5502 27 วันที่ผ่านมา

    Kilichotokea kwa nape ndo kilekile kilicho tokea kwa ndugai

  • @hassanlikwenangu8471
    @hassanlikwenangu8471 หลายเดือนก่อน

    Bye Bye NAPE

  • @martinemaganga5253
    @martinemaganga5253 หลายเดือนก่อน

    Makala haijui CCM vizuri na muda siyo mwingi utaenguliwa

  • @Kwelihukuwekahuru
    @Kwelihukuwekahuru หลายเดือนก่อน

    Hamuwezi kushinda kwa haki ingekuwa hivyo mngeruhusu katiba mpya na tume huru ya uchaguzi isiyoteuliwa na mshindani yaani refa awe mwanachama wa timu hata akanushe afafanue Mungu amemsukuma aseme ukweli CCM wanashinda kwa giliba

  • @johngibson3089
    @johngibson3089 หลายเดือนก่อน

    Kauli ya hovyo kupata kutokea. Yani waziri anajivunia upumbavu?

  • @billgussy6099
    @billgussy6099 หลายเดือนก่อน

    Mungu hadhihakiwi kimemlamba

  • @RaymondMbogo
    @RaymondMbogo หลายเดือนก่อน

    Nothing

  • @omaryyusuph7877
    @omaryyusuph7877 หลายเดือนก่อน +1

    Kwa staili hii tanzania maendeleo tusaau

  • @ndukulusudikucho_
    @ndukulusudikucho_ หลายเดือนก่อน +1

    Wasiruhusu hata kidogo zile nyongeza ya Utumbo wachukue Nchi, Kagame ameshinda Urais Kwa 99.99 % hakuna maendeleo kwenye kelele nyingi

    • @lawimanumbu5103
      @lawimanumbu5103 หลายเดือนก่อน

      Rwanda wanaangalia kiongozi bora siyo kubadirishabadilisha ovyo ovyo

  • @EmilyMakelele
    @EmilyMakelele หลายเดือนก่อน

    Huu ni uchafuzi wa hali ya hewa. Ukiwa shushushu haya ndo matokeo yake. Mwisho wa ubaya ni aibu.

  • @GoodluckNjau-km3ym
    @GoodluckNjau-km3ym 23 วันที่ผ่านมา

    Ushaidi tosha

  • @meshmeshak1095
    @meshmeshak1095 หลายเดือนก่อน +1

    Huuu ni ujinga uliopitiliza

  • @giftkalenge418
    @giftkalenge418 หลายเดือนก่อน

    mi naona wamemuo ea kwa kuwa amesema ukweli kinafanyika huo ndio uhalisia wapinzani mnapaswa kumpongeza Kwa ukweli huo na sada wananchi wanapata kufahamu kuwa hakuna kura halali kwa wanaotangazwa hivyo mmube aje kwenu awasdidie kuwapa ufahamu zaifi wananchi

  • @scolasticamwakaje6579
    @scolasticamwakaje6579 หลายเดือนก่อน

    Ugomvi wako na mama Samia ataamua Mungu! 😮😮 Kiburi kimekujaa kaka,km ambavyo uliropoka kuwa ugomvi wako na Magufuli aliamua Mungu! Endelea kuropoka😅😅

  • @barakamanga5502
    @barakamanga5502 27 วันที่ผ่านมา

    Nape hajawahi kuwa muongo

  • @user-qn8pb9er6c
    @user-qn8pb9er6c หลายเดือนก่อน

    Kauli kama hizi zinafunua wizi unaofanyika na huishia kufanya viongozi kuuliwa na Mungu maana sio chaguo la wananchi

  • @ntegrity277
    @ntegrity277 หลายเดือนก่อน

    KAULI ZA KIJINGA SANA KUTOKA KWA WAZIRI TENA KIONGOZI MKUBWA USELESS STATEMENTS CCM NI TAABU KATIKA NCHI HII

  • @AlfredRutaguza
    @AlfredRutaguza หลายเดือนก่อน

    Yaani huyu ni kiraza wa mwisho hapa tanzania

  • @SuperMukama
    @SuperMukama หลายเดือนก่อน

    Anam dhihaki MUNGU

  • @isackdanford8531
    @isackdanford8531 หลายเดือนก่อน

    Hao wanaoshabikia akija Nape utawaskia wanasema tena ndioooo semaaaa waambieee haoooo

  • @AbdulhaamidSoud
    @AbdulhaamidSoud หลายเดือนก่อน

    CCM ni chama cha Magizi sishangai kwa nape kunya hayo leo wameiba nakuuwa na wataendelea nampa mauwA yake🎉🎉🎉🎉

  • @AshaMwamba-g3l
    @AshaMwamba-g3l หลายเดือนก่อน

    Tunajuwaa mnaanza kutowaaa sirii sisi tunapajuwaaa

  • @AbuJunaidi
    @AbuJunaidi หลายเดือนก่อน

    Kashamuibia mama samiya pesa za kutosha

  • @ceciliaonyango5367
    @ceciliaonyango5367 หลายเดือนก่อน

    Huo ni ujinga maana kiongozi anatoka kwa Mungu TU hao mnaotuwekea ni majambazi acheni hii nchi

  • @SalehMwiru
    @SalehMwiru หลายเดือนก่อน

    Umetuangusha mwana ccm mwenzetu,au kirus

  • @johnmwita221
    @johnmwita221 หลายเดือนก่อน

    Hiyo ni kuwadharau WATANZANIA.

  • @michaelmagwaza-bc6mk
    @michaelmagwaza-bc6mk หลายเดือนก่อน

    Viongozi wa Dini Cpct, Bakwata, Jukwa la Wakristo, Cct, N.k Mko wapi.? Au mnasubiri uharibifu ndio muitishe Maombi.?

  • @LusunguLupenza-lf7fk
    @LusunguLupenza-lf7fk หลายเดือนก่อน

    "Kauli hiyo ipokelewe sio ya chama cha mapinduzi"
    Elewa body language na ujumbe unaowasilishwa

  • @MehmetMtonga
    @MehmetMtonga หลายเดือนก่อน

    Afaikwa kauriyakenivema ametenguriwa

  • @ZakayoReuben-ow9tz
    @ZakayoReuben-ow9tz หลายเดือนก่อน

    Hivi mimi leo ninamakampuni ya simu 5 kama yake vile

  • @albertasukile477
    @albertasukile477 หลายเดือนก่อน

    Mbona anawapa points wapinzani? Anadhihirisha Nini, kweli mwache Mungu nje ya hili

  • @frankpeter-of8xp
    @frankpeter-of8xp หลายเดือนก่อน

    watu wanashangilia uovu watz tuna safari ndefu sana

  • @Gibson-d3m
    @Gibson-d3m หลายเดือนก่อน

    300m ni pesa ndogo! 😢😢

  • @PeterNMzee
    @PeterNMzee หลายเดือนก่อน

    MUNGU ananamna nyingi za kuwa weka wazi majambazi

  • @andrewkissava9184
    @andrewkissava9184 หลายเดือนก่อน

    Makala acha utapeli na mpongeza nape kwa kusema ukweli ccm siku zote huwainashinda kwa hila ,giliba na kuiba kula na kutamgaza wasio shinda na walioshinda ndo wana ambiwa hawajashinda

  • @samsonsimon3138
    @samsonsimon3138 หลายเดือนก่อน

    Kila kitu wananchi wa tz ni kushangilia tu hata kma cha upumbavu bila kujitathimini ugumu wao wa maisha , sasa kma mtu ameongea hvo atashidwaje kuiba mali za nchi , wameiba mali za nchi kupitiliza kiwago hadi amejisahau kabxa anaona chochote anachoongea ni sawa tu kwake

  • @fatumadrosin996
    @fatumadrosin996 หลายเดือนก่อน

    Mbona tunajua ona wanavyo jikanyanga mambo hazarani 😅😅😅

  • @benedictmrisho1800
    @benedictmrisho1800 หลายเดือนก่อน

    Ukiona watu wanashangilia uovu ujue dhuluma imekomaa. Uwongo hadharani ukishakuwa sio kosa hadharani iko shida.

  • @samsonsimon3138
    @samsonsimon3138 หลายเดือนก่อน

    Watu wajinga kweli tenah wananchi wa hali ya chini wanaishi maisha magumu hawajui hata ugumu wao wa maisha wanabaki kushagilia tu uchafu uliongelewa na upumbavu kma hao

  • @PartySekemi
    @PartySekemi หลายเดือนก่อน

    Umejikanyaga

  • @ayobow56
    @ayobow56 หลายเดือนก่อน

    Mbwa Hawa ole wao nitawale Mimi ata ubunge

  • @uraiatv8455
    @uraiatv8455 หลายเดือนก่อน

    Hapa mwananchi wameandika nini?

  • @user-qb6dx2kv3z
    @user-qb6dx2kv3z หลายเดือนก่อน

    Mipango ya majambazi wa lasirimali za nchi yetu ndo mbinu wanazo shindia

  • @MehmetMtonga
    @MehmetMtonga หลายเดือนก่อน

    Kweri ametowa siliya chama atolewe

  • @magesamstiko3182
    @magesamstiko3182 หลายเดือนก่อน

    hakuna lolote hapo analotetea ,,Nape sio kichaa kua aliongeaa kwa bahat mbaya bali ni namna ambavyo Mungu anawaumbua waovi wanajitaja wenyewe

  • @ndinzeissa4778
    @ndinzeissa4778 หลายเดือนก่อน

    Mjijuwa ila.gz ya sasanhailali inawangoja mnawaumiza sana eatanzani mumbe mpo hapo.miaka yote k3a udanganyifu watanzaini wanawangoja keani kali zimeisha toka.hakunanea.kulaumiwanmazuzu hawpo.k alne hii

  • @evelynmwaimu-vd9jo
    @evelynmwaimu-vd9jo หลายเดือนก่อน

    Aibu hii ccm mtaiweka wapi looo

  • @jameskunogoleka5805
    @jameskunogoleka5805 หลายเดือนก่อน

    Ona xx watu wetu et tumetuma kwajili ya wananchi

  • @ayobow56
    @ayobow56 หลายเดือนก่อน

    Magufuri ndio aliyatowa haya majinga

  • @paulmadundo8084
    @paulmadundo8084 หลายเดือนก่อน

    huko ndani kadri muda unavyosogea shetani anazidi sogelea sebure, hatari sana hii.

  • @matatamatatatours3237
    @matatamatatatours3237 หลายเดือนก่อน

    Huyu jamaa kauli zake hazieleweki
    Labda anaongea akiwa amepasha kichwa
    Hii ni mara ya pili

  • @amotvtz1302
    @amotvtz1302 หลายเดือนก่อน

    Laana zinawatafuna mnaanza kuropoka

  • @jameskunogoleka5805
    @jameskunogoleka5805 หลายเดือนก่อน

    Do yenu maccm

  • @kagombaEnok
    @kagombaEnok หลายเดือนก่อน

    Acha kupiga makelele wewe Makala Ccm haijawahi kushinda kwa haki Nape mwenyewe amesema

  • @yusuphitambu3405
    @yusuphitambu3405 หลายเดือนก่อน

    Uteuzi

  • @mudhihirugara8845
    @mudhihirugara8845 หลายเดือนก่อน

    Niaibusanna yani wazili mzima unasema hivyo basi wana inchi hakunasababu yakwenda kupigakula

  • @SmilingCityMap-xb9md
    @SmilingCityMap-xb9md หลายเดือนก่อน

    Hawa ndio maadui. wa taifa letu waliojificha nyuma ya kivuli cha uongozi wanaoizamisha meli yetu tz

  • @meshmeshak1095
    @meshmeshak1095 หลายเดือนก่อน

    We ni mgeni huyo mwenzako ni mtaalamu wa goli la mkono na ni mwizi na huo aliongea ndo ukweli.

  • @user-qb6dx2kv3z
    @user-qb6dx2kv3z หลายเดือนก่อน

    Sorry ni kura

  • @johngerald4677
    @johngerald4677 หลายเดือนก่อน

    Mbwa mkubwa uyo nape kenge kabisa

  • @smallscaleminingsupplies9670
    @smallscaleminingsupplies9670 หลายเดือนก่อน

    Ila watz hata hawajielewi watu wanapjga makofi kabisa kwa upuuzi huyu jamaa anaongea

  • @deniccgabriel6153
    @deniccgabriel6153 หลายเดือนก่อน

    CCM ndio kazi yenu kwani CCM imedumu kwenye wizi wa kula mfano JPM alipitisha viongozi wabila kupingwa.,

  • @noellema9109
    @noellema9109 หลายเดือนก่อน

    Wizi uwo sipigi kura sina muda huo kwani kauli zipo wazi, mimi akuna ninachogombea, bakini na siasa zenu