UJUMBE "NITATOKAJE HAPA ?"
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 10 ก.พ. 2025
- Ujumbe NATOKAJE HAPA ni moja ya jumbe za baraka sana ambazo zimekuwa zikirushwa mubashara kila Jumamosi na Jumapili kwa wiki kupitia Redio maarufu Visiwani Zanzibar ambapo mtumishi wa Mungu ambaye pia ni Mchungaji kiongozi Pastor Samson Masasa wa Kanisa la EAGT KIDIMNI CHRIST`S SANCTUARY amekuwa akihubiri na kuombea wote wenye shida mateso na vifungo kwa jina la Yesu Kristo, wengi wamekuwa wakiponywa na kufunguliwa kutoka katika vifungo na mateso ya shetani na magonjwa.
Kipindi hiki ni mwitikio wa nidhamu na heshima kwa Agizo Kuu na Takatifu sana la Yesu Kristo kwa Kanisa lake dunia nzima na kwasababu hio sisi Kanisa la EAGT Kidimni Christ`s Sanctuary tuliopo Zanzibar tumeitikia Agizo hilo kuu kwa kukuletea Kipindi cha INJILI KWA ULIMWENGU kila siku ya Jumamosi kupitia Redio mbili nazo ni Bahari FM 97.3 kinachoanza saa kumi na mbili jioni hadi saa moja usiku . Lakini pia tunakuwa hewani tena Jumamosi hio hio kupitia ZENJ FM 96.9 kila saa mbili usiku hadi saa tatu usiku na pia tunakurudia tena siku ya Jumapili kuanzia saa moja asubui hadi saa mbili asubui kila wiki kupitia ZENJ FM Redio 96.9.
Kupitia kipindi hiki watu wengi wamefikiwa na Ujumbe wa Neno la Mungu na kuokolewa kutoka katika maisha ya dhambi na utumwa na laani za ibilisi na kufunuliwa Upendo na Neema ya Ajabu ipatikanayo kwa njia ya Wokovu na utii kwa Neno la Mungu kwa BWANA na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Kazi hii yote inakujia kutokana Agizo takatifu la BWANA na Mwokozi wetu Yesu Kristo aliloagiza kutoka katika Kitabu cha MARK 16:15-20.
Marko 16:15-20
'" Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihuribi Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa . Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha , hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya." Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu " Nao wale wakatoka , wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]
Karibu sana na utabarikiwa na kujengwa sana, sana .
By Pastor Samson Masasa
Amen