TCAA YAZINDUA MFUMO WA UTOAJI WA VIBALI KWA NDEGE ZINAZOTOKA NJE YA NCHI
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 23 ม.ค. 2025
- Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezindua mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa vibali kwa ndege zinazotoka nje ya nchi na kutua ama kupita katika anga la Tanzania.
Mfumo huu unarahisisha maombi pamoja na utoaji wa vibali kutoka masaa 48 ya awali hadi masaa mawili. Vilevile mfumo huu unampa nafasi muombaji wa vibali kunakili na kutoa nakala ya kibali chake popote alipo. Mfumo huu umetengenezwa na wataalamu wa ndani wa Mamlaka.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006).
Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege.
Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba