RC CHACHA ATINGA AIRPORT TABORA-ARIDHISHWA NA MRADI WA UPANUZI WA UWANJA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 7 ก.พ. 2025
  • #CgOnlineTv
    Mkuu wa mkoa wa Tabora, Paul Chacha amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege TABORA ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
    Akizungumza baada ya ziara ya ukaguzi wa mradi huo mkuu wa mkoa Paul Chacha amesema amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo na kuwapongeza wasimamizi wa mradi huo kwa kazi nzuri wanayoifanya.
    Chacha amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya uwekezaji huo mkubwa na akisema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Tabora.
    Naye muhandisi mshauri wa mradi huo Vicent Akaro amesema mradi umefikia asilimia 57.8 ya utekelezaji wake na kwamba wanaamini watafikia lengo la kukamilisha mradi huo kwa wakati.
    Kwa upande wake meneja wa TANROADS mkoa wa TABORA, Mhandisi Raphael Mlimaji amesema jengo la abiria linalojengwa katika mradi huo litakua na uwezo wa kuhudumia abiria 120 kwa wakati mmoja.
    Mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege Tabora unahusisha ujenzi wa uzio wa kilometa 6.25, jengo la abiria na packing yenye uwezo wa kupaki gari 24 kwa wakati mmoja.

ความคิดเห็น •