TCAA Yatunukiwa Cheti cha Ukusanyaji Kodi Bora na TRA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 23 ม.ค. 2025
  • Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imetunukiwa cheti na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),ikiitambua TCAA kwa ukusanyaji kodi mzuri.
    Cheti hicho kilikabidhiwa kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa TCAA Bw. Teophory Mbilinyi. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mhe.Nape Nnauye (MB), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
    Halfa ya Tuzo za Walipa Kodi bora wa mwaka 2021/22 iliyoandaliwa na TRA imefanyika usiku wa tarehe 17 Novemba 2022 katika ukumbi wa Johari Rotana, jijini Dar es Salaam.TCAA imetambuliwa kama mkusanya kodi mzuri katika Mkoa wa Ilala.
    Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006).
    Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege.
    Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba

ความคิดเห็น •