Sizonje - Mrisho Mpoto ft Banana Zorro (Official Video)
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 7 ก.พ. 2025
- Nyimbo Mpya ya Mwaka 2016, Sizonje.
[Kibwagizo - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
[Bridge - Banana Zorro]
Tulikaa barazani, tukasikia kelele
Kelele toka ndani, mtu anaruka dirishani
Sizonje, karibu nyumbani kwetu
Uone maajabu ya nyumba yetu
[Verse 1 - Mrisho Mpoto]
Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu,
Tulipoficha mundu za kupondea wezi,
Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya?
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne,
Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango,
Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili,
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea,
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni,
Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako
Wanashangaa mbona ghafla
Samahani sana mgeni
Wapishi wameniomba kwamba
Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba
Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje
Sizonje chumba hiki naomba usiingie
Ukimaliza nitakwambia kwanini
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa
Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa
“USIYEMTAKA KAJA”
Hatukuwahi kuelewa maana yake
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia
[Chorus - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
[Verse 2 - Mrisho Mpoto]
Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto
Na kamwe mtoto hawezi kuungua
Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi
Njoo huku uone Sizonje
Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue?
Sawa, Sizonje, huu hapa ni ua
Lile pale ni shimo la taka
Na kile pale ni choo
Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi
Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka
Wala kwenda chooni
Kama ukiwa makini
Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu
Wengi ni vijana, wana bahasha za khaki mikononi
“KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?”
Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje
Kuna watoto, wazee na kina mama
Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele
Ninavyosikia, ila sina uhakika
Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao
Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki
Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni
Uone maajabu mengine ya nyumba hii
Sizonje, ukiona tembo anaringa
Ujue mvua zinakaribia
[Chorus - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
2025 huu mwaka tunategemea sana nyimbo zako,,, ganga like nying km mpo pamoja na mimi
huu wimbo ulikuwa special to MAGUFULI..Rest in paradise our icon 🕯🕯😭😭
Nyumba ni nchi,kwa nje inatafsirika na kuonekana ni maskini ila ndani ina utajiri mkubwaa,ila inaibiwa na manyemera wanaopita njia za panya kuiba rasilimali zetu, pia undugunization kwenye ajira ni tatizo,afya za kina mama na watoto,uchumi,rushwa na uwajibikaji ila sizonje ushafika umekomesha hayo yote. Hongera sana sana Mrisho na hongera kwa Sizonje.
Leo ndio nimeielewa atari sana uyu jamaa
Hongera mrisho, ila bado mwendo hujaumaliza endelea kuwa kumbusha wenye dhamana , hakika bado tunakuhitaji.
Elenzea zaidi tafadhali
duuuuuuh kumbe ndo nimejua leo hii maana ya wimbo huu
Asante kwa tafsiri yako ndugu from 🇰🇪 🙏
nyimbo hii ulimuimbia maghufuli nae akaskia sauti yako akawaadhibu wadhalimu hadi wakaanza kupitia mlangoni r.i.p maghufuli tutakukumbuka milele
Ila mpoto I nyimbo nimekuja kuelewa leo trh 5-3-2024😂😂😂
Inamaanishi nini kwani? Mimi bado naangaika
Hongera kijana
Mm cjaelewa bado
Bila akili ya ziada kwa mrisho mpoto hutoki na kitu njooni tuungane jaman gonga like hapa kama umeikubali hii
Duuuh miaka nenda miaka rudi leo ssa ndonimeelewa maan ya huu winbo
MLANGO UPO WANAPITA MADIRISHANI.... ..kwamba Kuna utaratibu wa kufikia jambo fulani Ila watu hutumia njia za mkato(rushwa) kupata jambo hilo.....SHIMO HALITUPWI TAKA WALA HAWAENDI CHOO... maana yake Kuna mfumo wa watu kustaafu Lakini Kuna watu hawaachii nyazifa na pia kuna kazi fulani hivi zimekuwa za koo fulani wanarithishana kutoka kwa baba then mtoto hatimae mjukuu mfano(benki kuu) na hivyo kusababisha vilio vya vijana wengi wasomi kuzunguka na bahasha kwa kutafuta ajira na ajira hamna.......This is the best literature song I ever meet. Good work for this guy
Asante kwa kufafanua kidogo nadhan umesoma kiswahili vzr
Sikuachwa nyuma sana katika fasihi
Nakubaliana nawe Jodasonu kabisa, the best oral lit, of modern time, big up MPOTO.
Jodasonu Davis yani huko benk kuu ndio ucseme watu wapitishana tu msemo wao hpa kaz tu
Asante kwa kunifafanulia
Tutolee nyimbo nyingine nzuri kama hii Mrisho! Asante kwa kutufundisha Kiswahili na utunzi!
Mashairi Yako natamani watoto wetu wayasome shuleni!
Hakika huyu ni Artist❤ mbobevu na gwiji la Mashahiri yaliyosheheni Ujumbe mzito kwa Jamii Ni style ya Wimbo usio na Vionjo vya Tamaduni za nje Wimbo huu umebeba maisha yetu kupitia mila,desturi na Tamaduni zetu Hongera Msanii Mwamba Mrisho Mpoto
Mjomba Tanzania imekumiss sana. Tunaamini bado unatupenda yapo mengi tunahitaji utusemee hasa ktk wakati huu.
Tangu apewe kipande cha keki saut haitoki tena
Mrisho mwalimu wako wa kiswahili alikuwa anapata shida saana kwa kukosolewa na wewe 🙏🏽 amen
😀😀😀😀
Nampnda mpka bac huyu kaka mola ampe umri mrefu wenye kheri ishllh
@S Sur AMINA
Pamoja na hayo mjomba Mpoto,leo hii nikiwa natokea kwenye kilele cha sherehe ya kilele cha miaka mia moja ya vita kuu ya Dunia ya kwanza! Mjomba Mpoto nimelazimika kutumia au kuiba jumbe zako hizi kwa mapenzi na ujumbe sahihi kwa wakati mwafaka hasa hapa kwetu Zambia!
Mjomba Mpoto utaniwia radhi kwakweki mjomba uliwahi kuniliza enzi za awamu ya nne ya Mzee wetu Dr. wa Ukweli wa Msoga, niliwahi kulia na kucheza sana pala LUGOBA!ulikuwa wimbo Adela,na Sasa hivi SIZONJE huu si tu ni wimbo ni FASIHI KALI!!!!. Wewe kweli ni aina ya akina Shaban Robart
Kama unamkubari mrisho mpoto gonga like hapa
ukiisikiliza mankini itailewa 2..hongera. mjomba coz umenifanya ninitulie xanaa kukusikiliza Na kufafanua..wakuache jomba..nakusikiliza. mwana Kenya nikiwa saudia nimetua mankini..
Kama umesoma sana vitabu vya Hayati Shabani Robert,hakika hutokuwa na kazi kubwa ya kumuelewa Mpoto.
SIKU ZOTE MWENYE HEKIMA HANUKI MDOMO NA MWENYE AKILI HASEMI NDANI YA MAJI.... HESHIMA KWAKO MR MPOTO NATAMANI NIJIFUNZE ZAIDI TOKA KWAKO.
Mwenye akili ndogo hawezi elewa nyimbo zako but wewe ni zaidi ya msaniu hapa afrika na natamani siku nikukumbatie kwa furaha. U are the best mjomba
Nakukukubali sana mtaalamu Mjomba, kazi zako huwa zina nipa shida kuzielewa lakini huwa nakuelewa taratibu. Ninahisi hakuna kazi niliyowahi kukuelewa kwa 100% maana kila nikirudia kusikia wimbo fulani huwa naongeza kitu fulani kutoka humo! Wewe ni Shaaban Robert wa pili kwakweli, yapasa nawe uandike kitabu cha KUSADIKIKA kama mzee Shaaban, sijui utakiita SIZONJE....., au NYUMBA YETU!
Sizonje ni jina la HAYATI JOHN POMBE MAGUFULI,alilopewa na Ndugu yetu msanii Mrisho Mpoto.Nyumba ktk wimbo huu ni IKULU YA RAIS MAGOGONI Dar es Salaam.
Wimbo huo ni wazamani mno hata kabla ya huyo magufuli hajajitambua kabisa
@@JoshuaLyalukiloAliutoa wakati magufuli ndo kaingia madarakani…nyumba ina vyumba 4 means awamu nne
Usiyemtaka kaja (Magu km Magu)
Mrisho Unajitahidi sanaaaa kusema kweli nazipenda nyimbo zakooo hasa Sizonje,kitendawili,nikipata nauli,Waiteee nk
My all time Tanzanian Artist..love from🇰🇪
Kaka hongera sana kaka, nimeielewa sana nyimbo hiii, hasa choo kipo lakini hakitumikiiii. Unatisha kaka.
Ila huyu mzee phana nasikilizaga nyimbozake lakn hii mh katumia methali tupu aisee safisana
Huu wimbo nimeusikiza Mara 7 sai
Mjomba juu wimbo unamafundisho saana
Siku hizi mrisho mpoto haimbi tena
Asali ni tamu mkuu
Mrisho shujaa shujaa shujaa,saluti kwako,mimi ni mkenya anaefurahia kazi yako nzuri mungu akubariki
Dah!!na mkubali sana mrisho miaka 7 imepita nasikia wimbo huu ila leo ndo mmeelewa sahihi ya wimbo huu
Mjomba hapa Kenya unapendwa kakangu
Apo Godfather au nenene? bonge la kichupa straight to Urban top Ten
Mjomba tumemiss mashairi yako, come back legend
daah kwa sisi tuliosoma arts aisee mzee mpoto unatisha baba angu.....nakutamani san katik matumizi ya lugha na hasa lugha ya picha kikubwa zaidi ni hiyo nyumba yaudongo lakin ndani noouma!! bila shaka watanzania waliotazama video hii wamejifunza kitu, binafsi sanaa yako sio tu kiburudisho kwangu maana najifunza mengi san na ni miongoni mwa mhimili wa utamaduni wa nchi yetu! unaimba kwa kusoma upepo unavyovuma ila ulituomba nauli ili uwende kwa mjomba na je sizonje ni naniiiiiii?
this guy is marvellous... your Tanzanian fan from Australia
We are together
nmeelewa kidogo,anamkaribisha maguful ikulu(nchi yetu)....asiye mtaka kaja hahaha I like this ....japo mafumbo n mnge
Kiongozzzz unajua sana ,sasa sijajua umesoma kiswahili sana au mimi ndio btplms
Mhhh ngoja niseme ukweli tuuu. Ni miaka 3 now nasikiliza nyimbo za huyu jamaaa cjawai elewa anae elewa anielekezeee
Amemaanisha kuwa nchi inaonekana masikin wakati ndani yake inautajir tena amemaanisha sheria ipo lkn watu wanatumia njia ya mkato ameelezea mambo mengi
Mjomba, kwa kweli nyumba za Africa mashariki zina mambo na maajabu, zaidi hapa Kenya.
one of the best video and nice message to Tanzanian. kazi nzuri Mjomba endelea kuelimisha ,kufundisha na kukosoa jamii
Sizonje naipenda mnoo sichoki kuiangalia wallah love u bro mrisho ❤️❤️❤️❤️❤️ kazi nzur sanaaaa👌👌👌👌👌👌
@@rashidikufinyu444 pouwa
Wakati leo nasom kiswahil ....mwalim wanv kantolea mfano wa mwanafasihi anaetumja lugh y fasihi kufikish ujumb ktm jamii....ndipo akntajia huu wimbo ....hap nmeelewa kwann mrisho umeamua kutmia lugha hii....hongera sana
Mjomba umetulia Sana. Tupe mashairi baba🔥
Huu ni usanii wa hali ya juu.Utumiaji wa kejeli ilikupeana ujumbe flani.
sizonje hii ndiyo nyumba yetu ingia uyaone hapa anaizungumzia tz yetu jinsi watu wanavyopenda rushwa na kurisishana madaraka na wakat kila mtu ana haki
Long live Mrisho mpoto. Nimekuelewa vzr mnooo. Mfumbie mtoto mkubwa ang'amue
2024 eeeeeh 🔥 "MASTERPIECE"
Usiyemtaka kaja, sizonje huyu huenda akawa ni JPM aka Jembe aka Chuma cha Pua, siyo lazima niwe sahihi kumtambua Sizonje kwenye ghani hii ya Mrisho
Who else is still here in 2019
A true Patriot, maisha marefu
Weng ni vijan na wanabahasha za kaki mikonon daaaaah nimeelewa sana nakupend sasa mpot ii ndo nyumb yetu TZ ingia uyaone
Kile ni choo wanaoish hawajawai kukitumia mean hospital zipo ila wanaenda nje hahahahahahaha
😍💞💕😘💜👏👏👏
Hii nyimbo iliimbwa na watu wenye IQ kubwa
Nyimbo ngumu sana kuielewa inahitaji utulivu wa kutosha
upenda Wangu nimependa kilakitu wanao sema sinzuri wajaribu nawao tuona zao zitakuaje
Wale WA 2023 tuktane
mtoto hawezi kubembelezwa kwa wimbo mbaya,na mtoto aungui na kiazi kilchopo kwenye kiganja cha mama yake,nimekusoma mjomba
nimeilewa asee...mashairi yanaeleweka kiasi! HII NDO TANZANIA
Hekima kaka safi sana
yan nimeskiliza zaid ya 10 tym sijaeleza zaid ya bahasha za kaki2...daaah shkaaaaamooooo burazaaaaa
hahaha kwel mtoto hawez kuungua kwa kiaz kilichopo kwenye kiganja cha mama yake ahsante sana
Wewe ni mwalimu , kazi zote zako hujawahi kosea
Nyimbo nzuli kweli uko posh kak kimziki nakupa respect
uliye post coment hapo juuu kuwa hujaelewa nyimbo .hujui nyimbo..
unavamiavamia tuuh ..imba wwe bac ueleweke
Daaaaaaah mjomba ulisomea wapi kiswahili chako maana hayo mashairi yako hakuna anaeyaweza duuu big up sana mziki wako ni wa kibantu zaid
Kiukweli wimbo umetulia una ujumbe wa maana sana.ukionesha kwamba tuwe na nguvu na kupambana
ahsante brother Mpoto
Huyo mzee anavyo Lia na mimi nimelia mmh!sizonje
Artist is more beautiful because one thing can bring different meaning and understanding as what it is in this song of. Sizonje salute mrisho mpoto
huyu hanscana ni director anayejielew pengine kuliko wote kwa sasa young but a real inspiration in music industry
Nimeingia nami nimeyaona maaaajabu ya nyumba yenu I say...great poetical pieces. Wengi waaalewa maaana ila kwa vile ina wachoma basi wanajifanya kutoelewa I say. He heeeeee.
Wana fasihi tupo tunakuewaga sanaaaa Asante MWL wanguu wa kiswahili MWL MACHUMU, MWL Alexander na PRISCA Bila nyie mm nisingejuaaa ujumbe wa mpoto Mbarikiwe sanaaa
aisehhh hii nyimbo ni hatari, xijui km ntakuja kuisikia nyimbo km hii tena
bonge la kazi kaka na kwa upande wa video ipo poa ile mbaya.
hongera Mjomba mi huwa nakuelewa sanaa nice song babaa
Mlisho kwangu hata usipoimba, kitendo cha kukuona nahisi nguli na gwiji la sanaa anajambo analitoa
duuh! maishairiii nondo sana
hehehe yes yes mr
nazipenda kazi zenu safi sana wanaTanzania... mwatufunza maadili mema ya upendo sis kama wakenya
lakini wote tu waafrika na hivyo nafurahia kazi zetu,, hongera sana
Asante sizonje, Kwa sasa wenye nyumba tunalala vyumban piah, Magufuli Oyeeee! Bahasha za kaki tu ndo bado ila karbu tena 2020, ulitatue na hlo! Kwa sasa hawapt madrishan tena,
Hatari sana
Genious sijawahi pata ona
Dah! Kwakweli mashairi yamesimama sana. Hongera Mrisho kwa mashairi haya
Maudhui, mashairi, rekodi,... Nimeipenda. Ahsante sana Baba Mrisho Mpoto.
Oooh Woookey Burhoney Wa Mponda Ha Hha Somehow Umenipa Idea
Naikubali xn hii ngoma🔥🔥🔥🔥👌🏻👌🏻👌🏻👌🏻
nakukubari sana mpoto aka MJOMBA mngu akubariki endelea kuwambia wana sizonje
Alaaah! Mrisho wanidekua kwa mishororo na ushairi wako kila tungo lanijenga ajabu. mie nasoma sana fan wako mpya hapa toka Kenya.
Ana kiazi cha moto mdomoni ataimbaje sasa
Mbona mrisho haimbi tena..
PongeZi pia kwa director aise ameitendea haki hii ngoma
I love the patriotism in this guys music,
Yuliopo hapa 2020 tupia like
African have to proud of our culture.we are top
nakubali Sana'a Kaz za mjomba nyimbo ujumbe Kwa waelewa
"Najua, wimbo mbaya haufai kumbelezea mtoto,
Na kamwe mtt hawez kuungua kwa kiaz kilichokua kweny kiganja cha mama yake mzazi,
Njoo huk uone sizonje
Siunajua, harufu ya uzaz haiish mpk mtt akue?
Haa haa haa daahh mpoto unaandk xn, hongr xn kwa uandsh Mzur, nazkubal xn nyimbo zko
✋✋✋✋
Tanzania inaonekana masikini ndani nitajiri hyo ndio jambo nimeona
mrisho mpoto kwa hakika nyimo zako za burudisha hasa katika matumizi la lugha yetu teule kiswahili
kiukweli hii nyimbo huwa ninaipenda . sana
we unayesema amealibu au angemuonesha sizonje auna uelewa kumbuka wimbo uu ni fumbo akikuonyesha sizonje utaelewa yeye mpoto anatupa mtiani tumjue sizonje ni nani kua mwelewa sio unakulupuka kuongea tu au unadhani mpoto ni sawa na wale wa mpenzi nakupenda
Johanness Hornest
Mbona hote mnabaki jujuhu majela yamejengwa lakini wafisadi wakubwa ambao wangefaha watupwe na kuozea huko kama kinyesi kinavyo hozea chohoni awatupwi huko.
Wasomi wanaho maliza awapewi kazi wanashinda waki zunguka mahogisini lakini awapati milango.
Sizonje niserekali na nyumba ni inchi.
Sio Tanzania tu Africa yote.
hii ngoma bhana ni balaa
Yaani nyumba yetu kwa nje ni mbaya sana nayakizamani mno ila ukiingia ndani ndo utajua uzuri wake najinsi ilivonakshiwa kwa mapambo ya gharama na ustaarabu uliotukuka
Imemaaanisha mbuga za wajama na dhahabu tulizonazo na maziwa
Imemaaanisha mbuga za wajama na dhahabu tulizonazo na maziwa
Nkukubali sana mkubwa hongera huna spair
video ni nzuri, tuendelee kumpigia kura tuzo ya kola! wonderful video,
Yes Leonard!
Mjombaaa, Banana kazi nzuri sana, ni pekeee
madhumuni nimeyapata