Tenzi za Rohoni No 129 - Karibu Na Wewe

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 28 ก.ย. 2024
  • Lyrics: Karibu na wewe
    1. Karibu na wewe,
    Mungu wangu
    Karibu zaidi,
    Bwana wangu
    Siku zote niwe
    Karibu na wewe,
    Karibu zaidi
    Mungu wangu.
    2. Mimi nasafiri
    Duniani,
    Pa kupumzika
    Sipaoni,
    Nilalapo niwe
    Karibu na wewe,
    Karibu zaidi
    Mungu wangu.
    3. Na kwa nguvu zangu
    Nikusifu;
    Mwamba, uwe maji
    Ya wokovu;
    Mashakani niwe
    Karibu na wewe;
    Karibu zaidi
    Mungu wangu.
    4. Na nyumbani mwa juu,
    Baba yangu,
    Zikikoma hapa
    Siku zangu,
    Kwa furaha niwe
    Pamoja na wewe,
    Karibu kabisa
    Mungu wangu.
    Tenzi za rohoni, Wimbo wa tenzi, hymn songs
    Tenzi za Rohoni No 129 - Karibu Na Wewe

ความคิดเห็น •