Pastor Fred Msungu - Vita vya Kiroho
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 16 ต.ค. 2024
- VITA VYA KIROHO
( WAEFESO 6:12 )
Moja kati ya masomo tata , lakini muhimu sana kwenye mwili wa Kristo ni hili somo la vita Vya kiroho .
Kweli Muhimu
Vita ya Kiroho ni halisi
Uwe unakubali au haukubali , vita ya kiroho ni halisi . Kwa sababu uliwengu huu unaratibiwa rohoni sio mwilini
Kila mwamini , yupo vitani
Iwe unajua au haujui, lakini siku uliyotangaza tu hadharani umeokoka , ni siku ambayo ulitangaza vita kwenye ulimwengu wa roho
katika somo hili utajifunza vita ya Kiroho ni nini ? Inapiganwaje ? Na uwanja wa vita hii uko wapi.
Lakini utajifunza kwa nini kwa watu wa Mungu kumekuwa na ugumu na upinzani sana kupenya na kufanikiwa ? Pia utapata namna ya kutoka na kufanyika kuwa mshindi kwenye kila unalo lifanya .