TFS UYUI WAPEWA MAAGIZO MAZITO /MAGARI 5 YADAKWA YAKIWA NA MAZAO YA MISITU KINYUME NA UTARATIBU

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 28 ส.ค. 2024
  • Jumla ya magari matano yamekamatwa wilayani Uyui mkoani Tabora yakiwa na zaidi ya magunia ya mkaa 200, mbao pamoja na nguzo yakidaiwa kukiuka taratibu za vibali na kuvuna mazao ya misitu bila kufuata utaratibu.
    Kufuatia suala hilo Mkuu wa wilaya ya Uyui Zakaria Mwansasu ametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaokiuka taratibu za vibali huku akisema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao
    Pia MWANSASU ameagiza wakala wa misitu Tanzania-TFS wilaya ya Uyui kufanya kazi kwa weledi bila kumuogopa mtu yoyote.
    Muhifadhi misitu wilaya ya Uyui Majaliwa Maginga amesema watahakikisha wanafanya doria za mara kwa mara ili kuwabaini na kuwakamata wanaokiuka sharia za uvunaji misitu.
    Operesheni hiyo ya kufuatilia wanaokiuka taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu wilayani Uyui imeanza wiki ya mazingira mei 29 mwaka huu ikiwa na kaulimbiu isemayo "urejeshwaji wa ardhi iliyoharibiwa, ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame"
    #uyui #tfs #misitu

ความคิดเห็น •