PUTIN ATOA KAULI SHAMBULIZI LA KAZAN, AAPA KUWA UKRAINE…….

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ก.พ. 2025
  • RAIS wa Russia, Vladimir Putin amesema walioratibu mashambulizi ya ndege za Droni kwenye majengo yaliyopo mjini Kazan siku ya Jumamosi kuwa watajutia uamuzi huo.
    Rais Putin amesema Russia haitokaa kimya kuhusiana na mashambulizi hayo ambayo yalisababisha uharibifu wa miundombinu na kudai kuwa vikosi vyake vitalipiza vikali hivyo Ukraine ijipange kuona majibu yake muda wowote.
    “Yeyote na kivyovyote wanavyojaribu kuiharibu Russia watarajie kwamba wao watapata madhara zaidi kwenye taifa lao kutokana na kile wanachojaribu kufanya katika taifa letu,” alisema Vladimir Putin jana Jumapili.
    Putin pia alimhakikishia kiongozi wa Mkoa wa Tatastan lilipo eneo la Kazan ambapo yamejengwa majengo hayo, Rustam Minnikhanov, kuwa yatafanyiwa matengenezo makubwa na shughuli za Umma zitarejea kama awali.
    “Ninauhakika kwamba mamlaka za eneo husika zitashughulikia suala hilo kwa ukamilifu kutokana na uharibifu uliofanywa na maadui zetu,” alisema Putin alipozungumza kupitia video wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usafirishaji nchini humo.
    Shambulio la Ukraine eneo la Kazan Disemba 21, lilisababisha uharibifu wa majengo ya makazi na sehemu ya kiwanda japo mamlaka zilidai kwamba hakuna madhara yaliyosababishwa na mashambulizi hayo ya ndege zisizo na rubani kwa binadamu.
    Maofisa wa Serikali walitoa taarifa kwamba Droni nane zilipiga maenel mbalimbali ya Mji wa Kazan Mkoani Tatanstan, kati yake droni sita zilipiga kwenye majengo ya makazi ya watu, moja ilipiga eneo lenye kiwanda cha uzalishaji bidhaa na nyingine ilidhibitiwa ikijaribu kukatiza juu ya mto.
    Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Russia, Ukraine ilipeleka mashambulizi ya aina tatu ya ndege hizo zisizo na rubani yakilenga majengo ya makazi na miundombinu ya Raia eneo la Kazan nchini humo.
    Kwa mujibu wa Jeshi la Nchi hiyo, mfumo wa anga kujilinda wa Russia pia ulifanikiwa kudungua droni tatu zilizorushwa nchini humo, udunguaji huo uliratibiwa na mfumo wa kujilinda unaotumia Umeme.
    Tangu kuanza kwa Operesheni za Kijeshi za Russia nchini Ukraine Februari 2022, Ukrainw imekuwa ikirusha Ndege zisizo na rubani kwenda nchini Russia bila mafanikio kutokana na kudhibitiwa na mfumo wa kujilinda wa taifa hilo.
    Ni Droni chache ambazo zimefanikiwa kupenya na kupiga maeneo ya taifa hilo hata hivyo ndege hizo hazijaripotiwa kuleta madhara yoyote kwa binadamu zaidi ya kusababisha uharibifu wa miundombinu.
    Mashambulizi mengi ya ndege hizo yanayofanywa na Ukraine yanalenga maeneo ya mipakani kati ya Russia na Ukraine, hata hivyo shambulizi la juzi lililenga eneo la mbali na mipaka hiyo kwani Kazan inakadiriwa kuwa zaidi ya Kilometa 1,379 kutoka ulipo mpaka wa mataifa hayo.
    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova aliyaita mashambulizi ya ndege hizo za Ukraine kuwa ni ya kigaidi na kusema Ukraine ilifanya hivyo ili kulipiza kisasi kutokana na Kazan kuwa mwenyeji wa Mkutano wa BRICS ulioketi Oktoba mwaka huu.
    Pia alisema mashambulizi hayo yanalenga kuibua hofu miongoni mwa wakazi wa eneo ambalo ndege hizo zilishambulia katika taifa hilo.
    Katika mashambulizi hayo, makombora aina ya Kamikaze yaliyokuwa kwenye droni hizo yalipiga majengo hayo ya Russia na kuibua hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.
    Ukraine ya Volodymyr Zelenskyy bado inapambana kuhakikisha inayarejesha maeneo yake yaliyotwaliwa na Russia tangu kuanza kwa uvamizi huo mwezi Februari 2022.
    Miongoni mwa mikoa ya Ukraine ambayo ilitwaliwa na Russia ni pamoja na Donetsk, Luhansk, Pekrovisk, Zaporizhia, Kherson na Crimea ambayo ilitwaliwa na Russia kutoka mikononi mwa Ukraine mwaka 2014.
    Katika kujibu hilo, Vikosi vya Ukraine vilifanya mashambulizi mfululizo vikisaidiana na Majeshi ya Marekani, Uingereza na baadhi ya nchi za Jumuiya ya Kujilinda ya NATO na kuteka eneo la Kursk eneo ambalo hadi sasa mapigano yameshika kasi kutokana na vikosi vya Russia kuanza kulirejesha kwa kasi ya ajabu japo bado eneo lote halijarejea mikononi mwa utawala wa Rais Vladimir Putin.
    IMEANDIKWA NA MGONGO KAITIRA

ความคิดเห็น • 19

  • @LupakisyoKandonga
    @LupakisyoKandonga หลายเดือนก่อน +2

    Ujawahi shindwa putn💪🇫🇷

  • @suratibrahim6417
    @suratibrahim6417 หลายเดือนก่อน

    Watajutia hakika✍️🇷🇺🇷🇺🇷🇺🇷🇺💯

  • @StellaCharles-zk4kb
    @StellaCharles-zk4kb หลายเดือนก่อน +1

    We umechelewa cna imani na wew tena

  • @josepheriah5977
    @josepheriah5977 หลายเดือนก่อน +1

    Urusi zaif

  • @josepheriah5977
    @josepheriah5977 หลายเดือนก่อน +1

    Achaapigwe yeye nan

  • @DeusRobart
    @DeusRobart หลายเดือนก่อน +1

    Nani mwingine amesikia ndege zisizo na ruban kwa binadam 😂😂😂😂😂

  • @albertsanga4615
    @albertsanga4615 หลายเดือนก่อน

    Tumekuchoka
    Putini Kila siku ivy ivy

  • @malkiawagiza1327
    @malkiawagiza1327 หลายเดือนก่อน

    Shetani alimzaini Zelenski sasa yuko matatani 😂

  • @YamunguMatamya
    @YamunguMatamya หลายเดือนก่อน

    Wewe ulizembea acha yakukute

  • @gregoryhaule2005
    @gregoryhaule2005 หลายเดือนก่อน

    West and U.S still problems on this world

  • @khalifasaidi7001
    @khalifasaidi7001 หลายเดือนก่อน

    Hivi visasi mpaka lini?

  • @geraldtarimo7379
    @geraldtarimo7379 หลายเดือนก่อน

    Putin piga hao mashoga kipigo cha mbwa mwizi

    • @MarcellySumaye-bv5lh
      @MarcellySumaye-bv5lh หลายเดือนก่อน +1

      Sawa mke wa putin

    • @williamsimusanga6605
      @williamsimusanga6605 หลายเดือนก่อน

      Wewe ni muke wa nani???​@@MarcellySumaye-bv5lh

    • @modestwenceslaus9
      @modestwenceslaus9 หลายเดือนก่อน

      Unawaonea wivu Mashoga wenzio siyo😂😂😂😂😂

  • @josepheriah5977
    @josepheriah5977 หลายเดือนก่อน

    Achaapigwe yeye nan