Baragumu Yake Bwana

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 26 ธ.ค. 2023
  • Baragumu yake Bwana wakati ikipigwa
    Na siku ya milele ikifika;
    Hapo waliokombolewa watakusanyika
    Nitakuwapo, jina kuitika
    [chorus]
    Na majina yaitwapo X3
    Kuitika jina, nitakuwapo
    [2]
    Wafu wa Kristo wafufukapo kwa siku ile,
    Tutashiriki na fahari yake;
    Waliochaguliwa watakaribishwa kwake
    Nitakuwako jina kuitika
    [chorus]
    Na majina yaitwapo X3
    Kuitika jina, nitakuwapo
    [3]
    Saa zote na tumfanyie Bwana kazi yake
    Tangu asubuhi hata jioni
    Maisha yetu ikomapo humu duniani
    Nitakuwako jina kuitika
    [chorus]
    Na majina yaitwapo X3
    Kuitika jina, nitakuwapo

ความคิดเห็น • 1