TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA 6 WA USALAMA WA ANGA AFRIKA MASHARIKI

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 23 ม.ค. 2025
  • Mkutano wa sita wa Taasisi inayosimamia Ulinzi na Usalama wa Usafiri wa Anga Afrika Mashariki (CASSOA) unatarajia kufanyika kuanzia tarehe 15 hadi 16 Mei 2024 , katika Hoteli ya Verde visiwani Zanzibar.
    Mkutano huo utawakutanisha wadau muhimu wa Usafiri wa Anga ikiwa ni pamoja na makampuni ya ndege, viwanja vya ndege, wasimamizi na wadau wa usalama katika sekta ya anga kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo pia wajumbe watajadili maswala ya utunzaji wa mazingira.
    Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari amesema mikutano ya EAC Aviation ilianzishwa na Bodi ya EAC-CASSOA kama njia ya kuongeza uelewa juu ya maswala yanayoathiri Usalama wa Usafiri wa Anga katika kanda yetu wa Africa Mashariki na Duniani kwa ujumla.
    Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006).
    Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege.
    Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba

ความคิดเห็น •