Ukiwatusi Masahaba na wake wa Mtume wewe si Mwenzetu || Sheikh Samir Sadik (Chaka la Simba)

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 ธ.ค. 2024
  • 🕌🔊✍️Nukuu
    Alhabib Sheikh Samir Sadik (Chaka la Simba)
    01 Rabi ul Awwal 1442
    Kuna vitu nikikutana navyo katika shughuli Stimu zinakata,
    Sheikh Waleed kaniamrisha niseme, nami nitasema kama ifuatavyo,
    Sheikh Mziwanda amesema,
    ولو شاء ربك لجعل الناس أمة واحدة ولا يزالون مختلفين
    Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana,
    Mwenyezi Mungu angelitaka angetufanya tuwe wamoja, lakini hakutaka hivyo,
    Je Ingekuwa wote ni wanasiasa, Je wangekuwa ni maamuma tu, Je wangekuwa ni Waislam wote, wapo waislamu wasafi na wengine si safi,
    إذا جاءك المنافقون قالوا نشهد إنك لرسول الله والله يعلم إنك لرسوله والله يشهد إن المنافقين لكاذبون
    Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo.
    Mwenyezi Mungu anashuhudia hao ni waongo, tuushike Uislam ipasavyo, tukamate mambo yetu, ukiwa ni Sheikh usijiweke na watu na mambo yao, ukijichanganya utajiumbua,
    Anti Shia
    Alhabib Chaka la Simba anasema: Twariqa yetu ni kumpenda Mtume, wanafiq hawakumpenda na yanadhihirika wazi,
    Waliopo baa hao wamechagua kukaa huko, lakini umekuja kwenye jambo letu halafu watukana Masahaba, jamani tusikatane Stimu.
    Wale walomsingizia Mama Aysha walikuwa ni makosani, Na Mu'umin hawezi kumsingizia Mke wa Mtume,
    Wapo wanaosema Bibi Aisha kazini, hawa si wenzetu, Wale wanaosema Masahaba walikuwa majambazi, wamedhulumu haki za Bi Fatma,
    النبي أولى بالمؤمنين من أنفسهم وأزواجه أمهاتهم وأولو الأرحام بعضهم أولى ببعض في كتاب الله من المؤمنين والمهاجرين إلا أن تفعلوا إلى أوليائكم معروفا كان ذلك في الكتاب مسطورا
    Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuliko Waumini wengine na Wahamiaji. Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu. Haya yamekwisha andikwa Kitabuni.
    Mtume hakukosea kuchagua marafiki, hakukosea kumuoa Bi Aysha na wengineo, ukiwatukana wapendwao na Mtume basi umemtukana Mtume, wewe hutufai.
    Amemaliza Alhabib Sheikh Samir Mudir Shamsul Maarif (Chaka la Simba), ukiingia kwenye Chaka la Simba hakika utararuriwa tu, hakuna namna,
    Ibn Umar A'naqshbandy
    Shadhully News

ความคิดเห็น •