'HOUSE GIRL' ALIYEITIKISA DAR AKAMATWA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 6 ก.ย. 2024
  • DAR ES SALAAM: JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata dada wa kazi za nyumbani 'House Girl', Clemensia Cosmas Mirembe (19) aliyekuwa anatafutwa kwa kosa la kumjeruhi mtoto wa mwajiri wake Maliki Hashimu (5) Mkazi wa Goba jijini Dar es salaam ikidaiwa alimkata na kitu chenye ncha kali shingoni kilichotenganisha njia ya hewa chini ya sanduku la sauti na kumsababishia kushindwa kupumua, kuongea, kupata maumivu na kupoteza damu nyingi sana.
    Akiwa Mkao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro ameeleza kuwa baada ya tukio mtuhumiwa alikimbia.
    "Upelelezi wa tukio hilo la kikatili ulianza mara moja na Julai 21, 2024 saa 4:00 usiku Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa huyo akiwa amejificha kwenye jumba bovu maeneo ya Goba Kizudi Kinondoni,” amebainisha.
    Follow us on:
    FACEBOOK;
    SpotiLeo: / spotileo-176. .
    HabariLeo: / habarileo
    DailyNews: / dailynewstz
    INSTAGRAM;
    HabariLeo: ....
    SpotiLeo: ....
    TWITTER;
    Twitter HabariLeo: Ha...

ความคิดเห็น • 1