05b Jinsi ya Kuwa Mkristo; (Imani Itakayotuokoa ni Ipi?) Madaraja ya Kumfikia Mungu

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 31 ธ.ค. 2024
  • Katika kuokoka tunaona hatua tatu kubwa. Kuamini Kutubu na Kupokea.
    Kuamini inamaana gani? Imani inayotuokoa ikoje? Mtu anaweza kuamini rais yupo ila kumwamini kama mtu mwaminifu ni hatua kubwa kubwa zaidi. Tunapomwamini Mungu tunapaswa kumwamini zaidi ya kuamini yupo tu. Bali matokeo ya kumwamini yataonekana katika maisha yetu ya kila siku.
    Kutubu inamaana gani?
    Mchungaji Justin anakazia umuhimu wa kuweka sawa makosa tuliofanya kadiri ya uwezo wetu.
    Kupokea inamaana gani?
    Hatupaswi kuwa na mashaka juu ya wokovu wetu, ikiwa tumemwamini Mungu na kumfuata.
    Je! Shetani anaweza kuwa na nguvu juu ya Mkristo? Karibu kujifunza haya pamoja na mengine mengi katika somo hili. Mungu akubariki.
    Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
    Barua pepe: neno@majiyauzima.com
    Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
    Tovuti majiyauzima.com

ความคิดเห็น •