Tenzi za Rohoni No 135 - Mapenzi Ya Milele

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 28 ก.ย. 2024
  • Lyrics: Mapenzi ya milele
    1. Mapenzi ya milele
    Ndiyo yanipendezayo;
    Yalinipenda mbele,
    Sina fahamu nayo;
    Sasa amani yake
    Tele rohoni mwangu,
    Ni mimi kwa kuwa wake,
    Na yeye kuwa wangu,
    Ni mimi kuwa wake,
    Na yeye kuwa wangu
    2. Mbingu zinang’ara juu,
    Na nchi nayo vivyo;
    Macho ya dunia tu
    Hayajaona hivyo;
    Nyuni huimba sana,
    Maua yana rangi,
    Ni kumjua Bwana
    Na pendo zake nyingi,
    Ni kumjua Bwana
    Na pendo zake nyingi,
    3. Mambo mengi maovu
    Nayo yenye kutisha,
    Sasa hayana nguvu,
    Si yenye kututisha;
    Ni mkononi mwake,
    Nalindwa salamani
    Ninajua ni wake,
    Ni wake mapenzini.
    Ninajua ni wake,
    Ni wake mapenzini.
    4. Wake hata milele,
    Si kutengana tena;
    Hunipa raha tele
    Moyoni mwangu, Bwana;
    Hiyo nchi na Mbingu
    Zitatoweka zile,
    Ni wake, Yeye wangu,
    Milele na milele.
    Ni wake, Yeye wangu,
    Milele na milele.
    Tenzi za rohoni, Wimbo wa tenzi, hymn songs
    Tenzi za Rohoni No 135 - Mapenzi Ya Milele

ความคิดเห็น •