BI ZAHARA (WAONE MISUKULE WAO) PART 2

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 22 ต.ค. 2024

ความคิดเห็น • 24

  • @jojojospecial4581
    @jojojospecial4581 5 หลายเดือนก่อน +1

    Tunangoja muendelezo

    • @jodastories
      @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

      Mwendelezo ni kesho jioni

  • @KimamiMa-rt8gf
    @KimamiMa-rt8gf 5 หลายเดือนก่อน +1

    Sehem ya 3 naomba🙏

    • @jodastories
      @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

      Naipost Leo ndugu,subscribe ili ikitoka uwe wakwanza kuipata

  • @SummyStories
    @SummyStories 5 หลายเดือนก่อน +1

    Mr Unkown ndo nn we Joda 😂😂

    • @jodastories
      @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

      😅😅😅asiyejulikana

  • @THEDONSIMULIZI
    @THEDONSIMULIZI 5 หลายเดือนก่อน +1

    Bado mambo ni moto

    • @jodastories
      @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

      Pamoja Sana kaka

  • @MariamSaid-ds2yt
    @MariamSaid-ds2yt 5 หลายเดือนก่อน +1

    Sehem yatatu naomba

    • @jodastories
      @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

      Kesho mapema sana

  • @SummyStories
    @SummyStories 5 หลายเดือนก่อน

    MAMBO MATAMU SANAAA ❤❤

    • @jodastories
      @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

      Asante summy

  • @joycesemizigi5300
    @joycesemizigi5300 5 หลายเดือนก่อน

    😮iko vizuri

    • @jodastories
      @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

      Shukurani,mwendelezo utaupata hapahapa, usiache Ku subscribe

  • @jodastories
    @jodastories  5 หลายเดือนก่อน +1

    BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji)
    SEHEMU YA NANE(08)
    MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA
    MAWASILIANO: 0748862999
    **
    Mama angel anaonekana akiwa amefungwa kamba ndani ya chumba cha nyumba iliyochakaa,nyumba hii inapatikana katikati ya msitu wa kutisha.
    Chumba kilikuwa kitupu na mlango wa kuingia ndani uliachwa wazi.Mama angel akawa anajitahidi kujifungua kamba lakini hakuweza.
    Akiwa anahangaika kujinasua katika mtego huu,kuna nyoka mkubwa akaonekana akiingia ndani.Nyoka alikuwa na rangi nyeusi tii,macho makubwa pamoja na umbo lake la kutisha.
    Urefu wa nyoka ni mita saba,alikuwa anateleza kuingia ndani waweza dhani anatembea juu ya nyasi,nyoka akaanza kujivuta kuelekea chumbani,na ndani ya hicho chumba anachoelekea yupo Mama angel.
    Mama angel alipigwa na butwaa baada ya kuona kichwa cha nyoka akiingia ndani ya nyumba,baadae nyoka mzima akaingia chumbani kisha akamzunguka Mama angel.
    Mama angel akawa anatetemeka, alijua siku zake za kuishi ndio zimefika mwisho.
    "Uwiii...uwiii" (Mama angel akawa ana jaribu kupiga kelele za kuomba msaada ila sauti yake haikuweza kufika mbali).
    **
    Upande wa pili nyumbani kwa Bi Zahara,kile kikao cha dharura walichokuwa wamekaa wachawi kiliisha muda wake,Zahara alikubali kulala na hassan Usiku wa Leo ili wachawi wapate nguvu.
    Wakamchukua hassan kisha wamamfungia ndani ya chumba ambacho atakaa mpaka muda wa kufanya Mapenzi na Zahara ufike. Bi Zahara akawaaga wachawi wenzake kwa kusema.
    "Kila mmoja akaendelee na majukumu yake,ila tukumbuke Usiku wa Leo tutakuwa na tambiko la kuongeza nguvu"
    Baba otieno akauliza.
    "Vipi kuhusu mwili wa hassan hawatauzika Leo?"
    "Hawawezi kuuzika ,najua wataka kufanya mazishi siku ya kesho,sisi tukimaliza haja zetu hassan tutamfufua,lakini hatuwezi kumrudisha hivi hivi lazima tufanye jambo,sawa?"
    "Sawa Mkuu"
    "OK,sambaeni"
    Wachawi wote wakapotea,nyumbani akabaki Bi Zahara pamoja na mjukuu wake Zahara.
    Zahara akamwambia Bibi yake.
    "Natamani hassan anioe"
    Bi Zahara akatabasamu
    "Kuhusu hilo wala usijali mjukuu wangu,Mimi nipo na wewe bega kwa bega mpaka malengo yako yatimie"
    "Asante Sana Bibi"
    "Lakini Zahara kuna jambo haujaniambia vyema"
    "Jambo gani?"
    "Kuna muda ulikuwa unatumia uchawi wa kimbunga,je,ulikuwa unatumia kwa lengo gani?"
    Zahara akakaa kimya,bi Zahara akarudia tena swali lake.
    "Ni kipi ambacho kimekufanya utumie uchawi wa kimbunga?"
    Zahara akajibu kwa sauti ya chini.
    "Nilikuwa namtumia mwanamke ambaye alitakiwa kuolewa na hassan(angel)"
    "Kwanini?"
    "Kwa sababu sikuwa nataka ndoa yao itimie,niliona Kama unachelewesha mambo nikaamua kuwatumia kimbunga"
    "Aah.sawa,na ule muda ulikuwa unatoka wapi?"
    "Muda gani?"
    "Wakati nimewaita wanachama wote,wewe na Baba otieno mlikuwa watu wa mwisho kufika hapa,kuhusu Baba otieno nilikuwa nafahamu kinachoendelea, ila wewe sijui ulikuwa wapi"
    Zahara akamjibu Bibi yake.
    "Nadhani nilikujibu,nilisema kuwa nilienda kumtembelea Babu"
    "Nani kakuambia uende kule?hauoni Kama ni hatari?"
    "Hapana Bibi,nilimpelekea Chakula"
    "Chakula?"
    "Ndiyo"
    "Kwahiyo ,unataka kuniambia kuna mtu umempeleka kwenye nyumba anayoishi Babu yako?"
    "Ndiyo" (Zahara hakuogopa kumjibu Bibi yake)
    Bi Zahara akaonekana kutokupendezwa na matendo ya mjukuu wake,kwa mujibu wa Maneno ya Zahara,anadai kuwa amempelekea Babu yake Chakula.
    **
    Upande wa Mama angel,nyoka akaendelea kumzunguka kisha akainua kichwa juu akawa anatazamana na mama angel.
    Mama angel akaanza kusali sala ya mwisho,aliamini muda wowote kuanzia sasa ataenda kuitwa Maiti.
    Mama angel akafumba macho,lakini cha ajabu akasikia sauti ya kiume ikimuongelesha.
    "Siwezi nikakumeza"
    Mama angel akafumbua macho,akabaki kushangaa ni wapi sauti imetokea maana hapa chumbani yupo na nyoka pekee.
    "Ondoa wasiwasi" (Sauti ilitoka mdomoni kwa nyoka)
    Kumbe nyoka anaongea Kama binadamu wa kawaida,yaani anaumbo la nyoka lakini anaongea Kama binadamu,haya yalikuwa ni maajabu kwa Mama angel,akayatoa macho nje mithili ya Fundi saa akiwa amepoteza nati ya saa.
    Nyoka akaanza kujiondoa mwilini kwa mama angel kisha akajikusanya mbele yake,akawa anatamtazama.
    Nyoka akasema
    "Naitwa Mzee kabiba,nilikuwa binadamu Kama wewe ila nikageuzwa kuwa nyoka na watu wabaya,ilikuwa nikumeze lakini siwezi"
    Mama angel alikuwa haamini kumuona nyoka anayeongea,Mama angel akajikaza kuongea na nyoka.
    "Kwani hapa ni wapi?"
    "Siwezi kukuambia hapa ni wapi,ila nachoweza kukwambia kwa sasa hapa ni sehemu mbaya Sana ambayo hakuna binadamu anatamani kufika,kuna kila aina ya mateso"
    "Unaweza nifungulia hizi kamba?"
    "Siwezi pia,Mimi naondoka ,tutaonana baadae endapo ukiwa unaendelea kuishi,ushauri wangu kwako usijaribu kumwambia mtu yeyote Kama umeonana na nyoka aina yangu"
    "Kwanini?"
    "Huwezijua unayemwambia,anaweza akawa ni mtu mbaya akaamua kukuua kwa kujua siri yao" (nyoka akaanza kutoka ndani ya chumba)
    **
    "Bibi nitaenda kumtoa mwenyewe,kwa sasa muache kwanza apate mateso" (ilikuwa ni sauti ya Zahara akimuomba Bibi yake)
    Bi Zahara akashusha pumzi.
    "Sawa,naomba asikae huko siku nyingi awe amerudi duniani,sipendi kuona unatumia nguvu za kichawi pasipo ridhaa yangu"
    "Sawa Bibi"
    Bi Zahara akataka kuondoka lakini akakumbuka jambo,akashika mdomo wake na kusema
    "Hao wakulima wetu wamekula?"
    "Niliwaletea mihogo nahisi watakuwa wamekula"
    "Hebu nenda kawaangalie"
    Bi Zahara akaingia ndani na kumuacha mjukuu wake akiwa anaingia kwenye nyumba ambayo misukule wanakaa.Zahara akawakuta misukule wakiwa wamekaa kwa unyonge huku mbele yao kukiwa na mihogo.
    "Nyie!kwanini hamjala mihogo!"
    Misukule wakabaki kumtazama.
    "Aah..!nimekumbuka Kama huwa hamli Chakula mpaka mpatiwe amri..Haya basi kuleni"
    Zahara akatoa amri kwa misukule wale Chakula, papo hapo misukule wakaanza kugombania Chakula,kila mmoja alikuwa anawahi kuchukua kipande cha mhogo mbichi ambacho kitamsaidia Kupunguza njaa.
    **
    Baba hassan akawa anajadiliana na wazee wa busara pembeni kidogo na nyumba yake,maongezi yao yalionekana kuwa ya usiri Sana ndio maana wameamua kujitenga mbali na watu wengine.
    Mzee mmoja wa busara anayefahamika Kama Mzee Chacha,akasema
    "Pole Sana Mzee mwenzetu kwa yaliyokukuta,najua haya yote yanatokana ma uchawi ambao umekuwa gumzo kwa miaka mingi"
    Mzee wa pili wa busara akadakia
    "Hata Mimi nahisi ni wachawi, hebu tazameni vifo vya ajabu ajabu vinavyotokea ndani ya hichi kijiji kisha mlinganishe na kilichotokea kwa Hassan"
    Mzee wa busara wa tatu
    "Haswaaa..!"
    Mzee Chacha akasema
    "Kinachonishangaza ni kitu kimoja,hapo zamani tuliwafukuza wachawi wote ndani ya kijiji,tukawaita mpaka waganga watusaidie kutatua changamoto zetu,ikaonekana wachawi wote wamefukuzwa,iweje tena Leo yanitokeze?"
    Mzee wa tatu akajibu
    "Huenda kukawa na wachawi wengine waliobakia"
    Mzee Chacha akadakia
    "Sasa tutafanya nini kuwapata?na vipi kuhusu mazishi ya Hassan?"
    Mzee wa tatu akajibu
    "Kuhusu hili suala itabidi tumshirikishe mwenyekiti wa kijiji,kupitia mwenyekiti tutaweza kupata mwafaka,na mazishi sioni umuhimu wa kuzika Leo,tusubirini siku ya kesho jioni ,au nyie mwasemaje?"
    Mzee wa pili akasema
    "Sahihi kabisa,labda Kama baba Hasan anajambo la kusema"
    Baba hassan akaanza kwa kukohoa kidogo.
    "Khoho khoho...kwangu Mimi sioni wazo baya,nipo pamoja na nyie katika kuhakikisha tunatokomeza uchawi."
    Baba Hassan na wazee watatu wakakubaliana namna gani wanaweza kuwaporomosha wachawi.Hawakuwa wanatambua Kama Uchawi wa Bi Zahara ndio nuksi kubwa kwao.
    **
    Angel akatafuta muda wa peke yake,akaingia ndani ya chumba chenye mwili wa marehemu Mume wake mtatajiwa,angel akawa analia kwa masikitiko.
    "Mume wangu kipenzi,kwanini umeniachia mateso makubwa namna hii!" (Angel akaendelea kulia)
    "...mume wangu jamani, nitakuwa mgeni wa nani Mimi? Mapenzi yangu nitamuonesha nani!hebu rudi basi " (Angel alilia Sana)
    Angel hakuwa anajua mtu ambaye anamlilia ameshachukuliwa kichawi na sasa yupo ndani ya chumba chenye giza nene akiwa anasubiri muda ufike afanyishwe Mapenzi na Zahara.
    Hassan hana kumbukumbu yoyote,anachokiona na kukisikia hakikai kichwani hata dakika moja.Laiti Kama hassan angelitambua kosa lake la kumuacha Zahara na kwenda kumuona angel basi asingelibaki kimya,angeliomba msamaha zamani Sana ili kuepusha matatizo zaidi.
    Itaendelea........

  • @jodastories
    @jodastories  5 หลายเดือนก่อน +1

    BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji)
    SEHEMU YA SABA(07)
    MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA
    MAWASILIANO: 0748862999
    Songa nayo.......
    **
    Mchawi wa Wachawi (Bibi Zahara),alijiandaa kulitupa kombola la kichawi kwa Baba Hassan lakini akaghairisha.
    "Huyu ni Mtoto mdogo Sana,yanini nimuue kwa kombola kubwa namna hii,hahahah"(Bibi Zahara akapotea kichawi)
    Sekunde tatu zikatosha kwa bi Zahara kurudi nje kwa wanakijiji ambao wamemzunguka Lizy,akamtazama lizy akakuta bado anarusha miguu na mikono.
    Bi Zahara akatabasamu,akapepesa macho kwa wanakijiji wote waliokuwa wamemzunguka Lizy,alipotupa macho mlangoni akamuona mama Hassan akitoka nje,Bi Zahara akatazama juu kisha pale pale akapotea kichawi na kwenda kumuingia Mama hassan.
    Bi Zahara akaingia kwenye mwili wa Mama hassan,na kwa Sasa mama hassan atakuwa anafanya Yale yote anayoamuliwa na bi Zahara.
    Mama hassan alipoingiwa na uchawi wa Bi Zahara,akatupa macho kwenye nyumba ambayo mume wake ana jaribu kumfufua mwanae.
    Pale pale Mama hassan akaanza kuelekea ulipo mlango,akausukuma kwa nguvu zote mpaka ukabamiza ukutani.
    " unafanya nini wewe?"(Mama Hassan alimuuliza mume wake kwa kupaza sauti)
    Mume wake baada ya kusikia sauti ya mama hassan akaacha kufanya maombi ,looh..!laiti angelijua Kama Bi Zahara anamuongoza mke wake asingethubutu kuacha maombi kwa sababu ulimwengu wa Giza alikuwa ameanza kuushinda.
    "Mke wa...."
    "Nani mke wako?unajidai kumfanyia maombi mwanangu au ndio uchawi wa mama yako umekuambia ufanye hivyo?"
    "Hebu tulia mama hassan"
    "Nitulie nini?mwanangu ameuawa na mama yako mzazi,kwanini mama yako hajafika mpaka Sasa kwenye sherehe ya mjukuu wake?hauoni kama mama yako ni mchawi? Siku zote nilikuwa nakuambia umeona Sasa"
    Mama hassan aliongea kwa kufoka mpaka wanakijiji waliokuwa nje wakasikia,ama hakika siku ya Leo imekuwa mbaya Sana nyumbani kwa akina hassan.Wanakijiji waliohudhuria hapa walijionea mambo ya aibu kutoka katika familia hii.
    Leo wale wapenda umbea ndio imekuwa siku nzuri kwao,walikuwa wanabadilisha vituo kutoka kwa lizy aliyepatwa kifafa wanaenda kutega sikio karibu na nyumba ambayo kuna ugomvi Mwingine ulioamshwa na Mama hassan.
    Matendo anayoyafanya mama hassan kwa Sasa hakuwa anajitambua,akili yake imetekwa na ulimwengu wa giza unaoongozwa na Bi Zahara.
    Umbo na sura ni Mama hassan,lakini anayemuongoza ni Bi Zahara.
    Mama hassan akaendelea kutema cheche(kuropoka)
    "Mwanangu amekufa,unajidai mtu wa maombi,umekuwa mtume?hee?hebu nijibu"
    Baba Hassan akainamisha kichwa chini.
    "We mwanaume hebu nipe jibu,umekuwa mtume?tangu lini ukaanza kusali?"(Mama Hassan hakumpa kituo Mume wake)
    Wazee wa busara watatu wakaingia ndani,wakajaribu kuamua ugomvi lakini na wao wakaambulia kutukanwa,kwa heshima aliyonayo mama hassan na matusi anayoyatoa havikuwa vinaendana.Mama Hassan haoni tatizo kutoa maneno machafu mbele ya wazee wa busara wanaoaminika na kijiji na Mashene.
    **

  • @jodastories
    @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

    BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji)
    SEHEMU YA TISA(09)
    MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA
    MAWASILIANO: 0748862999
    **
    Masaa yalisogea na hatimaye ule Usiku uliosubiriwa kwa hamu na wachawi ukafika,ilikuwa yapata saa sita usiku,katikati ya uwanja wa makutano wanaoutumia sikuzote,walionekana wachawi wakiongozwa na Bi Zahara wakiwa wamekusanyika,nyimbo za hapa na pale za kutukuza mizimu yao ilikuwa inaendelea.
    Bi Zahara alikuwa amesimama karibu na mjukuu wake Zahara ambaye alikuwa amebeba kitambaa kikubwa chekundu.
    Baada ya dakika moja kupita,Bi Zahara akainua mkono juu ikiwa ni ishara ya kuwazuia wachawi wasiendelee kuimba nyimbo zao.
    Wachawi walipokaa kimya,Bi Zahara akapaza sauti.
    "Siku ya Leo ni siku nzuri Sana kwetu,mpaka sasa tunaongoza ushindi wa hichi kijiji,hakuna mtu ambaye anaweza kuzuia nguvu za Bi Zahara, nadhani mmeona matukio yote yaliyotokea siku ya Leo,Kama mtakuwa mmesahau ngoja niwakumbushe kidogo"
    "...siku ya Leo tumeweza kumchukua kijana (Hassan) ambaye amemchezea mjukuu wangu halafu akamuacha na kwenda kutaka kuoa mwanamke mwingine,hii ni aibu na kejeli kubwa kwangu na kilinge chote hichi,Kama mnavyojua tatizo langu lenu pia" (akavuta pumzi)
    "..si hicho tu,bali siku ya leo mjukuu wangu amefanya jambo kubwa na zuri upande wetu,ingawaje hapo mwanzo nilikuwa mkali Sana kwanini amefanya vile,mjukuu wangu ametuongezea mgeni kwenye nyumba yetu ya siri,mgeni huyo ni mama yake na Binti ambaye alitakiwa kuolewa na Hassan"
    "Jambo la tatu,tumeweza kuingiza nafsi ya kichawi ndani ya mwili wa Mma hassan,hivyo tutaweza kumtumia tutakavyo,nisije nikapoteza Muda wa kuongeza nguvu, si mnajua usiku wa Leo Mjukuu wangu Zahara ataenda kufanya Mapenzi na hassan mbele yetu ili tupate nguvu!"
    Wachawi wakaitikia kwa sauti kubwa.
    "Ndiyooooo"
    Sauti za Paka,fisi na mbwa zikaanza kulindima kila kona ya kijiji cha Mashene,hii ni baada ya Wachawi kufurahia tukio linaloenda kutokea.
    Wachawi huwa wana namna mbalimbali za kuongeza nguvu zao,na katika ulimwengu wa Wachawi kuna madaraja Kama ilivyo katika Serikali ya nchi,kuna Wachawi wenye hadhi ya Paka,hawa kazi yao kubwa ni kutuma chuma ulete kwenye biashara za watu,vilevile wanauwezo wa kuiharibu biashara yako.
    Ngazi nyingine ya Wachawi ni wale wanaotumia uchawi wa Fisi,hawa ni hatari Sana katika maisha ya mwanadamu,hawa kazi yao kubwa ni kuchukua nafsi za binadamu wasio na hatia ,wanauwezo wa kujigeuza kuwa Mdudu kisha wakikung'ata palepale unaanza kupata matatizo, Wachawi wa aina hii huwa wanatumwa kuwaua wagonjwa mahospitali na kutengeneza ajali kwa kuwachanganya dereva wakati wa safari.
    Ngazi kubwa kuliko zote ni hii aliyonayo Bi Zahara,ni Wachawi wanaotumia nembo ya Fuvu la binadamu aliyekufa zamani, mchawi wa aina hii anauwezo wa kuwaongoza Wachawi wa kila aina,huyu anauwezo wa kuwatuma na kuwapatia nguvu kwa siku maalumu.
    Siku maalumu ambazo mchawi Kama Bi Zahara anaweza kuwaongezea nguvu Wachawi wenzake ni siku ya katikati ya mwaka,yaani mwezi wa sita.
    Hivyo basi ,kila inapofika mwezi wa sita saa sita usiku,Bi Zahara anauwezo wa kuwaongezea nguvu Wachawi wenzake endapo wakifanya kafara ama mmoja Kati yao akifanya Mapenzi na mtu mfu.
    Kwakuwa usiku wa Jana walikula nyama ya binadamu,na kwa bahati nzuri kwao wakawa wamemuua hassan,hivyo ikabidi Zahara ajitoe kimasomaso kulala na hassan.
    Endapo Zahara akilala na hassan usiku wa Leo ,Basi kila mchawi atapata nguvu ambazo zitamfanya atoke daraja moja kwenda lingine,siku Kama ya Leo huwa inasubiriwa kwa hamu Sana na Wachawi wanaopatikana nchi nzima.
    Bi Zahara akamtazama mjukuu wake na kusema.
    "Nenda katandike hilo shuka pale" (Alimuelekeza aende katikati yao)
    Zahara hakusita,akaenda kutandika shuka jekundu alilokuwa amebeba,Wachawi wote walikuwa wamemzunguka zahara.
    Baada ya kumaliza kutandika shuka,bi Zahara akachukua mkia wake wa fisi akaanza kuuzungusha zungusha kila Pande kuu za dunia,alianza kusini,akaelekea mashariki,akageukia magharibi kisha akamalizia kaskazini.
    Alipomaliza akainua mikono yake juu,akasema.
    "Chabolande,ndelemane kolembo" (ikiwa na maana ya mizimu ya mababu zangu nipo tayari)
    akaendelea Kusema
    "Kolomile,talamise,talamise" (ikiwa na maana ya we kijana,njoo,njoo)
    Baada ya kutamka maneno yale,pale pale kuna upepo ukaanza kuvuma,punde si punde akatokea hassan katikati yao akiwa hajitambui.
    Wakaanza kucheka kicheko cha ajabu.
    "Hahahah....hehehe...hahahahah"
    Bi Zahara akasema
    "Muda ndio huu,mjukuu wangu kazi kwako kutupatia nguvu"
    Zahara akatamka maneno kadhaa ya kichawi,pale pale hassan akaanza kulala juu ya shuka jekunde lililotandikwa na Zahara.Hassan hakuwa anajitambua hata kidogo,familia yake wanajua amekufa kumbe Wachawi wamemchukua kwa masilahi yao binafsi.
    Hassan akalala chali,Zahara akamtazama Bibi yake.Bi Zahara akampatia ishara ya kuendelea.
    Lengo Lao ni Zahara afanye Mapenzi na Hassan mbele yao,Zahara akaanza kumvua nguo hassan mpaka alipomuacha mtupu.
    Zahara akasimama katikati ya miguu ya hassan,na yeye pasipokuwa na aibu akafungua nguo nyeusi alizojifunga,kwa kweli Zahara alibarikiwa umbo,kila sehemu ya mwili wake ulikuwa unavutia,Wachawi hawakuwa wanaoneana aibu kwa sababu muda mwingi huwa wanaenda kuwanga wakiwa uchi,yaani Zahara anaujua mjegeje wa baba otieno na Wachawi wengine wa kiume,lakini hata wao wanaujua vyema uchi wa Zahara.
    **
    Wakati yote yanaendelea,nyumbani katika familia ya Hassan kulikuwa kunasikika nyimbo za msibani,wanakijiji walikuwa wamekoka moto kwa ajili ya kuwasaidia kukesha usiku wa Leo.
    Angel na Dada yake Patricia walikuwa wamejikunyata karibu na Mama hassan.
    Mama hassan na angel walikuwa na mazungumzo.
    "Mwanangu nisamehe kwa kauli zangu nilizotoa mchana wa Leo"
    "Usijali mama,Mimi nimeshakusamehe" (angel akamjibu mama mkwe wake)
    Mama Hassan akaendelea kusema
    "Mwanangu aliniambia amempata mwanamke mwema na mcha Mungu,nimeumia Sana hata hamjaijenga familia yenu mwenzako katangulia"
    Angel akasema
    "Yote tumshukuru Mungu tusije kufuru,lakini kifo cha mume wangu kimekuwa cha kutisha na kushangaza,ila nakumbuka Mume wangu aliniambia tusije kufunga ndoa huku kwa sababu ya...."
    Kabla angel hajamaliza sentensi yake pale pale Mama mkwe akamuwekea ishara ya kukaa kimya.
    "Shiiiiiii..." (Akatazama huku na kule,akawaona wanakijiji wakiwa bize na mambo yao,wengine walikuwa wameanza kupitiwa na usingizi)
    Mama hassan akamtazama angel,akaanza kuongea kwa kunong'ona.
    "iwe mwanzo na mwisho kuzungumzia hizi taarifa,wakikusikia itakuwa hatari,hata kupotea kwa mama yako usitangaze kwa watu,acha ibaki hivyo hivyo mpaka pale atakapopatikana,lasivyo familia nzima tutaisha"
    *
    Upande wa pili kwa Wachawi, Zahara alikuwa anapambana kuziamsha hisia za hassan lakini nyeti za hassan zilikuwa zimenywea kama zikiwa ndani ya maji ya barafu.
    Zahara akasimama
    "Bibi,mbona ha..."
    "Subiri nikuonyeshe" (bi Zahara akasogea karibu na hassan)
    Bi Zahara akachuchumaa kando na mwili wa hassan,akapeleka mkono wake wa kulia kwenye nyeti za hassan,akazishika kisha akaongea maneno ya kichawi,palepale nyeti za hassan zikasimama na kukakamaa.

  • @jodastories
    @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

    9b
    *
    Upande wa pili kwa Wachawi, Zahara alikuwa anapambana kuziamsha hisia za hassan lakini nyeti za hassan zilikuwa zimenywea kama zikiwa ndani ya maji ya barafu.
    Zahara akasimama
    "Bibi,mbona ha..."
    "Subiri nikuonyeshe" (bi Zahara akasogea karibu na hassan)
    Bi Zahara akachuchumaa kando na mwili wa hassan,akapeleka mkono wake wa kulia kwenye nyeti za hassan,akazishika kisha akaongea maneno ya kichawi,palepale nyeti za hassan zikasimama na kukakamaa.
    Zahara akaachia tabasamu baada ya kuona Mali aliyobarikiwa nayo hassan,bi Zahara akarudi kusimama kwenye sehemu yake akamuachia uwanja mjukuu wake.
    Zahara akasimama katikati ya mapaja ya hassan,akaanza kuchuchumaa taratibu mpaka pale ambapo alipogusanisha hasi na chanya,Mhogo wa hassan ukaingia kwenye sufuria dogo la Zahara,kwa kuwa siku ya Leo Zahara ameachiwa jiko,akaanza kupika na kupekua ujazo wa Chakula anachotaka yeye.
    Zahara akaendelea kukoroga Chakula kitamu ,alifurahia kupata Chakula ambacho anasiku nyingi hajakipata,utamu wa Chakula ulimnogea Zahara akajikuta akianza kuongea maneno ambayo hayakuwa yanaeleweka.
    Wakati yeye anajipimia Chakula akitakacho,Wachawi wenzake walikuwa wanafurahi maana muda si mrefu wanaenda kupata nguvu zitakazowafanya wawe na uwezo wa kuamua jambo walitakalo ndani ya kijiji cha Mashene.
    Itaendelea.......

  • @jodastories
    @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

    "Nitaoana naye vipi na wakati atakuwa msukule?"
    "Hassan hatakuwa msukule,atabaki kuwa binadamu wa kawaida,kuhusu maiti watakayozika,tutawawekea mgomba ila wao wataona ni mwili wa hassan"
    "Bibi hiyo hapana,unaonaje tukitafuta mpango Mwingine wa kumfanya hassan awe chini yangu?"
    Bibi Zahara akajitoa mwilini Mwa mjukuu wake,akavishika viganja vya mikono ya Zahara.
    "Mjukuu wangu,kumbuka hassan alikuadanganya kwa kukupatia ahadi za kukuoa akirudi kutoka masomoni,maneno yake yakakufanya umpatie Bikra uliyoitunza kwa miaka nenda rudi,kwanini tusimuue?"
    "Lakini Mimi bado nampenda"
    Bibi Zahara akaanza kunusa harufu huku anatazama juu Kama mbwa,alinusa kwa sekunde kadhaa kisha akasema
    "Kuna mpuuzi mmoja anajikuta nabii,anataka kumrudisha mtu tuliyemchukua,Hahahah"
    **
    Upande wa pili Kwa Baba hassan,alikuwa anaendelea kuufanyia maombi mwili wa hassan pasipo kuchoka, kumbe maombi anayofanya yanasikika kwa Bibi Zahara.
    Bibi Zahara akawa anacheka kwa nguvu maana anajua Baba hassan hawezi kumrudisha mwanae.
    **
    Ndani ya nyumba aliyopo Mama hassan kulisikika varangati.
    "Niache mama,sijamuua mwanao Mimi" (sauti ya angel)
    "We mchawi mkubwa,haiwezekani mwanangu umuue nikuache hivihivi" (sauti ya Mama hassan)
    Sauti zile zikawafikia wageni waliokuwa nje,kila mmoja akawa na shauku ya kutaka kujua ni jambo gani linaendelea ndani ya nyumba?.Wale wanawake wapenda umbea wakaanza kusogea karibu na mlango wa nyumba inayosikika ugomvi.
    Mama hassan alikuwa amemkaba koo angel,wamama wachache waliokuwa ndani walikuwa wanauamua ugomvi.
    Mama wa kwanza akasikika akisema
    "Mama Hassan muache"
    Mama wa pili
    "Jamani mnagombana msibani?"
    Sauti ya Patricia ikasikika
    "Mama acha kuniumizia Dada yangu" (Patricia akawa anamsukuma mama hassan asiendelee kumkaba angel)
    Angel alikuwa ametulia wakati ambao mama hassan anajichukulia 'pointi' kwa kumkaba na kumsukuma ukutani.
    Machozi hayakukata wa binti angel,ni maumivu kiasi gani anayapata kwa kusingiziwa kesi ya uchawi.
    Ugomvi ukaendelea ndani ,na wakati huohuo Baba hassan alikuwa anaendelea na maombi yake ya kumfufua mwanae.
    Baba otieno alikuwa hana amani kabisa, amejaribu kutumia kila aina ya mbinu atoke nje imeshindikana.Lengo la Baba otieno akitoka nje anataka apotee kichawi aende kwa Bibi Zahara.
    Kimoyo moyo Baba otieno akasema
    "miungu ya Bibi Zahara naomba mniumbuke"
    Alivyotamka tu maneno yale,yakapenya mpaka masikioni mwa Bibi Zahara. Huwezi amini Bibi Zahara amesikika maneno ya Baba otieno ingawaje wapo mbali mbali kwa kilometa kadhaa.
    Bibi Zahara akagusa paji lake la uso kwa kidole gumba,akasema
    "Usijali Baba otieno, hizo nguvu haziwezi kukudhuru"
    Sauti ya Bibi Zahara ikapenya masikioni mwa Baba otieno, yaani walikuwa wanafanya mazungumzo kana kwamba wapo karibu.
    Baba otieno alipoisikia sauti ya Bibi Zahara ikimtia moyo akatabasamu, Mzee mmoja akamuona Baba otieno akitabasamu,akamsogelea.
    Mzee yule akamuuliza kwa kunong'ona
    "Mbona unatabasamu na wakati mwenzio anamfanyia maombi mwanae?"
    Kabla Baba otieno hajajibu swali,kelele za ugomvi wa wanawake zikasikika.
    "We ni mchawi" (sauti ya Mama hassan)
    Baba otieno na wazee wawili waliokuwa pamoja ndani wakatoka nje, walimuacha Baba hassan akiwa anamuombea mwanae.
    Baba otieno akaona hii ni nafasi yake ya pekee kupotea kichawi.Akazunguka nyuma ya nyumba kwa kunyata,Baba otieno akafanikiwa kufika nyuma ya nyumba ambayo ndani yake kuna ugomvi wa Mama na mkwe wake.
    Baba otieno akatazama kushoto na kulia ,alipoona hakuna mtu akapiga goti moja chini kisha akafumba macho,pale pale Baba otieno akapotea kichawi.
    Looh..!ule msemo wa 'siku za Mwizi ni arobaini' ulitimia kwa Baba otieno,kumbe wakati anatoweka kichawi kuna Binti mwenye umri wa miaka kumi na nane alikuwa anamuona.
    Binti yule hakuonekana na Baba otieno kwa sababu alikuwa amejificha chooni.Choo kinachotumiwa na familia ya Baba hassan kimejengwa nje kwa kutumia nyasi na makuti yaliyokauka,kwa bahati nzuri kulikuwa na matobo matobo ambayo yalimsaidia Binti huyu kuona kila kinachoendelea. Binti baada ya kulishuhudia tukio lile akashindwa kabisa kuendelea na kukata gogo(kujisaidia haja kubwa),akavuta juu gauni alilokuwa amelishusha wakati wa kukata gogo,Mbio mbio akatoka ili akawaambie wanakijiji wengine kuhusu uchawi wa Baba otieno.
    **
    Baba otieno akafika nje ya nyumba ya Bibi Zahara, akawakuta wachawi wenzake wakiongozwa na Zahara.
    "Mkuu yupo wapi?" (Lilikuwa ni swali la Baba otieno baada ya kufika na kutokumuona Bibi Zahara)
    Zahara akamjibu kwa madaha
    "Ameenda kusafisha uchafu uliouacha"
    "Uchafu gani?"
    "Tulia anarudi muda si mrefu,twendeni ndani" (wachawi wakaanza kuingia ndani ya nyumba ya udongo ya Bibi Zahara)
    **
    Binti ambaye amemuona Baba otieno akipotea kichawi akawa amefika mpaka kwa wanakijiji waliohudhuria sherehe ambayo imegeuka kuwa msiba,akakuta umati mkubwa wa watu ukiwa nje ya nyumba ambayo mama hassan na angel wapo ndani.
    Akapepesa macho huku na kule,akamuona Mama yake mzazi akiwa anasikiliza umbea unaohusu ugomvi wa angel na Mama mkwe wake.
    Binti yule akapaza sauti
    "Mamaaaa...."
    Mama yake na watu wote waliokuwa nje ya mlango wakageuka,wakamuona binti akiwa anahema juu chini tena kwa wasiwasi mkubwa.
    Watu wote wakatega sikio kumsikiliza maana anaonekana mwenye kuwa na jambo kifuani.
    "Ma..ma....ma" kila alipotaka kuongea kuna kitu kikawa kinamkaba kooni.
    "Ma....ma...Ku...Ku...." (Jasho likaanza kumtoka)
    Mama yake akamsogelea mwanae
    "We lizy,kuna nini?"
    "Ku...Ku...Ku" (lizy alishindwa kuongea,akawa anajikaba koo kwa mikono yake mwenyewe)
    Macho ya lizy yakaanza kubadilika rangi na kugeuka kuwa meupe mithili ya theruji.
    "Jamani mwanangu" (Mama lizy akapiga ukunga baada ya kuona hali ya mwanae inazidi kuwa mbaya)
    Macho ya wanakijiji yakageuka kwa Mama lizy,wakaanza kumsogelea.
    "Mwanangu umepatwa na nini?"
    "Ku...Ku...Ku" (lizy hakuweza kuongea)
    Pale pale lizy akadondoka chini,akaanza kurusha miguu na mikono Kama mtu aliyepatwa na kifafa,macho yake yalikuwa meupe, mdomo wake ukawa unatoa povu jeupe huku anaung'ata ulimi.
    Sauti ya kiume ikasikika ikisema
    "Jamani amepatwa na kifafa,njoeni tumsaidie"
    Wanaume kadhaa wenye nguvu wakasogea karibu na lizy,wakaanza kumpatia huduma ya kwanza kwa mtu aliyepatwa na kifafa,cha kwanza waliweka kipande cha mti mdomoni Mwa lizy akawa ameking'ata kwa ajili ya kuzuia kung'ata ulimi.
    Cha pili wakamlaza ubavu,Shingo na kichwa chake wakakiinua juu,wakaendelea kumpatia huduma ya kwanza.
    Mama lizy alikuwa analia
    "Mwanangu.... Mwanangu....."
    'Ukistaajabu ya musa ,utayaona ya filauni',Bi Zahara alikuwepo eneo la tukio na mavazi yake ya kichawi,mkononi alibeba mkia wa fisi ambao anautumia kwa kazi mbalimbali.
    Hakuna mwanakijiji hata mmoja ambaye alifanikiwa kumuona Bi Zahara, walikuwa wanampita pale pale.
    Bi Zahara ndiye aliyesababisha haya yote,akawa anacheka "Hahaha,..hahahah"
    Bi Zahara akatupa macho kwenye nyumba ambayo yupo Baba Hassan na mwanae,ikumbukwe Baba hassan anamuombea mwanae afufuke.
    "Nimeshamalizana na huyu, Sasa ni zamu yako Baba Hassan"
    Bibi Zahara akapuliza mkia wake wa fisi,mara ghafla akapotea kichawi.Bi Zahara akaenda kutokelezea kwenye kona ya nyumba aliyopo Baba hassan.
    Bi Zahara akawa anatabasamu
    "Hakuna ambaye amefanikiwa kunizuia Mimi,unajiona mtu wa maombi Sasa ngoja nikuonyeshe Mimi ni nani"
    Baba Hassan hakuwa amemuona Bi Zahara maana bi Zahara ametokea nyuma yake,Baba hassan alikuwa anafanya maombi mpaka jasho linamtoka.
    Bi Zahara akaandaa kombola la kichawi lililopo katika mfumo wa moto mkali,akawa analizungusha zungusha akijiandaa kulitupa mgongoni kwa Baba hassan.Aina ya kombola la kichawi analolitumia Bi Zahara huwa ni hatari Sana,hakuna ambaye amewahi pona baada ya kutupiwa kombola hili.
    Bi Zahara akakusanya nguvu zake nyingi,akaanza kuhesabu kuanzia namba moja ili ifikapo namba tatu aliachie.
    "Moja......mbili....." Bibi Zahara amebakiza kutamka namba moja ya mwisho ambayo ni namba tatu,atakapoitamka atamtupia Baba hassan kombola.
    Itaendelea........
    😈BABA HASSAN ATAPONA KWELI?
    😈BABU ZAHARA YUPO WAPI?
    😈MAMA ANGEL YUPO WAPI?
    😈LIZY ATAPONA?
    😈NI SAHIHI MAMA MKWE KUMTUHUMU ANGEL KUWA NI MCHAWI?

  • @jodastories
    @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

    BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji)
    SEHEMU YA SITA(06)
    MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA
    MAWASILIANO: 0748862999
    TULIPOISHIA......
    Baba otieno akawa anatembea huku na kule,hakuwa na sehemu ya kuelekea maana ndani wapo watu wanne,yeye,Baba Hassan anayefanya maombi pamoja na wazee wawili wanaoonekana kuwa wazee wa Busara.
    Baba Hassan anafanya maombi na wakati huohuo wachawi wameanza kukusanyika nyumbani kwa Bibi zahara.Baba otieno hajapata mbinu ya kutoka ndani asije onesha upande wake wa pili wa shilingi.Endapo akipotea kichawi sasa hivi itaonekana kuwa yeye ndio mchawi anayehusika na kifo cha Hassan.
    Angel na Patricia wakafika nyumbani kwa akina Hassan,majonzi mazito yalikuwa upande wao, wakikumbuka muda si mrefu wamempoteza mama yao ndio wakazidi kulia.Ndugu,jamaa na marafiki waliokuwa eneo hili wakawafariji angel na Patricia. Wanawake waliokuwa nje wakawachukua angel na Patricia mpaka ndani ya nyumba ambayo yupo Mama yake na Hassan.
    **
    SONGA NAYO.......
    Bibi Zahara akawahesabu wana kilinge wenzake.
    "Bado wawili...Zahara na Baba otieno wapo wapi?" Bibi Zahara akaanza kutembea huku na kule.
    mara ghafla kuna bundi mkubwa akatua katikati ya wachawi wanaoongozwa na Bibi Zahara.
    Tabasamu likashamili kwa Bibi Zahara baada ya kumuona bundi.
    Bundi akabadilika kutoka umbo la ndege mpaka Zahara,kumbe Bundi ni Zahara.
    Bibi akamuuliza Zahara
    "Ulikuwa wapi?"
    Zahara akawatazama wachawi wengine ,akarudisha macho kwa Bibi yake.
    "Nilienda kwa Babu"
    "Babu...!!!nani kakuambia uende kwa Babu yako?"
    "Bibi nisamehe,Babu ana njaa,nilimpelekea Chakula"
    "Chakula..!!"
    "Ndiyo Bibi"
    "Umekitoa wapi?"
    Zahara akavuta pumzi na kuishusha taratibu.
    "Ni mama yake na yule mwanamke aliyekuwa anataka kuolewa na Hassan" (Mama angel)
    "We zahara,tangu lini umeanza kujichukulia sheria mkononi?umeharibu kila kitu mjukuu wangu,muda wa kuwaua hao bado"
    "Bibi siwezi nikakuelewa ,ulisema utanisaidia kumpata hassan,cha ajabu umemuua,Mimi nitaolewa na nani?hee..?Kumbuka Hassan ni mwanaume wa ndoto zangu Bibi ,atanioa vipi ilihali amekufa?Kama hassan amekufa ,huyo mwanamama anahaja gani ya kuendelea kuishi?" (Zahara aliongea kwa uchungu mpaka machozi yakamtoka).
    Bibi Zahara akamkumbatia mjukuu wake.
    "Pole Sana mjukuu wangu,nisamehe kwa kukufanya ukose Furaha,ila Mimi nilitaka tumchukue hassan halafu uoane naye kwenye himaya yetu ya kichawi"
    "Nitaoana naye vipi na wakati atakuwa msukule?"
    "Hassan hatakuwa msukule,atabaki kuwa binadamu wa kawaida,kuhusu maiti watakayozika,tutawawekea mgomba ila wao wataona ni mwili wa hassan"

  • @jodastories
    @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

    **
    7b
    Baada ya kupatiwa huduma kwa muda mrefu na hatimaye lizy akaacha kurusha mikono na miguu Kama mwenye kifafa.Lizy akawa bado amelala chini.
    ndugu zake na lizy wakakubaliana wampeleke nyumbani kwao akapumzike,kijana mmoja akajitolea kumbeba lizy mgongoni kwake.
    Baadhi ya wanakijiji walioguswa na hali ya lizy wakaongozana na ndugu zake kumpeleka nyumbani. Timbwili likawa limebaki kwa mama hassan ambaye hataki kusikia neno lolote kutoka kwa wazee wa busara na hata Mume wake.
    Angel hakufurahishwa na tabia za mama mkwe wake,ukizingatia muda mchache uliopita walikuwa na ugomvi ambao chanzo chake kinafanana na hiki.Angel akaingia ndani kwa hasira,akawakuta wazee wa busara wakiwa wameinamisha vichwa chini kwa aibu maana matusi wanayopatiwa yaliwavua utu wao.
    Angel akasema
    "Jamani wazee wangu,huyu mama atakuwa amerukwa na akili naomba tumkamate"
    "Nani amerukwa na akili?we binti unanitafuta nini?" (Mama hassan akaanza kumfokea Angel)
    Angel akautazama mwili wa Mume wake Hassan uliolala kitandani,akapiga moyo konde.
    "Jamani naomba vijana wenye nguvu waje na kamba tusaidizane kumkamata huyu mama" (angel aliwaomba wanakijiji wenye nguvu kwa kupaza sauti akiwa ndani ya nyumba)
    Yanayoendelea yalikuwa ni mageni kwa wanakijiji,kila mmoja akawa na maswali lukuki kwamba inakuwaje Angel atoe amri Mama mkwe wake akamatwe? Tangu lini mama mkwe akafokewa?.
    Mama hassan alikuwa Kama kichaa ,akamsogelea angel na kumkaba shingo,ugomvi ukaanza tena ndani ya nyumba yenye maiti ya Hassan.
    Wazee wa busara na baba Hassan wakaanza kuamua ugomvi, awamu hii angel hakutaka kuonekana mzembe,alikuwa anasukumana na mama Mkwe wake bila kujali Kama yupo ukweni.
    Mzee mmoja wa busara akatoka nje
    "Jamani naomba vijana wenye nguvu wake na kamba"
    Vijana waliposikia sauti ya Mzee wa busara wakachukua kamba ngumu zilizotengenezwa kwa magome ya miti.
    "Fanyeni haraka watauana"
    Vijana wanne wakaingia ndani,wakakuta ugomvi bado unaendelea.
    Baba hassan akapaza sauti huku akiamua ugomvi
    "Mnasubiri nini?hebu mfungeni mama hassan,inaonekana hii siyo akili yake"
    Pale pale vijana wakamvamia mama hassan, wakashirikiana kwa pamoja mpaka pale walipofanikiwa kumfunga kamba Mama hassan.
    Mama hassan akawa bado anaendelea kutoa maneno machafu,akasema.
    "Kwanza Baba hassan kitandani hauna chochote"
    Hili lilikuwa ni tusi zito kwa baba hassan ,mbaya zaidi wanakijiji wote waliokuwa hapa wakasikia.
    Baba hassan akashikwa na hasira,akaenda kumpiga mke wake ngumi tatu za uso,uzito wa ngumi za Baba hassan ukapelekea mke wake kupoteza fahamu.
    Baada ya Mama hassan kupoteza fahamu,roho ya kichawi ya Bi Zahara ikatoka mwilini mwa Mama hassan.
    Bi Zahara akawa anawatazama huku anacheka,wao hawakumuona ila yeye aliwaona.
    Lengo la Bi Zahara la kumzuia Baba hassan kufanya maombi likawa limetimia,akasogea karibu na mwili wa marehemu hassan,akachukua mkia wake wa fisi anaotembea nao,akachora ishara ya msalaba juu ya mwili wa hassan kwa kutumia mkia wa fisi.
    Punde si punde roho ya Hassan ikatoka kwenye mwili wake,kila kitu, mwili ulikuwa unafanana na roho ambayo imetoka baada ya bi Zahara kufanya uchawi wake.
    Bi Zahara akaichukua roho ya Hassan na kupotea nayo kichawi,mwili ambao ulikuwa umelala kitandani haukuwa halisi bali wameachiwa gogo ambalo wao wanaliona ni hassan kumbe siyo.
    Mzee mmoja wa busara akaenda kumshika mkono Baba hassan
    "Tulia Mzee mwenzangu, utamuua bure mke wako,kukengeuka ni kawaida ya mwanadamu hasa hawa wakike,nadhani atakuwa amerukwa na akili baada ya kumuona mwanae amefariki,usiendelee kumpiga,akirudisha fahamu tutaendelea na yanayofuata,sawa?"
    **
    Wachawi wakiwa wamekaa ndani ya nyumba ya bi Zahara, wakasikia kishindo kimesikika nje.
    "Nini hicho?!!" Zahara akauliza kwa mshangao.
    Hakuna ambaye alikuwa anajua ni kitu gani ambayo kimetua nje kwa kishindo,ikabidi wachawi watoke nje.
    Walipotoka nje wakamkuta mkuu wao akiwa amesimama na Hassan.Zahara alikuwa mtu wa mwisho kutoka ndani ya nyumba, alipotoka hakuamini baada ya kumuona Bibi yake akiwa na hassan.
    "Bibi!"
    Bi Zahara akatabasamu.
    "Nimekuletea mtu wako mjukuu wangu"
    Zahara akasogea karibu na hassan,akaugusa mwili wa hassan huku akiwa haamini anachokiona.
    "La..lakini Bibi huyu anatofauti gani na hao misukule?kwanza anaonekana kutokutambua yupo wapi"
    "Kweli kabisa mjukuu wangu unachokisema,kwa Sasa hakutambui mpaka pale tukimfanyia tambiko la Pochala(kurudisha fahamu)"
    "Nitaishi naye vipi kwenye ulimwengu wa Giza?mimi nilitaka nifunge naye ndoa mbele ya wanakijiji wote"
    "Kuhusu hilo usijali,nimemleta hapa ili ufurahie naye tendo mwanangu, ukilala na huyu Usiku wa Leo,sisi sote tutazidi kupata nguvu"
    Zahara akamtazama Bibi yake kwa mshangao
    "Unataka nifanye Mapenzi na hassan ilihali hajitambui?mbaya zaidi kule kwao wanafahamu amekufa,hii inawezekana vipi?"
    "Mjukuu wangu,mpaka hapa nakuheshimu wewe kwakuwa uliamua kunichagua Mimi badala ya wazazi wako,ila huyu Kijana alipaswa kufa ,haiwezekani akutoe usichana wako halafu akatae kukuoa,mjukuu wangu,rudisha Furaha yako Usiku wa Leo kwa kulala naye,utapata faida mara mbili,raha pamoja na nguvu"
    Zahara akavuta pumzi, ni kweli hassan ndiye mwanaume wake wa kwanza,alimtoa usichana wake akamuahidi kumuoa,cha ajabu baada ya kwenda mjini akarudi na mwanamke Mwingine ambaye ni angel.
    Zahara akatafakari wema wa Bibi yake anaomfanyia kuanzia kuvuruga harusi ya hassan na angel mpaka Sasa,akamtazama hassan .
    "Bibi nilikuwa na...."
    "Najua unatamani kuolewa na huyu,kuhusu hilo usijali,ukilala naye kwenye ulimwengu wa Giza,hata akirudi katika ulimwengu wa kawaida hawezi kukukataa,hii ni zaidi ya limbwata mjukuu wangu"
    Ama hakika,'hakuna mkate mgumu mbele ya Chai',maneno ya bi Zahara yakaulainisha moyo wa mjukuu wake,akakubaliana na wazo la bibi yake kuwa Usiku wa Leo afanye Mapenzi na hassan.Ikumbukwe hassan amechukuliwa kichawi,kwenye ulimwengu wa kawaida Hasan amekufa lakini kwa Bi Zahara Hasan bado anaishi ila hajiambui ni sehemu gani yupo.
    **
    Ndugu zake na lizy walifanikiwa kumfikisha nyumbani kwao,wakatandika mkeka na kumalaza nje chini ya mti wa maembe.
    Baba yake na lizy hakuwepo,alikuwa ameenda kuchanja kuni msituni.
    Mama lizy aliumia Sana kumuona mwanae amelala chini pasipo kujitambua,wakaanza kumuita lizy kwa nguvu walau afunue macho.
    Baada ya kutumia dakika tano na hatimaye lizy akafumbua macho,lakini alipojaribu kuzungumza hakuweza,lizy alikuwa anaongea maneno yasiyoeleweka mbele ya ndugu zake.
    "Mwanangu umekuwa bubu!!" Mama yake alilia Sana,alipomtazama mdomoni mwanae akaona udenda unamtoka,ile kutazama mikono ya mwanae akaiona imejikunja,kwa ufupi Lizy amegeuka kuwa kichaa.
    **
    Upande wa pili kwa angel na Patricia,walisimama mbali na wanakijiji wengine wakaanza kujadili mambo yao.
    Angel akamuuliza Patricia
    "Tutampata wapi mama yetu?"
    "Hata Mimi sijui,ila unaonaje tukimpigia Simu Baba?"
    "Baba!!"
    "Ndiyo"
    "Baba alivyo mkali sijui Kama atatuelewa,kumbuka Patricia, Baba alikataa kata kata nisiolewe na hassan,tena ilipofika hatua tunakuja kufunga ndoa ndio akazidisha hasira Kama Mbogo,Leo hii tukimwambia mama amepotea atatuelewa?"
    Patricia akashusha pumzi
    "Dah..! Sasa tunafanyaje?mambo yenyewe kwenye hii familia ni Kama hivi,kila muda ugomvi na kutupiana lawama za kumuua mumeo"
    "Unaonaje tukisubiri kwanza,huenda tukapata namna nzuri ya kumpata mama yetu,kwa kweli siwezi kuondoka kwenye hichi kijiji bila Mama yangu".
    Patricia akasema
    " hata Mimi pia"
    Angel na Patricia wakakumbatiana, kila mmoja akiwa ameweka ahadi ya kumtafuta mama yao mzazi mpaka watakapompata.
    Itaendelea.....
    😈KIJIJI CHA MPEPO NA MASHENE KIPI NI HATARI?

  • @jodastories
    @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

    BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji)
    SEHEMU YA TANO(05)
    MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA
    MAWASILIANO: 0748862999
    **
    TULIPOISHIA.....
    Zahara alikuwa anapuliza mchanga ambao kila akipuliza kimbunga kikali kinawakimbiza Angel,Patricia na Mama yao.
    Upande wa pili kwa Baba hassan tuliishia pale ambapo ameingia ndani akidai atafanya juu chini awaoneshe wachawi kuwa yeye siyo mtu wa mchezo mchezo.
    SONGA NAYO......
    Zahara akaendelea kutuma kimbunga cha kichawi, kimbunga kilizidi kasi zaidi ya mwanzo,kikawa kimekaribia kuwafikia akina angel ambao wanakimbia mithili ya wanariadha wawapo mashindanoni.
    Walikuwa wamebakiza umbali mfupi mpaka kufika nyumbani kwa akina Hassan, ijapokuwa mita chache zimebaki ila kwao waliona ni kama kilometa Mia maana kimbunga cha kichawi kinataka kuwameza.
    Kifua cha Mama angel kikaanza kumbana,akajikuta akidondoka chini.
    "Mamaaaa" (Patricia alipiga ukunga baada ya kumuona mama yake amedondoka chini)
    Angel na yeye akageuka, ile kutupa macho anakiona kimbunga kikiwa kimemkaribia mama yao,angel na Patricia wakapiga kelele za kuomba msaada.
    "Msaada... Msaadaaaa"
    Mama angel alikuwa anahema chini,kila akitazama kasi ya kimbunga alishindwa kusimama,watoto wake walikuwa wanamuita lakini hakusikia,mama angel akakata tamaa,aliamini kimbunga hakitamuacha salama.
    Kimbunga cha kichawi kikafika mpaka alipodondoka mama angel,kikaanza Kumzunguka kwa spidi isiyopimika.Patricia akamvuta angel.
    "Twende...twende" (Patricia akawa anamvuta angel waondoke)
    "Siwezi kumuacha mama,uwiii" (angel alitamani akaingie ndani ya kimbunga na mama yake lakini Patricia alimzuia)
    Kimbunga cha kichawi kikambeba Mama angel mfano wa karatasi,pale pale kimbunga kikaanza kutokomea vichakani.Angel na Patricia walikisindikiza kwa macho kikiwa kinaondoka na mama yao,kwa mbali wakawa wanasikia sauti za mama yao akiomba msaada.
    "Msaada......"
    Angel aliumia Sana,maumivu yake hayakupimika,kumpoteza Mama yake kulizidi kutonesha maumivu ya kidonda kibichi alichonacho.
    Patricia na angel wakabaki wakiwa wamekumbatiana barabarani, kila mmoja alitokwa na machozi Kama bomba la mvua,mama yao mzazi amemezwa na kimbunga kisha kikampeleka kusikojulikana.Mauzauza yameanza kuonekana wazi mbele ya wageni wa kijiji cha Mashene.
    **
    Upande wa pili kwa Baba Hassan,aliingia ndani kisha akatoka akiwa amebeba biblia inayoonekana kuwa ya zamani kidogo.Baba Hassan akaingia kwenye nyumba yenye mwili wa marehemu,akamkuta mshenga wake na hassan akiwa analia.
    "Naomba utoke nje" (Baba hassan akamtoa nje mshenga wa Hassan).
    Baba otieno akapishana na mshenga wa hassan mlangoni,Baba otieno akaingia ndani akiwa ameongozana na wazee wawili.
    "Baba hassan unataka kufanya nini?" (Lilikuwa ni swali la Baba otieno baada ya kuingia ndani)
    Baba hassan akajibu huku akilia
    "Hebu tazama mwanangu amelala kitandani,kesho ilitakiwa afunge ndoa na mke wake,cha ajabu kesho atakuwa kwenye nyumba yake ya milele,kwa kweli sijakubaliana na hili" (akawa anajifuta machozi kwa mkono wake)
    Mzee mmoja aliyevalia kanzu nyeupe na baraghashia akamsogelea Baba Hassan, akamshika bega na kusema
    "Inatakiwa ukubaliane na hali hii ,mwanao ameshatangulia mbele ya haki"
    Baba Hassan akajibu kwa sauti iliyojaa masononeko
    "Si...si..siwezi"
    Baba otieno akamsogelea rafiki yake,
    "Sasa unataka kufanya nini na hiyo biblia?"
    "Nataka nimfufue mwanangu"
    "Umfufue?tangu lini ukawa na uwezo wa kumfufua mtu?halafu Mungu anajibu kwa wale wanaomwabudu,sasa wewe kanisani wala msikitini hauendi,Leo utafanya maajabu?" (Baba otieno alikuwa anampinga Sana Baba hassan)
    Baba otieno anaitambua siri nzima ya kifo cha hassan, yeye ndiye aliyeweka dawa nyuma ya nyumba.Baba otieno anaogopa huenda atapata matatizo kwa sababu nguvu zitaanza kukinzana.
    Baba hassan hakutaka kusikia maneno ya mtu yeyote yule,akaanza kuifungua bibilia taratibu huku akilia.
    Baba Hassan akazungumza kwa sauti ya kunong'ona
    "ee Mungu,najua huwa siendi kanisani wala msikitini,ila siku ya Leo pokea ombi langu" (Baba Hassan akaanza Kusoma mafungu ya biblia)
    **
    Angel na Patricia wakaanza kuelekea nyumbani kwa akina Hassan,vilio vya kwikwi vilitawala njia nzima,kila mmoja alikuwa haamini Kama wamempoteza mama yao.
    Patricia akasema
    "Laiti tungelimsikiliza Baba haya yote yasingelitokea" (akavuta kamasi)
    Angel alikuwa kimya akitafakari hatima ya maisha yake,anayoambiwa na Patricia yalikuwa yanaingia sikio la kulia yakanatokea la kushoto.
    Safari ya angel ilikaribia kufika tamati,wakaiona nyumba wanayotakiwa kwenda,wakasimama huku macho yao yakiitazama nyumba inayomilikiwa na familia ya Baba hassan.
    Nje kulikuwa na mapambo pamoja na turubai za kukinga jua siku ya harusi,angel akajikuta akianza kulia upya maana sehemu hiyo anayoitazama kwa mbali ndio sehemu ambayo siku ya kesho alipaswa kufunga ndoa na mume wake hassan.
    Patricia alitambua maumivu anayopitia dada yake,akamshika mkono.
    "Hatuna pa kwenda,inatakiwa tufike pale tukawaeleze mama yetu amepotea"
    "Sawa" (angel akajibu kwa masononeko)
    Angel na Patricia wakaanza kuisogelea nyumba ya akina Hassan,sehemu wanayoenda ndipo kuna msiba wa Hassan.
    **
    Baada ya jitihada za muda mrefu,hatimaye fahamu za mama hassan zikamrudia,wanawake wenzake wakampatia maji ya kunywa huku wakimpatia maneno ya kumtia moyo.
    Mama hassan alikunywa maji kisha akasimama.
    "Naombeni nitoke nje" (Mama hassan alikuwa anataka kutoka nje lakini wanawake wenzie hawakutaka atoke nje,waliogopa asije elekea kwenye nyumba uliopo mwili wa marehemu Hassan).
    Mama mmoja wa makamo akamshika mkono Mama Hassan
    "Naomba utulie kwanza mama Hassan,hebu tazama hali yako kwa sasa,haupo vizuri,kaa kwanza ndani utatoka tu"
    "Unanikataza kumuona mwanangu, hee?" (Akaanza kulia)
    "Sikukatazi mama hassan ila wewe unasumbuliwa na presha,hapa penyewe tumehangaika Sana,hofu yangu ni kukupoteza na wewe,hebu tulia kwanza"
    Mama hassan akarudi kukaa juu ya mkeka,kichwa chake akakiinamisha chini kwa mawazo,akawa anajiuliza mambo mbalimbali hasa kifo cha ghafla cha Mtoto wake.
    **
    Baba Hassan alisoma vifungu vitatu kisha akaanza kumuombea mwanae,maombi anayofanya Baba hassan alionekana Kama aliyerukwa na akili.Baba hassan alikuwa ana amini mwenyezi Mungu atamrejesha mwanae ingawaje huwa hasali.
    Baba otieno akatabasamu maana hakuna nguvu ya tofauti anayoihisi.Kwa kawaida sehemu ambayo kuna maombi ama dua nzito,mchawi na majini huwa wanahisi kitu cha tofauti mwilini mwao,ndio maana sehemu ambayo maombi/dua zimetamaraki basi mchawi hawezi kusogea.
    Kwa maombi anayoyafanya Baba hassan hayakuwa na nguvu ndio maana Baba otieno anatabasamu.
    Baba otieno akawa anazungumza kimoyo moyo.
    "Huyu anajisumbua tu,kwa uchawi wetu hakuna Mchungaji ama shekhe anayeweza kututetemesha hata kidogo"
    Wakati Baba otieno anamalizia sentensi yake,pale pale akaanza kuhisi kitu cha tofauti, kichwa chake kikaanza kumuuma mithili ya nyundo ikigongelewa katikati ya utosi wake.
    "Aghhh..." (akaugulia maumivu mpaka wazee wenzie wakamtazama)
    "Kuna nini?" (Mzee mmoja akamuuliza)
    (Akiwa ameshika mkono kichwani, Baba otieno akajibu)"Hakuna kitu,ni uchovu tu"
    Baba otieno hakusema ukweli, ila anachohisi ni zaidi ya maumivu.Akamtazama Baba hassan ambaye yupo bize kufanya maombi.
    Siyo kwa Baba otieno tu,wachawi wote waliopo chini ya Bibi Zahara walihisi kitu cha tofauti mwilini mwao,waliokuwa wamejipumzisha ndani waliamka,waliokuwa mashambani wakatupa majembe,kila mchawi akawa anatazama kushoto na kulia.
    Bibi Zahara akatoka ndani kwa kasi,na yeye alihisi kitu cha tofauti mwilini mwake,akawahi kuchukua mkia wa fisi akawa anauzungusha kila Pande za dunia(kusini ,kasikazini,mashariki na magharibi)
    Bibi Zahara akaanza kuruka ruka huku akimwaga dawa,hakuwa anaogopa kuwanga mchana tena nje kwa sababu sehemu hii anayoishi hakuna majirani.
    Baba hassan anafanya maombi na wakati huohuo wachawi wanahisi kitu cha tofauti mwilini mwao.Bibi Zahara akainua mikono juu,kibuyu cha kichawi kikashuka juu ya mikono yake,akakishika vyema.
    Bibi Zahara akaanza kupuliza kibuyu, kila alipopuliza kuna ujumbe ukawa unawafikia wachawi wake.Ujumbe walioupata wachawi ni wa dharura, na huwa wakisikia sauti hii inawabidi wafike kwa Bibi Zahara haraka Sana,yaani sehemu yoyote mchawi atakayokuwa itambidi apotee kichawi.
    Wachawi wakaanza kupotea,waliokuwa wanalima shambani na familia zao wakapotea bila ya familia kufahamu,waliokuwa ndani na wao wakapotea kichawi, kila mchawi akawa anaelekea nyumbani kwa Bibi Zahara.
    Baba otieno alipata tabu siku ya Leo,wachawi wanataka apotee lakini sehemu aliyopo ni ngumu kwake.Baba otieno akataka kutoka nje lakini Mzee mmoja akamzuia
    "Baki mpaka mwenzio amalize kufanya maombi,hata Kama anachokiomba hukielewi ni vyema ukakaa kumpatia sapoti"
    "Sa..sa..sawa" (Baba otieno alijibu kwa kubabaika maana anajua muda wowote atapotea kichawi,wasiwasi wake ni kujulikana Kama yeye ni mchawi, itakuwaje endapo akipotea mbele ya macho ya rafiki zake?)
    Baba otieno akawa anatembea huku na kule,hakuwa na sehemu ya kuelekea maana ndani wapo watu wanne,yeye,Baba Hassan anayefanya maombi pamoja na wazee wawili wanaoonekana kuwa wazee wa Busara.
    Baba Hassan anafanya maombi na wakati huohuo wachawi wameanza kukusanyika nyumbani kwa Bibi zahara.Baba otieno hajapata mbinu ya kutoka ndani asije onesha upande wake wa pili wa shilingi.Endapo akipotea kichawi sasa hivi itaonekana kuwa yeye ndio mchawi anayehusika na kifo cha Hassan.
    Angel na Patricia wakafika nyumbani kwa akina Hassan,majonzi mazito yalikuwa upande wao, wakikumbuka muda si mrefu wamempoteza mama yao ndio wakazidi kulia.Ndugu,jamaa na marafiki waliokuwa eneo hili wakawafariji angel na Patricia. Wanawake waliokuwa nje wakawachukua angel na Patricia mpaka ndani ya nyumba ambayo yupo Mama yake na Hassan.
    Itaendelea.....
    😈MAMA ANGEL YUPO WAPI?
    😈BABA OTIEONO ANAUMBUKA HUKU.

    • @NURUABDALLAH-r1k
      @NURUABDALLAH-r1k 5 หลายเดือนก่อน +1

      ❤❤

    • @jodastories
      @jodastories  5 หลายเดือนก่อน

      @@NURUABDALLAH-r1k endelea kuwa karibu nasi,na Kama bado hauja-subscrbe bonyeza alama ya subscribe