KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA JUMAPILI (IBADA YA KWANZA) 15/ 12/ 2024
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 14 ธ.ค. 2024
- KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA JUMAPILI (IBADA YA KWANZA) 15/ 12/ 2024
UJUMBE WA LEO: TUBUNI NA KUIAMINI INJILI
GEUKA UMRUDIE MUNGU TENA
Marko 1 : 1 - 3
Isaya 41 : 10 - 12
Zaburi 51 : 1 - 19
Marko 1 : 1 - 3
1 Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
2 Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.
3 Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Isaya 41 : 10 - 12
10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
11 Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.
12 Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe;
watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.
Zaburi 51 : 1 - 19
1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.
9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.
10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
11 Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
12 Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
13 Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.
14 Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na damu za watu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
15 Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako.
Zaburi 51:16 (SUV)
16 Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
18 Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako, Uzijenge kuta za Yerusalemu.
19 Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki, Na sadaka za kuteketezwa, na kafara. Ndipo watakapotoa ng'ombe Juu ya madhabahu yako.
Mhubiri: Mch. Anna Kuyonga
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
TH-cam: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe: Kijitonyamalutheran@gmail.com