KOCHA MPYA SIMBA AANZE KUYAFANYIA KAZI MAMBO HAYA MATATU MUHIMU

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 30 ก.ย. 2024
  • KOCHA AJAE WA SIMBA ANATAKIWA KUANZA KUYAFANYIA KAZI MAMBO HAYA MATATU NAYO NI
    KUTENGENEZA TIMU YA USHINDANI
    Kocha ajae Simba , moja kazi atakayokuwa nayo kwenye kikosi hicho ni kutengeneza timu mpya itakayo kuwa na muunganiko
    Hii ina maana sehemu kubwa ya wachezaji wa Simba wataondoka baada ya wengine kumaliza mikataba, lakini wengine wataachwa na kuuzwa, kutokana na wachezaji wengi msimu uliopita kuonekana kuwa chini ya kiwango hali ilyochangia timu hiyo ikose matokeo mazuri kwenye mechi zake.
    Uongozi wa timu hiyo tayari umeshasema kuwa kuna wachezaji wataondoka kwenye timu hiyo
    Hapo kocha mkuu atakuwa na kazi ya kuijenga timu hiyo upya bila kujali wachezaji atakaowasajili yeye ama atakaowakuta.
    KUTULIZA PRESHA YA MASHABIKI
    Kila Mwanasimba anatamani kuiona timu hiyo inatwaa makombe msimu ujao baada ya kuyakosa kwa misimu mitatu mfululizo. Hiyo tayari ni presha kwa kocha mpya atakayetambulishwa Simba kwa kuwa mashabiki hawawezi kuvumilia kukosa ubingwa msimu wa nne mfululizo.
    Kocha mpya ana kazi ya kurejesha furaha na kupunguza presha kwa wadau, wanachama na mashabiki wa timu hiyo ambao wamechoka kushuhudia watani wao Yanga wakitwaa makombe kila msimu, lakini Kwa sasa
    wanataka kuona timu hiyo inatimiza malengo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika angalau kufika nusu fainali.
    KURUDISHA HESHIMA YA DABI
    Jambo lingine ni Dabi ya Kariakoo. Mechi yenye mvuto na msisimko wa hali ya juu.
    Kocha mpya wa Simba anakuja wakati timu hiyo ikiwa na kidonda kikubwa kutoka kwenye dabi. Imepoteza mechi mbili zote za ligi kwa msimu uliopita mbele ya mtani wake, Yanga na kubwa zaidi ilichapwa idadi kubwa ya mabao kwa jumla ya 7-2 kwenye mechi mbili za ligi.
    Kocha atakutana na presha hii na kwa bahati mbaya mechi yake ya kwanza ya mashindano itakuwa dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Akishinda ataanza kurudisha imani kwa mashabiki wa timu hiyo bila kujali wanachezaje
    Hata hivyo Inaelezwa kwamba Steve Komphela ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya Golden Arrows inayoshiriki Ligi kuu ya Afrika Kusini, anatajwa kuwa Mrithi wa nafasi ya Benchika ambayo ilikuwa ikikaimiwa na Juma Mgunda.
    Simba na Coastal Union wamemalizana na Kocha Mgunda ambaye, atajiunga nao kama kocha mkuu ili kukinoa kikosi hicho cha Wagosi wa Kaya kwenye mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho, ratiba inaonesha Agosti michuano hiyo itaanza kwa timu zinazoanzia hatua ya awali kabisa. #simba #yanga #trending #simbanayanga #alikiba #biashara #dar #china #singidabigstars#mambomatatu ya kufanyika kazisimba#kocha MPYAsimba

ความคิดเห็น •