Maelekezo ya Mheshimiwa Dkt Pindi Chana kuhusu mifumo

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 31 ธ.ค. 2024
  • Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa Mashamba na Wilaya wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kutumia Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuboresha utendaji kazi na kuchagiza utawala bora.
    Ameyasema hayo katika mkutano wa Tatu wa Makamanda wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) uliofanyika leo Novemba 5, 2024 kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha.

ความคิดเห็น •