Kitabu cha Hosea - Sura ya 1 Hadi ya 14

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 5 เม.ย. 2020
  • #Hosea, #Hosea, #Biblia, #Bible
    Hosea ~ Sura ya 1 Hadi 14
    UTANGULIZI
    Hosea aliitwa kuwa msemaji wa Mungu katika nchi yake, yaani katika utawala wa kaskazini wa Israeli, mnamo mwaka 750-725 K.K. Alitanguliwa na nabii Amosi ambaye pia alihubiri katika utawala wa kaskazini wa Israeli.
    Hosea anashutumu vikali ibada za miungu ya uongo ya nyakati zake na ukosefu wa imani kwa Mungu miongoni mwa Waisraeli. Hali hiyo ya kumwasi Mungu Hosea anailezea kwa picha ya maisha yake ya ndoa. Kama vile mkewe Gomeri alivyomgeuka na kuacha kuwa mwaminifu, ndivyo watu walivyomwacha Mungu. Kwa sababu hiyo, watu wa Israeli wataadhibiwa. Hata hivyo mwishowe Mungu, kwa upendo wake mkuu, atawarudisha na kurejesha uhusiano wake nao.
    Sura 1-3 yaelezea maisha ya ndoa ya Hosea na mkewe ambayo ni kielelezo cha uasi wa Waisraeli kwa Mungu. Hosea anatangaza hukumu ya Mungu kwa watu wote, lakini anaonesha pia kwamba mwishowe upendo wa Mungu utashinda.
    Sura 4-14 yahusu mahubiri mengine ya nabii.

ความคิดเห็น •