TFS Community Support wilaya ya Rombo.
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 31 ธ.ค. 2024
- Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ni washirika na wadau katika miradi ya maendeleo iliyopo katika jamii. Wakazi waliopo karibu na maeneo ya uhifadhi wamekuwa wanufaika wakuu hasa kipindi cha uvunaji katika hifadhi za misitu pale wanapata gawio ili kuweza kuwekeza kwenye huduma mbalimbali za kijamii kama elimu, barabara, hospitali nakadhalika.
Uhifadhi unaofanyika katika Shamba la miti Rongai umewanufaisha wakazi wa maeneo hayo kwa kuwapa fursa mbalimbali kama;
Ajira ili kuweza kukidhi mahitaji yao muhimu ya kila siku.
Wamenufaika kwa kupewa vipande katika shamba ili kufanya shughuli zao za kilimo.
Vilevile uwepo wa shamba la miti Rongai umeweza kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi jinsia ya kike katika shule ya sekondari Motamburu ili kupata huduma ya malazi shuleni. Bweni hilo limekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi hao hasa kwa wale wanaotokea vijiji vya jirani kutokana na umbali uliopo ili kufika shuleni.
Ni jukumu letu sote kutunza uoto wa asili ili kuendelea kunufaika kupitia hifadhi hizi.