GESI ASILIA || NISHATI MBADALA “ namna bora ya kuokoa misitu ya asili katika hatari ya kutoweka.
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 31 ธ.ค. 2024
- Gesi asilia ni nini?
Ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali kama methani zilizotokana na kuoza kwa mata ogania (viumbe hai) kama mimea ya miaka mingi iliyopita.
Upatikanaji wake;
Gesi asilia inapatikana katika ardhi yenye mwamba wenye vinyweleo vingi ulioko chini ya ganda la mwamba imara zaidi unaozuia gesi kupanda juu zaidi. Gesi asilia hutumiwa katika matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na upishi majumbani, sehemu za biashara na hupatika ama kwa bomba hadi kila nyumba au katika chupa za gesi.
Uhamasishaji wa matumizi ya gesi asilia umelenga kupunguza uchafuzi wa mazingira, matumizi na gharama za kununua mkaa na kuni pamoja na adha kutafuta kuni porini kwa ajili ya kupikia ili kuokoa misitu ya asili katika hatari ya kutoweka.
Wakala wa huduma za misitu Tanzania pamoja na wadau wa nishati wanahamasisha matumizi ya nishati mbadala(gesi asilia) kama namna bora ya kuhifadhi misitu ya asili na mazingira kwa ujumla kwa kutenga fedha ili kuwekeza katika miundo mbinu ya gesi asilia, kutoa elimu ya matumizi na upatikanaji wake pamoja faida za kutumia gesi asilia ili kuitunza misitu yetu. Misitu ni mali, misitu ni uhai.