AEISH AKABIDHI VIFAA TIBA VYA MILIONI 170 KITUO CHA AFYA MATANGA NA MOLLO.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 15 ต.ค. 2024
  • AEISH AKABIDHI VIFAA TIBA VYA MILIONI ITUO CHA AFYA MTANGA NA MOLLO.
    Mbunge wa Sumbawanga Mjini Mhe.Aesh Hilaly Leo Tarehe 10 Julai, 2024 amefanya Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo katika Kituo Cha Afya Mtanga na Kituo cha Afya Mollo na kuchangia Vifaa tiba ili kuboresha Mahitaji na huduma za Afya katika vituo husika.
    Katika kituo cha Afya Matanga na Mollo Mhe. Aeshi amechangia vifaa vyeny thamani ya Shilingi Milioni 170 ambavyo ni vitanda vya kulalia wagonjwa na vya kuzalishia,mashuka,magodoro,meza na Tripod stand kwa ajili ya kutundikia dawa na katika kituo cha Afya Mollo amekabidhi vitanda 10,Mashuka 60,meza 7, na Stendi za kutundikia dawa.
    Akikabidhi vifaa tiba hivyo Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe.Aeshi Hilaly ameeleza kuwa adhma yake katika jimbo hilo ni kuhakikisha kata zote zinakuwa na vituo vya Afya ili kupanua wigo wa utoaji huduma kwa wananchi na kupunguza changamoto.
    Mhe.Aesh ameeleza kuwa katika kipindi chake cha Uongozi tayari kata 7 zimefanikiwa kuwa na vituo vya Afya na tayari vinafanya kazi hali inayochangia kuboresha huduma za Afya kwa wananchi na kuokoa gharama za wananchi kufuata huduma za Afya kwa umbali mrefu kama ilivyokuwa hapo awali.

ความคิดเห็น • 1

  • @justinekiboko616
    @justinekiboko616 3 หลายเดือนก่อน +1

    Kazi nzuri sana mh Aesh mtu bingwa sana💪