VITABU VYA MUSA (PENTATEUCH).....SEHEMU YA 1

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 19 ก.ค. 2022
  • VITABU VYA MUSA (PENTATUKI)
    Malengo ya mada.
    Baada ya kumalza mada hii mwanafun zi ataweza:
    • Kueleza maana ya Pentatuki.
    • Kueleza maana ya torati.
    • Kufafanua maana ya kila jina la vitabu vitano vya Musa.
    • Kutaja watu mashuhuri katika kila kitabu
    • Kueleza matukio makuu katika kila kitabu
    • Kutaja mitajo ya Kristo katika kila kitabu
    • Kutaja baadhi ya mafundisho makuu katika kila kitabu
    • Kutaja mistari ya Msingi katika kila kitabu N.k
    I. Utangulizi.
    Katika mada hii tutatazama vitabu vyote vya Musa kwa muhtasari
    Tutachunguza mwandishi, matukio makuu, watu mashuhuri, muundo, mtindo,mafundhisho makuu, mitajo ya Kristo na mistari ya msingi au kiini cha kila kitabu.
    Vitabu vitano vya kwaza vya Biblia hujulikana kama vitabu vya Musa. Pia huitwa Sheria au Torati. Vitabu hivi hufanya katiba ya thiolojia kwaajili ya taifa la Israeli na pia vina misingi ya kweli iliyodhihirishwa na Mungu ambapo juu yake ukristo husimama. Vitabu hivi vitano vinatoa taarifa tangu mwanzo wa uumbaji hadi wakati wa matayarisho ya kuingia nchi ya ahadi yaani Kaanani.
    Pia vitabu vitano vya kwanza vya Biblia hujulikana kama Pentatuki ambalo ni neno la kiyunani lililotokana na maneno mawili ya kiyunani ambayo ni Penta maana yake tano na Teuchos maana yake kitabu.
    Hapo awali vitabu vyote hivi vitano vilikuwa kitabu kimoja tu, lakini viligawanywa kuwa vitabu vitano li kurahishisha kuvitunza katika magombo matano.
    Wayahudi walikitaja kitabu cha Pentatuki kuwa sheria tu.(2Nya 17:9, Neh 8:1-3,18, Mt 5:17, Luk 24:44).
    Kimsingi haiwezekani kuzifahamu vizuri sehemu zingine za Biblia bila ya kuvifahamu vitabu hivi vitano vya kwanza.
    Vitabu hivi vitano ni muhimu sana kwa kwa sababu vinatusaidia katika kuelewa:
    Mungu mwenyewe
    Mwanzo wa ulimwengu na mwanadamu.
    Msingi wa mawazo ya kithiolojia kama vile
    -Dhambi
    -Wokovu
    -Utakaso
    -Imani. N.k.
    Mwandishi wa Pentetuki. Katika mapokeo ya Kiebrania na ya Kikristo tangu zamani Musa anatambuliwa kuwa ndiye mwandishi wa Pentatuki.(Neh 8:1, 13:1, Dan 9:11, Mk 12:26.
    Pentatuki yeenyewe haielezi kwamba Musa ndiye mwandishi wake isipokuwa inaonesha kazi za uandishi ambayo Musa aliifanya. Aliandika sheria ambayo Mungu aliwapa wana wa Israeli Kut 24:4, 34:27, Kum 31:9,24, Kut 17:14, Hes 33:2. N.k.
    Ufunguo katika usomaji wa Agano la kale:
    1. Kuchunguza yale yaliyotokea kwa watu wa Munguwa kale. (Taifa la Israeli na watu wa Agano la kale.)
    Matukio yaliyoandikwa katika Agano la kale ni halisi yalitukia kama Agano la kale linavyoeleza.
    2. Kutazama unabii kuhusu Yesu Kristo. Bwana Yesu Kristo ameoneshwa katika kila kitabu cha Agano la Kale. (Mt 5:17-18, Yn 5:39).
    3. Kutazama utimizo binafsi. Kuangalia kile Agano la Kale linachomaanisha kwetu sasa.
    +255 763 53 89 42

ความคิดเห็น •