Tanesco kuajiri watumishi wapya 430 mwaka 2024/25

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 20 ส.ค. 2024
  • Bunge limeelezwa kuwa watumishi 430 wataajiriwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika mwaka 2024/25.
    Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 19,2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini Daimu Mpakate.
    Mbunge huyo amehoji ni lini Serikali itaajiri Madereva na Mafundi ambao wamekuwa vibarua wa muda mrefu Tanesco.
    Akijibu swali hilo, Kapinga amesema Tanesco imekuwa likiajiri watumishi wa kada mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya kiuendeshaji na uwezo wa kibajeti kwa mwaka husika.

ความคิดเห็น •