HALOTEL YAWAPA TABASAMU WATEJA WENYE KIPATO CHA CHINI

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 12 ก.ย. 2024
  • HALOTEL YAWAPA TABASAMU WATEJA WENYE KIPATO CHA CHINI
    KATIKA kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano nchini, Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel imeendelea kubuni mbinu mpya kuhakikisha kwamba wateja wake wa kada zote wanapata suluhisho la changamoto ya gharama za mawasiliano na kupata huduma kwa urahisi zaidi.
    Hii ni mkakati wa kuendelea kuboresha huduma, Halotel imepunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wake kwa kuzindua huduma mpya ya vifurushi maalum kwa Halopesa ili kuwawezesha wateja wa mtandao huo kuepuka gharama kubwa za mawasiliano.
    Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo mara baada ya kuwapa elimu wateja wa mtandao huo eneo la stendi ya Makumbusho jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa mtandao huo, Stella Pius, amesema kuwa huduma hiyo itawawezesha wateja wote nchi nzima kuweza kununua vifurushi maalum kupitia Halopesa ambapo wamezingatia uhitaji wa mahitaji yao.
    “Huduma hii inawalenga wateja wa vipato vya chini wanaofanya mawasiliano yanayolingana na wenye vipato vya kati lakini wanapata huduma hii kwa gharma nafuu kwa kujiunga kupitia Halopesa tofauti na wateja wengine,”alisema Stella.
    Aliongeza kuwa Halopesa ni huduma ambayo inaendelea kukua zaidi ambapo mbali na mteja kuweza kupata huduma za miamala ya kifedha, kulipa bili mbalimbali simu za mkononi, lakini pia anaweza kujiunga na vifurushi mbalimbali kwa punguzo la gharama ya asilimia 30 ya kiasi cha pesa atakachotumia na punguzo la kiasi hicho cha pesa atawekewa kwenye akaunti yake ya muda wa maongezi ambapo anaweza kutumia apendevyo.
    Subscribe muda huu / uwazi1
    Install #GlobalPublishersApp
    Android: bit.ly/2AAQe1d
    iOS: apple.co/2Assf4M
    Subscribe / uwazi
    FACEBOOK: / globalpublis. .
    TWITTER: / globalhabari Visit globalpublishe..., Subscribe / uwazi1
    Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… / uwazi1 / uwazi1 / uwazi1 WEBSITE: globalpublishe... FACEBOOK: / globalpublis. . TWITTER: / globalhabari INSTAGRAM: / globalpubli .

ความคิดเห็น •