Angalia maajabu ya ngoma ya KEYAMBA kutoka milima ya Uluguru

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 2 ต.ค. 2024
  • JUU AFRIKA ni tamasha pekee linalofanyika katika vilele vya safu ya milima ya Uluguru.
    Ni tamasha linalowakutanisha watu waishio kando ya misitu ya asili ya Uluguru ambako juu yake kuna uwanda wa maajabu wa Lukwangule.
    Unapofika katika tamasha hili utapewa nafasi ya kupanda milima mpaka uwandani na kuona maajabu ya uumbaji. Vyanzo vidogo vya maji vinasababisha mto mkubwa unaopeleka maji katika bonde la mto Ruvu. Usipende kusimuliwa kwa mambo unayoweza kushuhudia mwenyewe. Njoo usikie sauti ya maji yanayopita chini ya ardhi na kuibuka juu na kupotea tena ardhini. Utashangaa kukanyaga ardhi inayonesanesa katika sehemu moja wapo ya uwanda huo. Ukifika Lukwangule utaelewa vizuri kwanini ni muhimu kulinda na kutunza misitu ya asili ya Uluguru na kwingineko. Utakunywa maji masafi na salama yasiyokuwa na madawa wala uchafu. Ni maji yenye ladha ya kipekee yatakayokutamanisha kunywa wakati wote.

ความคิดเห็น • 13