Longido waanza kunufaika na biashara ya hewa ya ukaa

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 5 ก.พ. 2025
  • Arusha. Zaidi ya wananchi 40,000 wa vijiji vitano wilayani Longido, wameanza kunufaika na biashara ya hewa ya ukaa baada ya kulipwa Sh372.3 milioni kama malipo ya awali kwa ajili utekelezaji wa mradi wa nyanda za malisho.
    Vijiji hivyo vitano ni sehemu ya vijiji 16 ambavyo vilisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa hewa ukaa ya udongo na kutenga jumla ya hekta 71.656.3 kwa kwa ajili ya nyanda za malisho ya mifugo.
    Akipokea hundi ya fedha hizo leo Juni 20, 2024 kwa niaba ya vijiji hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marko Ng'umbi amesema mradi huo utanufaisha wananchi katika utekelezaji wa miradi ya elimu, maji na afya lakini pia itasaidia mateso ya nyanda za malisho kukoma na na kupatikana mifugo bora.

ความคิดเห็น •