Kipindi cha Ujuzi ni Maisha Mafunzo kwa madereva wa magari makubwa
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 17 ม.ค. 2025
- Takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa ajali nyingi za barabarani katika ukanda wa Afrika Mashariki zinatokana na kutozingatia sheria za barabarani na hilo huchangiwa kwa kiasi kikubwa na madereva wengi kuendesha magari pasipo kupitia mafunzo stahiki.
Tanzania imetunga sheria na taratibu nzuri za vyombo vya usafirishaji na matumizi ya barabara. Miongoni mwa sheria na taratibu hizo ni pamoja udhibiti wa mwendo kasi, kuzuia mtu kuendesha akiwa amelewa na kuhimiza matumizi ya vifaa vya usalama kama mikanda, kofia za ngumu yaani Helmet na hata viti maalumu kwa watoto. Hata hivyo, madereva wengi hawazingatii.
VETA inatambua changamoto hiyo na imekuwa ikihimiza mafunzo kwa watumiaji wote wa vyombo vya moto na imekuwa ikitoa mafunzo ya udereva karibu katika kila chuo chake.
Katika kipindi hiki tumeangazia Mchango wa VETA juu ya Mafunzo kwa madereva wa magari makubwa yanayotolewa katika chuo cha VETA Kihonda mkoani morogoro.
Mpo vizuri sana kihonda
Maashaallah maashaallah
Hongera veta kihonda,,mimi ni mmojawapo nije kupata mafunzo ya magazine makubwa
Ada
Naomba mawasiliano ya sim
Course ya udereva ni muda gani na inachukua miezi mingapi?
Nataka kujifunza Basi na garama kiasi gani
Natakakujifunza maloli nawezanikapatanfas
Natakiwa niwe na nini ili niweze kujiunga
Kujifunza shingapi kwamdagani
Nataka kusoma ufundi magari naweza nikapata nafasi
Mafunzo ya magari makubwa