Fahamu mengi kuhusu Uhamiaji Mtandao

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 30 ม.ค. 2018
  • Uhamiaji Mtandao (e-immigration) ni muunganiko wa mifumo mbalimbali ambayo imesanifiwa kufanya kazi kwa pamoja na kutoa taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za kiuhamiaji.
    • Kupitia teknolojia hiyo, Idara itaweza kutoa viza za kielektroniki (e-Visa),
    • Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki (e- Residence Permit),
    • Pasipoti za Kielektroniki (e-Passport)
    • Pamoja na kusimamia masuala ya mipaka kielektroniki (e-Border Management).
    Mfmfumo huo wa Uhamiaji Mtandao unalenga kutusaidia;
    • kutoa Pasipoti ya Kielektroniki ya Afrika Mashariki (e-Passport) ambayo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambapo itakuwa na ‘chip’ iliyobeba taarifa mbalimbali za mwombaji pamoja na alama nyingi za kiusalama “Security Features”
    • Mfumo utasaidia kudhibiti na kuwezesha Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Raia na Wageni wanaoingia nchini kwa madhumuni mbalimbali hususan katika maeneo ya mipakani ikiwa ni pamoja na kutunza kumbukumbu zao. Hii itasaidia kuzuia ongezeko la wahamiaji haramu nchini.
    • Pia utasaidia usimamizi wa utoaji viza na mwombaji atawasilisha maombi yake kwa njia ya kielektroniki; hii itasaidia kupata taarifa za malipo ya viza kwa wakati na, kudhibiti upotevu wa maduhuli ya Serikali.

ความคิดเห็น •