Ufafanuzi wa Rais Magufuli kuhusu kuminywa kwa demokrasia Tanzania

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 26 ก.ย. 2024
  • Ni wakati wa mkutano kati ya viongozi wa dini na Rais Magufuli uliofanyika Januari 23, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo mchungaji Amani Lyimo wa KKKT alitoa ushauri kuhusu suala la demokrasia nchini.
    “Baba unafanya kazi sana, lakini Baba Demokrasia,Watanzania wengi wana hofu, wengi hawathubutu kuzungumza wana hofu...nakuomba Rais kama kuna uwezekano Baba waachie pumzi wazungumze.."
    Akijibu hoja hiyo, Rais Magufuli alikanusha kuhusu kuwepo kwa suala hilo akifafanua kuwa hakuna mahali ambapo demokrasia imeminywa nchini Tanzania na kusisiza kuwa viongozi wote wa kisiasa wako huru kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo yao pekee.
    Rais Magufuli amesema alichokizuia ni maandamano na mikusanyiko ya kisiasa yenye vurugu ndani na inayoambatana na matusi kutoka upande mmoja kwenda mwingine jambo linaoweza kusababisha uvunjivu wa Amani.

ความคิดเห็น • 18