TFS| SHAMBA DARASA WILAYA YA NJOMBE “kutuondoa kwenye utofauti wa kupanda miti kimazoea"
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 31 ธ.ค. 2024
- Wakala wa huduma za misitu Tanzania ni wadau wakubwa wa miradi na mipango ya maendeleo katika jamii zetu, inafanya hivi kwa kuweka mahusiano ya karibu sana na jamii kwa kutoa elimu, mafunzo, ushauri na ushirikishaji wa mipango yenye tija kwa maendeleo kama kutunza mazingira, kuhifadhi vyanzo ya maji, uhifadhi wa mazao ya misitu nakadhalika.
Elimu (shamba darasa) inayotolewa kwa wadau wa mazao ya misitu, kwenye mashamba ya vikundi na jamii kwa ujumla inatoa fursa ya mafunzo haya kwa vitendo kwa kuwawezesha kupata mbegu bora za mazao ya misitu, uandaaji wa shamba, ushauri pamoja na misaada mbalimbali lengo likiwa ni kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa mazao ya misitu na kuwasaidia
wakulima kupata thamani ya mazao yao katika soko la mazao ya misitu.
Wakazi wa kijiji cha Mikongo wilayani Njombe wamepata fursa ya kushiriki katika mafunzo haya ikiwa ni mwendelezo wa kueneza elimu hii katika jamii ili kuendelea kunufaika na Mazao ya misitu na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
Ni jukumu letu sote kuendelea kushirikiana wa wakala wa huduma za misitu Tanzania katika uhifadhi wa mazao ya misitu kwaajili ya kizazi cha sasa na cha baadae.