UTAPENDA MAPOKEZI YA KIDUNDA SONGEA NI BALAA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 24 ก.ค. 2022
  • Bondia Mtanzania Seleman Kidunda Amepokelewa na wazee Wa kimila na kupewa baraka Kuelekea Pambano La Kimataifa La " PAYBACK NIGHT Dhidi Ya Mkongo Man Erick Katompa Litakalopigwa Julai,30, Mwaka huu Katika Uwanja Wa Maji maji songea Mkoani Ruvuma.
    Akizungumza Seleman Kidunda Mara Baada Ya kupokelewa na wazee wakiongozwa na chifu Wa Wilaya hiyo Amesema amefurahishwa na mapokezi hayo kwani ni ishara ya kumtakia heri Kwenye Pambano lake na kuahidi Ushindi usiku huo.
    Kwa Upande Wake Chifu Yasin Yusuf Mbano Amesema Washatimiza wajibu wao kwa kuweza kumtambua bondia huyo kwa kuwa ni kijana wao ambaye wanaamini atashinda pambano lake na kuheshimisha nchi kimataifa.
    Wezee hao wakimila waliongozwa na chifu Yasin Yusuph Mbano ambaye amsimika kama shujaa wao kabla ya msafara wake kukatisha katika mitaa mbalimbali wilayani hapo na kuelekea kwenye Makumbusho ya vita ya majimaji ambapo aliweza kuweka shada la mauwa katika kaburi moja walilozikwa mashujaa 66 walionyongwa na mkoloni wa Kijerumani.
  • กีฬา

ความคิดเห็น • 2