MASWALI NA MAJIBU YA BEMBEA YA MAISHA/ DONDOO / KCSE PREDICTION/ MASWALI ZAIDI YA BEMBEA YA MAISHA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 1 พ.ย. 2024
  • MAJIBU ni haya 👇
    • MAJIBU YA MASWALI YA #...
    Filamu hii ina maswali ya Tamthilia ya #BEMBEA YA MAISHA kumi na Matango. Maswali haya yatamsaidia msomi kudurusu kitabu hiki cha tamthilia na kujiandaa kwa mtihani wa Kitaifa wa KCSE. Kuna video zingine za maswali kama haya na pia kuna zingine za kuonyesha majibu ya maswali mengine. #kiswahili #nguu #maudhui #nafasi
    MAJIBU yake yako kwa link hii:👇
    • MAJIBU YA MASWALI YA #...

ความคิดเห็น • 71

  • @FurahaJuma-f5l
    @FurahaJuma-f5l 6 วันที่ผ่านมา +2

    Asante Mwalimu kwa hayo machache

  • @ReheriChacha
    @ReheriChacha วันที่ผ่านมา +1

    Swali la kumi jibu msemaji n bunju n msemewa n neema ni nyumbani kwao bunju na neema ❤❤

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  18 ชั่วโมงที่ผ่านมา

      Asante 🤗

  • @MageboAmos
    @MageboAmos หลายเดือนก่อน +3

    Kazi nzuri sana.Asante kwa kutupevusha kupitia maswali haya.Mola aibariki kazi yenu

  • @faithNafula-x5c
    @faithNafula-x5c 3 วันที่ผ่านมา +1

    n nzuri sana

  • @LucyMwangi-b5i
    @LucyMwangi-b5i 9 วันที่ผ่านมา +1

    Mwalimu Asante kwa maswali lakini majibu

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  9 วันที่ผ่านมา

      MAJIBU yapo kwenye comments, na yenye hayapo kwa comments kuna video tofauti na majibu yake

  • @MageboAmos
    @MageboAmos หลายเดือนก่อน +4

    Astaghafirulahi!kazi nzuri.Pongezi.

  • @VictimMlaguzi
    @VictimMlaguzi 29 วันที่ผ่านมา +1

    Asante sana na Mola azidi kuwabariki

  • @PelesiaMuga-o1r
    @PelesiaMuga-o1r 6 วันที่ผ่านมา

    Mwalimu nmeshindwa nice majibu tafadhali

  • @FaithWangui-s9e
    @FaithWangui-s9e 2 หลายเดือนก่อน +2

    ✅ done,,,, hongera mr.wanjala 👏

  • @ReheriChacha
    @ReheriChacha วันที่ผ่านมา +1

    Mbona hupeani majibu🎉🎉

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  15 ชั่วโมงที่ผ่านมา

      Majibu yapo, Kila swali liko na video yake na jibu

  • @saeedmualim9592
    @saeedmualim9592 2 หลายเดือนก่อน +2

    Asante mwalimu tukidurusu maswali haya na nyingine ya sampuli hiyo tutapita mtihani mia fil mia InshaAllah.

  • @BerylMalaba
    @BerylMalaba 2 หลายเดือนก่อน +2

    ❤❤❤

  • @SharonBarasa-m6h
    @SharonBarasa-m6h 8 วันที่ผ่านมา +1

    Mwalimu Asante kwa maswali lakini naomba majibu

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  8 วันที่ผ่านมา

      MAJIBU yote yako kwa comments, angalia comments utapata majibu hapo

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  8 วันที่ผ่านมา

      Au pia Taja swali unataka MAJIBU yake nikupee

  • @PatrickOdokeOdoke
    @PatrickOdokeOdoke หลายเดือนก่อน +3

    Mwalimu swali langu ni bainisha namna elimu katika bembea ya maisha imekumbwa na changamoto

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  หลายเดือนก่อน

      Kuja WhatsApp nikujibu kaka...

  • @JaneAkinyi-z2r
    @JaneAkinyi-z2r หลายเดือนก่อน +5

    Swali langu ni namna matumizi ya kisengere nyuma imejitokeza katika bembea

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  หลายเดือนก่อน +2

      1.Sara anakumbuka namna alivyopewa masomo ya unyago na nyanyake namna ya ya kuisha maisha ndani ya ndoa.
      2. Yona anakumbuka akiwa miongoni mwa vijana wa kwanza kijijini mwao kuingia kwa dini.
      3. Yona anahadithia wazee wenzake wa kijiji, Luka na Beni namna alivyokuwa akirauka mapema shuleni.
      4. Yona anaambia wazee wenzake kwenye kikao kuwa hizo enzi akiwa mwalimu viboko viliruhusiwa. Yeye binafsi hakuwahi kukosa kiboko mkononi.
      5. Yona anasema babake Kalasinga alikuwa mwafrika wa kwanza kuajiriwa na mhindi na kufanya kazi na kupandishwa cheo hadi akawa dereva.
      6. Neema anakumbuka namna Yona alivyokuwa mkali, kuwagombeza na kuwapiga.
      7. Sara anaambia Asna kuwa aliachia masomo kwa darasa la Saba kwa sababu enzi zao katika jamii Yao elimu ya mtoto wa kike ilifanyiwa bezo. Akishabaleghe aliozwa kwa lazima.
      8. Kiwa anaambia Dina namna Neema walivyokuwa kama ncha ya sindano masomoni na pia akiangalia mtu usoni ungeona akizisoma fikra zake.
      9. Sara na Dina wanasema kuwa kuna mabadiliko upande wa usafiri, kitambo wangechukua siku nyingi kufika mjini.
      10. Bunju anapogorofishana na Neema , anamkumbusha mahali alimpata kwa ajali mbaya na kumuitia flying doctors na kusimamia gharama ya hospitali .
      11. Bella anaambia Neema kuwa kitambo Mila zilifwatwa kwa Sana. Sasa hivi mambo ya mila yamepitwa na wakati. Sara anaweza lala kwa Bunju.

    • @LucyMuhia-x4r
      @LucyMuhia-x4r 9 วันที่ผ่านมา +2

      Pale ambapo bunju anamkumbusha neema alivyompata Hali mahututi na kumpeleka hospitali,

    • @LucyMuhia-x4r
      @LucyMuhia-x4r 9 วันที่ผ่านมา +2

      Pale ambapo tunapata Yona anakumbusha beni vile alivyokuwa akirauka na kwende shuleni na kufunza wanafunzi

    • @LucyMuhia-x4r
      @LucyMuhia-x4r 9 วันที่ผ่านมา +2

      Pale ambapo Sara anamkumbusha neema vile babayao alivyoshika rekodi na kuwa na akila za ncha

    • @LucyMuhia-x4r
      @LucyMuhia-x4r 9 วันที่ผ่านมา +2

      Hio ndo kisengere nyuma mmi ni mwanafunzi

  • @Hani-s7p
    @Hani-s7p 5 วันที่ผ่านมา +1

    Tafadhali naweza pata majibu

  • @alfredmaria9833
    @alfredmaria9833 12 วันที่ผ่านมา +1

    Jibu yote mwalimu tafadhali

  • @MahmudBaba-f6p
    @MahmudBaba-f6p หลายเดือนก่อน +1

    Mr hi naomba sana majibu kw
    a sahi

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  หลายเดือนก่อน

      Sema swali nikupee majibu

  • @PetersonJohn-o2k
    @PetersonJohn-o2k 5 วันที่ผ่านมา +1

    Ungepeana majibu kabla kusonga mbele na maswali mengine

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  5 วันที่ผ่านมา

      Kuna watu waliomba maswali ya kudurusu, sikujua kama kuna watu watahitaji MAJIBU yake. Lakini majibu yake yapo kwa comments section na mengine naendelea kuyaweka hapa

    • @PetersonJohn-o2k
      @PetersonJohn-o2k 5 วันที่ผ่านมา +1

      @@MwalimuWanjala otherwise good job Mwalimu

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  5 วันที่ผ่านมา

      @@PetersonJohn-o2k asante Sana🤗🫡

  • @MwalimuWanjala
    @MwalimuWanjala  11 วันที่ผ่านมา

    Jibu la swali la Kwanza .
    1. a)( i)Msemaji - Dina
    (ii) Msemewa -Kiwa
    (iii) Mahali-Nyumbani kwa Dina
    (iv) Anarejelea busara na bidii za Neema
    b) (i) Chuku- Yule tangu akiwa kiduchu amekuwa na kiimo cha sindano ya nguo.
    (ii) Tashbihi- mwenye akili za ncha ya sindano
    (iii) Taswira - akikutazama unahisi anazisoma fikra zako
    (iv) Yule tangu akiwa kiduchu

  • @danielkarisa2260
    @danielkarisa2260 13 วันที่ผ่านมา +1

    Naomba ukipea swali tupe na majibu tafadhali! Ninahakika kabisa maswali haya Kuna badhi yatakuja kwa mtihani! Tusaidia tafadhali

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  13 วันที่ผ่านมา +1

      Haya maswali yote Yana majibu kwa video zingine. Au kama kuna swali lakulemea, niambie kwa WhatsApp 0707286397 nikupee majibu. Shukran sufufu kwa kutazama

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  11 วันที่ผ่านมา

      Nimeweka majibu kwa comments kaka

  • @MwalimuWanjala
    @MwalimuWanjala  11 วันที่ผ่านมา

    2. a) (i) Msemaji -Dina
    ii) Msemewa -Kiwa
    iii) mahali- Nyumbani kwa Dina
    iv) Kiwa amefanya mazoea ya Kula chakula kidogo. Anasema kutokana na mabadiliko ni wakati wa kujifunga masomo.
    b) i)Taswira oni- tazama ulivyokonda
    C) -Swali balagha- hiyo nafasi ya ng'onda unaitaka kwa nini?
    -Istiara - unaelekea kushindana na ng'onda
    -Chuku- Tazama ulivyokonda. Unaelekea kushindana na ng'onda.

  • @BalibinaOkoth
    @BalibinaOkoth หลายเดือนก่อน +2

    Swali langu ni Fafanua namna suala la urafiki linavyoshughulikiwa katika tamthilia ya bembea

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  หลายเดือนก่อน

      Nitakujibu.

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  หลายเดือนก่อน

      1. Sara anamwita Dina kwake kuja kumsaidia katika mapishi anapokuwa mgonjwa. Dina anaenda kumsaidia kwa sababu ya urafiki wao.

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  หลายเดือนก่อน

      2. Wakati Dina ako kwa Sara, mazungumzo yananoga na kuingia kwa vicheko hadi wanasahau kuwa maji yameshachemka.
      3. Bella na Neema ni rafiki wa dhati. Urafiki huu unamfanya wanasikizana na Bella anakaa kwa Neema kwa muda mrefu hadi Watoto wake wanamsahau.
      4. Beni, Yona na Luka ni marafiki. Kila siku wanakutana katika kikao cha wazee wakijadiliana mambo ya jamii, mavuno na kuburudika kwa ujumla.

  • @Euginemitoko-y6n
    @Euginemitoko-y6n 26 วันที่ผ่านมา +1

    majibu ya maswali hyo

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  26 วันที่ผ่านมา

      Kama kuna swali gumu hujui jibu taja nikutatulie

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  26 วันที่ผ่านมา

      Kama kuna swali gumu hujui jibu taja nikutatulie

  • @saeedmualim9592
    @saeedmualim9592 2 หลายเดือนก่อน +1

    Utusaidie majibu pia itatusaidia zaidi.

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  2 หลายเดือนก่อน

      Asante, bila Shaka nitafanya hivyo

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  11 วันที่ผ่านมา

      MAJIBU yapo kwa comments

  • @PatrickOdokeOdoke
    @PatrickOdokeOdoke หลายเดือนก่อน +2

    Nisaidie hili swali eleza namna watoto waliodharauliwa walikuwa nyota ya jaha

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  หลายเดือนก่อน

      Jamii ilidharau familia ya Yona na Sara kwa sababu ya kupata Watoto wa kike pekee. Tunaona hawa Watoto wa kike wanakuja kuwa nyota ya jaha kwa njia zifuatazo:
      1. Neema anasoma na kufika chuo kikuu Jambo ambalo si la kawaida kulingana na utamaduni, mtoto wa kike kusoma hadi chuo kikuu ni nadra.
      2. Neema anahitimu na kupata ajira. Hiyo ajira inamsaidia kuinua Wazazi wake kimaisha. Kuna wakati anatumia Yona pesa za kununua dawa.
      2. Neema anamsaidia Sara katika matibabu. Anampeleka hospitali ya mjini na kusimamia gharama zote
      3. Neema anawajengea Wazazi wake nyumba mpya.
      4. Neema anakuwa msichana wa kwanza kuliendesha gari kijijini mwao.
      5. Mabinti wa Sara na Yona wanajiendeleza kielimu na kufanya wanajamii kuiheshimu familia ya Yona. Awali waliwadharau na kuwasimanga.

  • @edwinikavulu9143
    @edwinikavulu9143 หลายเดือนก่อน +1

    Dondoo la msimulizi linawekwa aje kwa mktadha wake

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  หลายเดือนก่อน

      Utajibu hivi 👇
      Mnenaji/msemaji- msimulizi
      Mnenewa/msemewa-
      Mahali/ mandhari-
      Kiini/sababu/tukio-

  • @AishaMawondo
    @AishaMawondo 2 หลายเดือนก่อน +3

    Mm sijakulewa mwalimu hijanionyesha vile mtu Hana jibu maswali ya bembea

    • @MwalimuWanjala
      @MwalimuWanjala  2 หลายเดือนก่อน

      Hayo ni maswali, kisha ukiangalia video zingine kwa channel hii utapaya MAJIBU yake

  • @ReheriChacha
    @ReheriChacha วันที่ผ่านมา

    Swali la kumi jibu msemaji n bunju n msemewa n neema ni nyumbani kwao bunju na neema ❤❤

  • @ReheriChacha
    @ReheriChacha วันที่ผ่านมา

    Swali la kumi jibu msemaji n bunju n msemewa n neema ni nyumbani kwao bunju na neema ❤❤