Naibu Gachagua awakemea wanaodai kuwa karibu na Rais Ruto

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 25 ก.ย. 2024
  • Naibu rais Rigathi Gachagua amekemea viongozi serikalini ambao anasema kuwa wanatumia uhusiano wao na Rais William Ruto kumdunisha. Gachagua ameshikilia kuwa anajua majukumu yake serikalini na kuwa hatakubali wabunge pamoja na mawaziri kumkemea na kumuita mkabila. Gachagua amekiri kuwa wanaompiga vita ni wale waliopinga kuteuliwa kwake kama naibu rais akisema kuwa bado hawajakubali kuwa ni yeye anayeshikilia wadhfa huo kwa sasa. Gachagua ameshikilia kuwa atazidi kupigania umoja wa mlima Kenya.

ความคิดเห็น •