CHADEMA WALALAMIKIA MAWAKALA WAO KUZUIWA VITUONI' MSIMAMIZI ASEMA...

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 29 พ.ย. 2024
  • Arusha. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelalamikia mawakala wao kuzuiwa kuingia katika vituo vingi na kudai kuwa waliopewa nakala za viapo wamekataliwa.
    Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 27,2024, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amedai kuwa mawakala wao waliopewa nakala za viapo wameambiwa hazitambuliki kwa kuwa hazina muhuri.
    Akijibu malalamiko hayo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini, John Kayombo amesema hajapokea malalamiko yoyote kuhusu mawakala katika vituo vyote 462 katika jimbo hilo.
    Amesema changamoto hizo zinatengenezwa na Chadema na kudai kuwa chama hicho kilipeleka mawakala wawili hadi watatu katika kituo kimoja, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za uchaguzi.
    Kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi kukosa majina yao kwenye vituo vya kupigia kura, Msimamizi huyo huyo amedai kuwa majina ya wapiga kura zaidi ya 389,000 waliojiandikisha yapo kwenye vituo na kuwa ambaye haoni jina lake, atakuwa amejiandikisha nje ya Arusha.
    (Imeandaliwa na Janeth Mushi)

ความคิดเห็น • 4

  • @ZakayoDionisi
    @ZakayoDionisi 3 วันที่ผ่านมา

    Hakuna hiyo ni uwizi

  • @denisipaulo7785
    @denisipaulo7785 2 วันที่ผ่านมา

    Akae nyumbani watu wenyewe ccm

  • @JumbeOjaso
    @JumbeOjaso 3 วันที่ผ่านมา

    Mgombea arudi nyumbani ili mumibie kura??

  • @RichardNtamakulilo
    @RichardNtamakulilo 3 วันที่ผ่านมา

    Tzvs USA