Posta Yatakiwa Kuhakikisha Mifumo Yake ya Utendaji Inasomana

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 10 ต.ค. 2024
  • Posta Yatakiwa Kuhakikisha Mifumo Yake ya Utendaji Inasomana
    Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb), amelitaka Shirika la Posta Tanzania kuhakikisha mifumo yake ya kutolea huduma inasoma ili kuongeza ufanisi na ubunifu katika utendaji, na hivyo kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wananchi.
    Mhe. Silaa aliyasema hayo leo, tarehe 07 Oktoba 2024, wakati wa ziara yake ya kufahamu utendaji wa Shirika la Posta katika Makao Makuu yake jijini Dar es Salaam.
    Aidha, Mhe. Silaa ameitaka Posta kuboresha huduma zake kidijitali ili kuendana na mkakati wa Serikali wa Tanzania ya Kidijitali, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anasisitiza umuhimu wa kuwa na Tanzania ya kidijitali.
    Waziri Silaa pia alisisitiza umuhimu wa Shirika la Posta kuchangamkia fursa mpya za usafirishaji wa bidhaa, mazao, na vitu vya thamani, huku akiahidi kuendelea kushirikiana na Shirika la Posta katika kuendeleza mabadiliko ya kidijitali.
    Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania, Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi, ameahidi kuwa uongozi wa Bodi uko tayari kusimamia mageuzi ya uendeshaji ndani ya Shirika ili kukidhi matarajio ya wateja na wadau wa Posta.
    Kwa upande wake, Postamasta Mkuu, Bw. Macrice Mbodo, ameelezea mpango mkakati wenye vipaumbele vya Shirika vinavyolenga kufanya mageuzi ya kidijitali ili kukidhi mahitaji ya wateja, hasa katika kipindi hiki cha maendeleo makubwa ya teknolojia.

ความคิดเห็น •