Mindsetting Initiative
Mindsetting Initiative
  • 741
  • 105 801
Fursa ya Kushiriki Program ya Mentorship - TALENT MINDSET
Nafurahi kutangaza fursa kwa Mtanzania 🇹🇿 kushiriki katika programu ya mentorship, TALENT MINDSET, ambayo inaanza rasmi Januari 2025! 🚀
Kama Mtanzania, unayo nafasi ya kushiriki kama mtaalamu/muelimishaji au kama mwanafunzi! 🌟
💡 TALENT MINDSET ni programu iliyoundwa kusaidia vijana wa kimataifa kupata mtazamo chanya na kutumia vipaji vyao kwa njia bora na yenye mafanikio.
👉 Ikiwa ungependa kuwa muelimishaji, tafadhali nitumie barua pepe kupitia anuani: ezekiel_kuhoga@outlook.com 📩
👉 Kama unataka kushiriki kama mwanafunzi, hakikisha unafuatilia matangazo yetu kupitia kurasa za Talent Mindset kwenye Facebook na Instagram. 🖥️📱
Jiunge nasi! Pamoja tunaweza kukuza vipaji vyetu! 💪✨
#TalentMindset #MentorshipProgram #KukuzaVipaji #Mtanzania #FursaZaVijana #PositiveMindset #Inspiration #January2025
มุมมอง: 88

วีดีโอ

Adui🚫 Wa Pili wa Maendeleo ya Mtanzania🇹🇿 Huyu Hapa
มุมมอง 91วันที่ผ่านมา
🔥 ADUI WA PILI WA MAENDELEO YA MTANZANIA NI UJINGA 🚫 Katika video hii, tunachambua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya Mtanzania na kwa nini ujinga ni adui mkubwa wa pili. Tunazungumzia masuala ya mahusiano ya kijamii 🤝 na kibiashara 💼, thamani ya elimu 📚 dhidi ya fedha 💰, na tabia zinazozuia maendeleo baada ya kupata fursa. ❓ Elimu au fedha - kipi bora zaidi? Tunatathmini mtazamo wa watu ku...
Adui wa Kwanza wa Maendeleo ya Mtanzania🇹🇿 Huyu Hapa!
มุมมอง 3.8K28 วันที่ผ่านมา
Adui wa Kwanza wa Maendeleo ya Mtanzania: Mafundisho Mabovu" Katika video hii, nimejadili kiini cha changamoto za maendeleo ya Mtanzania na kuangazia kwamba adui mkubwa sio serikali, elimu, au hata mkoloni mamboleo. Adui halisi ni mafundisho maovu ambayo yamekubalika katika jamii na kutumika kama msingi wa malezi ya watoto na vijana wetu. 🎯 Yaliyomo kwenye Video: 1️⃣ Kutowajali watu usiowafaham...
Masterclass | Namna Nzuri ya Uwekaji wa Malengo na Kufanya Tathmini Sahihi | Ezekiel Kuhoga
มุมมอง 201หลายเดือนก่อน
Jinsi ya Kufanikisha Malengo Yako kwa Ufanisi | Tathmini na Uwekaji wa Malengo 🎯✨ Katika video hii, tunajadili kwa kina jinsi ya kutafsiri malengo, nafasi, ndoto, na taarifa ili kufanikisha ndoto zako kubwa. 🏆🚀 Utaelewa kwa nini msingi wa malengo yako ni imani, kwa nini huwezi kufanikiwa zaidi ya kiwango cha malengo yako, na umuhimu wa kujizunguka na watu sahihi. 🔑 Sehemu Muhimu za Video: 1️⃣ T...
Kanuni ya Investment Annuity: Jinsi UTT AMIS Inavyosaidia Kuwekeza kwa Malengo
มุมมอง 671หลายเดือนก่อน
Katika video hii, tunachambua kwa kina kanuni ya investment annuity na jinsi inavyotumika na UTT AMIS kusaidia wawekezaji kufanikisha malengo yao ya kifedha. Utajifunza: Kanuni ya msingi inayotumika katika mahesabu ya uwekezaji. Jinsi ya kuainisha kiasi cha kila mwezi ili kufanikisha lengo fulani la muda mrefu. #UTTAMIS #InvestmentAnnuity #UwekezajiKwaMalengo #Fedha #MaarifaYaKifedha
Namna 5 za Kujua Mfuko Upi wa UTT-Amis ni Bora Zaidi | Ezekiel Kuhoga
มุมมอง 1.5Kหลายเดือนก่อน
Video Title: Jinsi ya Kuchagua Mfuko Bora Chini ya UTT AMIS Description: Unatafuta kuwekeza kupitia UTT AMIS lakini hujui ni mfuko gani bora kwako? Katika video hii, tunakupa njia 5 muhimu za kukusaidia kufanya maamuzi sahihi: 1️⃣ Sera ya Mfuko: Fahamu sera na mwelekeo wa kila mfuko. 2️⃣ Sifa za Mfuko: Angalia sifa mbali mbali za mfuko kama zinakidhi mahitaji yako. 3️⃣ Malengo ya Mfuko: Lingani...
Majibu yangu kwa comment ya, "Acheni Kuchanganya Kiswahili na Kiingereza".
มุมมอง 81หลายเดือนก่อน
Comments kadhaa zimekuja kutoka kwa wadau ambao wamependekeza tujitahidi kutumia Kiswahili bila kuchanganya. 🌍🗣️ Kwa heshima kubwa, nimepokea maoni hayo kwa uzito na leo nimeandaa majibu kwenye video maalum kwa ajili yenu. 🎥✅ Karibuni tena kwa maoni na maswali zaidi! Tunathamini sana mchango wenu. ❤️💬 #Kiswahili #MaoniYenu #Mawasiliano #TunaendeleaPamoja
Namna 5 Utanufaika na Tabia ya Usomaji wa Vitabu
มุมมอง 902 หลายเดือนก่อน
Namna 5 Utanufaika na Tabia ya Usomaji wa Vitabu
An Important Tip for Job Seekers
มุมมอง 482 หลายเดือนก่อน
An Important Tip for Job Seekers
How Do You Succeed in Any Area of Your Life?
มุมมอง 722 หลายเดือนก่อน
How Do You Succeed in Any Area of Your Life?
Uchambuzi wa Kampuni ya Nicol | Ammi Julian | Fortius Rutabingwa
มุมมอง 8642 หลายเดือนก่อน
Uchambuzi wa Kampuni ya Nicol | Ammi Julian | Fortius Rutabingwa
Hapa Ndipo Tulipofika | Mindsetting Initiative
มุมมอง 2093 หลายเดือนก่อน
Hapa Ndipo Tulipofika | Mindsetting Initiative
Faida na Hasara Kati ya Kuwekeza Moja kwa Moja ama Kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja
มุมมอง 9493 หลายเดือนก่อน
Faida na Hasara Kati ya Kuwekeza Moja kwa Moja ama Kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja
Mafanikio Halisi Huja kwa Kutoa Sio Kuchukua
มุมมอง 1443 หลายเดือนก่อน
Mafanikio Halisi Huja kwa Kutoa Sio Kuchukua
Je, Zipi ni #risks za kuwekeza Inuka Money Market Fund??
มุมมอง 2874 หลายเดือนก่อน
Je, Zipi ni #risks za kuwekeza Inuka Money Market Fund??
Masterclass 2 | Sera ya Uwekezaji | Inuka Money Market Fund
มุมมอง 1924 หลายเดือนก่อน
Masterclass 2 | Sera ya Uwekezaji | Inuka Money Market Fund
Masterclass 1 | Kwanini Kuwekeza Kupitia Mifuko ya Pamoja ni Muhimu | Inuka Money Market Fund
มุมมอง 1874 หลายเดือนก่อน
Masterclass 1 | Kwanini Kuwekeza Kupitia Mifuko ya Pamoja ni Muhimu | Inuka Money Market Fund
Mchache kuhusu tukio la Uzinduzi | Inuka Money Market Fund | Orbit Securities
มุมมอง 1904 หลายเดือนก่อน
Mchache kuhusu tukio la Uzinduzi | Inuka Money Market Fund | Orbit Securities
CRDB Investor Briefing | Quarter 2, 2024 | Fredrick Nshekanabo | Anna Mwasha | Orbit Securities
มุมมอง 3314 หลายเดือนก่อน
CRDB Investor Briefing | Quarter 2, 2024 | Fredrick Nshekanabo | Anna Mwasha | Orbit Securities
Kitabu Teule | Atomic Habits | MI Reading Club July 2024
มุมมอง 1325 หลายเดือนก่อน
Kitabu Teule | Atomic Habits | MI Reading Club July 2024
Taarifa na Maelekezo | MI Reading Club | July 2024
มุมมอง 476 หลายเดือนก่อน
Taarifa na Maelekezo | MI Reading Club | July 2024
My Life Story as a Foreigner in Finland | Ezekiel Kuhoga | Mindsetting Initiative
มุมมอง 2136 หลายเดือนก่อน
My Life Story as a Foreigner in Finland | Ezekiel Kuhoga | Mindsetting Initiative
UPDATE | Zoezi la kutafuta mawasiliano limeanza | UTT Amis
มุมมอง 1876 หลายเดือนก่อน
UPDATE | Zoezi la kutafuta mawasiliano limeanza | UTT Amis
Episode 5 | Ijue UTT Amis | Huduma za Usimamiaji wa Uwekezaji na Kukuza Thamani
มุมมอง 6616 หลายเดือนก่อน
Episode 5 | Ijue UTT Amis | Huduma za Usimamiaji wa Uwekezaji na Kukuza Thamani
About To Start Producing Podcasts with The City of Kuopio for The Internationals | Ezekiel Kuhoga
มุมมอง 296 หลายเดือนก่อน
About To Start Producing Podcasts with The City of Kuopio for The Internationals | Ezekiel Kuhoga
Episode 4 | Mfuko wa Ukwasi | Mfuko wa Hatifungani | Ijue UTT Amis
มุมมอง 4.2K6 หลายเดือนก่อน
Episode 4 | Mfuko wa Ukwasi | Mfuko wa Hatifungani | Ijue UTT Amis
Episode 2 | Uchambuzi wa NMB Bank | Soko la Mitaji | Uwekezaji wa Hisa | Bernard Majollo
มุมมอง 6577 หลายเดือนก่อน
Episode 2 | Uchambuzi wa NMB Bank | Soko la Mitaji | Uwekezaji wa Hisa | Bernard Majollo
Jinsi ya kunufaika Kifedha Kupitia YouTube (Kwa mtanzania 2024)
มุมมอง 1877 หลายเดือนก่อน
Jinsi ya kunufaika Kifedha Kupitia TH-cam (Kwa mtanzania 2024)
Episode 3 | Ijue UTT Amis (Mifuko ya uwekezaji)
มุมมอง 4127 หลายเดือนก่อน
Episode 3 | Ijue UTT Amis (Mifuko ya uwekezaji)
Maswali 7 ya Kumuuliza Dalali wako wa Hisa (Stock Broker)
มุมมอง 6597 หลายเดือนก่อน
Maswali 7 ya Kumuuliza Dalali wako wa Hisa (Stock Broker)

ความคิดเห็น

  • @rehemawalters8226
    @rehemawalters8226 2 วันที่ผ่านมา

    Jaman yani elimu yote hii mnatoa Bure .....nawapenda sana

  • @djramsoyusuph9661
    @djramsoyusuph9661 3 วันที่ผ่านมา

    Mimi ni fundi mzuri wa gari pia nidereva mzuri naitaji nafasi

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 2 วันที่ผ่านมา

      Unahitaji nafasi ya kushiriki kama mwanafunzi au mwalimu?

  • @g21955
    @g21955 3 วันที่ผ่านมา

    Keep it Up !!!!!!🙏🌍🌐🌞

  • @djramsoyusuph9661
    @djramsoyusuph9661 5 วันที่ผ่านมา

    Niunge group la WhatsApp

  • @bernadinbenard4596
    @bernadinbenard4596 6 วันที่ผ่านมา

    Asante kwa elimu kubwa kama hii akika nami nitaekeza

  • @JohnJelemia-x3v
    @JohnJelemia-x3v 9 วันที่ผ่านมา

    Kaka Mimi Najua Kushona Suti Kaunda Suti yani men's suit Niko Botswana Nahitaji Kujiunga

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 7 วันที่ผ่านมา

      Sawa sawa. Basi endelea kufuatilia kwenye kurasa zangu za Facebook ama LinkedIn. Nimeweka pale link ya Microsoft Team na unaweza kushiriki.

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 9 วันที่ผ่านมา

    Nitashiriki Kama Mwanafunzi

  • @mohammedrajab595
    @mohammedrajab595 12 วันที่ผ่านมา

    Je unapataje vitabu na je vipi vya ebook?

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 12 วันที่ผ่านมา

      Ili upate kitabu inabidi uwasiliane na Mwl. Busara. Kwa sasa vitabu vyote ni hardcopies.

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 12 วันที่ผ่านมา

    🎉🎉🎉

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 12 วันที่ผ่านมา

    Ahsante sana Kwa Somo la leo

  • @petrokapufi2666
    @petrokapufi2666 14 วันที่ผ่านมา

    Nivigezo gan vya kujiunga na hizo hisa

  • @kyaro5945
    @kyaro5945 15 วันที่ผ่านมา

    Shida ya tz ni rushwa. Nikiwa speaker wa Binge mie sitaki fareness au huruma ya kisheria eyi nisishtakiwe. Nitaharakisha sheria za rushwa ziletwe bungeni na kuzipitisha ziwe harsh laws. Eg. Sheria ya kunyonga kizazi chako chote utakapo bainika umehusika na rushwa au zile dalili tuu. Nitafanya hijimu za madawa ya kulevya ziwe za kunyonga.

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 15 วันที่ผ่านมา

      Je, kabla ya kuwa speaker wa bunge, umeshawahi kukemea wizi unaofanyika karibu yako? Mmoja akiiba daftari la mwenzie, ama mmoja kutokulipa nauli? Kama haujawahi kukemea vitabia hivi basi jua hautakuwa na tofauti nao unaosema unawachukia sasa.

  • @anastazianyambita5534
    @anastazianyambita5534 18 วันที่ผ่านมา

    Mimi naona hawa jamaa wajanjawajanja sana.....! Wana poor customer care....!

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 15 วันที่ผ่านมา

      Kwa nini unasema hivyo?

    • @ndossiadventurestz.6796
      @ndossiadventurestz.6796 10 วันที่ผ่านมา

      Mwenyewe nilizani ivyo ila ukifika ofisini kwao ndo utajua wako busy sana inabidi waongeze matawi ili waweze kumudu idadi ya wateja.

    • @anastazianyambita5534
      @anastazianyambita5534 9 วันที่ผ่านมา

      @@mindsettinginitiative Yaani ukiwapigia simu hawapokei...! Ku - update bank details ni issue....! Kwa hiyo ukikaa mikoani inakuwa changamoto kubwa....! Sasa huu si ubabaishaji.....? Yaani badala ya mteja kutengenezewa mazingira ya kutatua challenges zake MWENYEWE lakini mteja anatengenezewa mazingira ya kupoteza pesa zaidi ( Nauli ya kwenda kwenye ofizi zao). Sasa kwa Mfamo Mimi natoka Ruvuma sasa nauli ya kwenda Dar analipia nani?? Ndio maana nasem hiyo poor customer care

  • @paulkambonya8001
    @paulkambonya8001 19 วันที่ผ่านมา

    Kweli kaka thanks kwa ujumbe chanya

  • @ijampanzi6100
    @ijampanzi6100 24 วันที่ผ่านมา

    Ni rahisi kusema Adui ya Mtanzania ni Mtanzania wenyewe au Muafrika ni Muafrika mwenyewe, Tatizo huenda Haujaelewa Mfumo wa Utawala Unatengenezwa Vipi. Jifunze kwanza Mifumo inasukwa vipi. Badae jipe homework wewe mwenyewe wa kutengeneza Mfumo wa kutokana na Umasikini wewe na familia yako, ukiliweza utakua na haki ya kuongea na kutoa USHAHURI NA Elimu. Je unategemea Wafrika Marekani kukaa Mia 400 bila kujitoa kwenye Utumwa (kuonewa) na jambo wanajutakia wenyewe? Tatizo kubwa kwa Muafrika popote ni Kukosa Viongozi wenyewe MAONO ( LEADERSHIP WITH VISION= ÉLITES)

  • @tugemwakilewa1298
    @tugemwakilewa1298 24 วันที่ผ่านมา

    Nimekukubali asilimia mia, ndio maana wasukuma ni viongozi bora sana. Mimi sio msukuma ila hii jamii ni moja ya jamii yenye malezi bora sana, jamii nyingine ni wamasai.

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 24 วันที่ผ่านมา

      Sijaishi na wasukuma kwa sehemu kubwa. Ila ninachoona hili ni jambo lina athiri wa Tanzania kiujumla. Wako baadhi ya watu ambao bado wana maadili na kujali wengine ila ni wachache sana.

  • @katemachanda7035
    @katemachanda7035 25 วันที่ผ่านมา

    Huwezi acha kuzungumzia mfumo wa utawala ambao ndio Serikali, wala huwezi acha kutupa lawama kwa ukoloni mambo leo ambao ndio mfumo wa juu zaidi ya utawala unatawala Serikali za nchi moja moja. Anayeweka mfumo wa Elimu sio raia, ni Serikali ambayo hupata miongozo karibu ktk kila nyanja ya kimaendeleo kupitia Mashirika ya Kimataifa. Advantege kubwa anayoweza kupata Mwafrika wa kawaida ktk kujiendeleza pale anapoamua kufuata misingi ya Dini/imani ambazo zinafunua mbinu zilizo juu ya hila za watu walioshika utawala wa Serikali zetu na hao wa taasisi za Kimataifa. Vinginevyo kwa ushahidi ulio wazi pale unapotaka kwenda kinyume dhidi Serikali na taasisi hizi ili ulete maendeleo ya kweli ni kuhatarisha maisha yako kwa asilimia 100. Tazama yaliowakuta akina Gadafi, Magufuli n.k ambao nyio mnaoishi na wazungu uelewa wenu kwamba hawa ni Madikteta sana hapa Afrika, lkn kiuhalisia ndio wakombozi wakweli wa Waafrika kupitia nchi zao. UMELETA MADA NGUMU SANA. BADO KUNA MENGI SANA YA KUSEMA, WACHA TUISHIE HAPA.

  • @jumafaki7473
    @jumafaki7473 25 วันที่ผ่านมา

    wewe umechukua na tabia ya kiislam , Mimi mtoto wangu , miaka 5 mwema kwa wenzake , ukiwa na pesa , atawagawia wenzake ,ulimpa pesa atakuomba wenzake , uwape , nawao chakula atawapa ,Mimi napenda ,tabia ya kujali wengine ,

    • @toivokaya1890
      @toivokaya1890 24 วันที่ผ่านมา

      Huo ndiyo ukweliiiii

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 24 วันที่ผ่านมา

      Karibu kila mtoto mwanzoni huwa na tabia ya kujali wengine (baada ya kuanza kujielewa). Wako watoto ambao huwa na tabia mbaya toka mapema ila ni wachache sana. Ila jamii ndio hufanya juhudi ya kuwafundisha watoto/vijana tabia za kutowajali wengine.

    • @FelisterMichael-r8t
      @FelisterMichael-r8t 24 วันที่ผ่านมา

      Hata Mimi hujitaidi kuwa msaada kwa wengine ila sasa jamii itakavyokusema dah hatari!

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 22 วันที่ผ่านมา

      Safi sana. Keep it up.

  • @kilimanjarotv255
    @kilimanjarotv255 25 วันที่ผ่านมา

    kaka umeelezea sana vizur sana lakini kwa maoni yangu kutoka rohoni kiukweli viongozi wetu sio wazalendo kabisa bado wazungu wametubana kutokana na ukombozi wa fikra bado tunaamin maendeleo yanatoka kwa mzungu na serekali ndio uongozi wakutuvusha lakini haijali kesho yetu wangekua wanajali tungekua mbali sana hii tanzania ni tajiri na africa ni tajiri sana watu wengi hawafatili vitu vya maana chukulia mfano kwenye trending za mitandaoni vitu gani vina trend visivyo na maana vya maana hatufuaatlii kabisa tunabaki kulalalamika hivi unajua tz ikiamua na africa iikaamua kujisimamia kwa haki na thabiti rasilimali zetu vizur hakuna bara lingefikia kwa utajiri africa dunia nzima fuatilia takwimu za kila nchi ya africa inazo mali za kutosha na wazungu hapo walipofika sisi tukiamua africa nzima kuungana pesa 1 raisi mmoja katiba 1 tupate raisi na watendakazi wazuri ndani ya miaaka 10 tu hata china na marekani haitatufikia hata robo

  • @brightonephraim9158
    @brightonephraim9158 26 วันที่ผ่านมา

    Big up Sana mkuu

  • @kazimotofashe2938
    @kazimotofashe2938 26 วันที่ผ่านมา

    Na malanyingi watu huingia kwenye system ya uongozi wakiwa vizuri lakini wanapoingia tu hulazimishwa kuwa vibaka na watu wanao wakuta huko, ukiingia kwenye system kama wewe haubi viongozi wako, watumishi wenza hata hao unao watumikia watakuona adui Yao na wanakutengezea vikwakozo vingi matokeo yake inakulazimu ufanane nao ili uishi vizuri nao na uilinde kazi yao

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 25 วันที่ผ่านมา

      Uko sahihi sana. Watu wengi kabla ya kushika dhamana huwa warahisi kuonesha ni namna gani wao wangewajibika lakini wakipewa kiti huwa ngumu kwa sababu mfumo wa maisha yao yote haujawa mfumo wa kusapoti uwajibikaji.

  • @ME-kb8rk
    @ME-kb8rk 26 วันที่ผ่านมา

    100%

  • @MuhammedAliOmar-c9u
    @MuhammedAliOmar-c9u 26 วันที่ผ่านมา

    Kweli kabisa.... Na adui wa maendeleo ya Mzanzibari ni Tanganyika.

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 26 วันที่ผ่านมา

      😅😅..Hili sasa ni jambo jingine linahitaji mjadala wake tofauti.

    • @eddyvillejracamosie5562
      @eddyvillejracamosie5562 25 วันที่ผ่านมา

      Hapana adui wa maendeleo ya Mtanganyika ni Wazanzibari, mmepewa upendeleo katika kila sekta lakini bado mnalalamika.

    • @MuhammedAliOmar-c9u
      @MuhammedAliOmar-c9u 25 วันที่ผ่านมา

      @@eddyvillejracamosie5562 sekta ipi tuliyopewa upendeleo? Weak hoja

    • @eddyvillejracamosie5562
      @eddyvillejracamosie5562 25 วันที่ผ่านมา

      @@MuhammedAliOmar-c9u Kwa mfano linapokuja suala la umiliki wa ardhi, hakuna Mtanganyika anayeruhusiwa kumiliki ardhi Zanzibar wakati wazanzibar mmejazana huku bara na mnamiliki ardhi pia. What you brings on the table is minimal comparing to what Tanganyika brings, and still you’re here complaining, so maybe tuambie ni kivipi Tanganyika ni adui wa maendeleo ya mzanzibari?

    • @mangulimanguli3974
      @mangulimanguli3974 25 วันที่ผ่านมา

      Akili una kwani kuna mtanganyika anae waongoza c mnajiongoza wenyewe

  • @jumamahunja2242
    @jumamahunja2242 26 วันที่ผ่านมา

    Naomba utoe namba ya simu

  • @bajagihaji8923
    @bajagihaji8923 26 วันที่ผ่านมา

    Brother umesema uhalisia wa maisha yetu rehema kwa jamii yetu ni ngumu maono yako ndiyo tatizo la maendeleo ❤

  • @othumntz6953
    @othumntz6953 26 วันที่ผ่านมา

    Bro umeongea ukweli kabisa

  • @bagumampenda
    @bagumampenda 26 วันที่ผ่านมา

    I have no respect for anybody who does not live in their country.

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 26 วันที่ผ่านมา

      I could have wished then you would love everyone in the country. But what you demonstrate here is the attitude of hating those you deem more successful than you are. Its another sick mentality challenging Africans.

    • @bagumampenda
      @bagumampenda 26 วันที่ผ่านมา

      @@mindsettinginitiative Brother, what does no respect have to do with hate? Sijasema nachukia, nimesema sina heshima. Unaishi nje alafu unakaa kukosoa vitu usivyovielewa vizuri. Tanzanians are hardworking, diligent and very intelligent people, you wouldn't know that because you do not live among them. So because you live abroad you automatically feel nakuonea wivu because to you, living abroad means success. Huo ndiyo ulimbukeni, free your mind kaka.

    • @katemachanda7035
      @katemachanda7035 25 วันที่ผ่านมา

      ​@@bagumampendaAmemanifest kitu alichokushutumu na kuwashutumu Watanzania😂😅 Kumbe wote ndio tuko hivyo😂😅😅

    • @alihussein4303
      @alihussein4303 24 วันที่ผ่านมา

      Big up yourself Bro, Uhakika ✊🏿

  • @robert.joseph
    @robert.joseph 26 วันที่ผ่านมา

    Campuni iki buy back shares to miniority shared holder ambao ndo sisi Je tunataarifiwa tuu na je kama mtu hutaki kuuza inakuaje ? Na je wanakulipa bei ya soko tuu ? Na je hawakulipi fidia ?

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 26 วันที่ผ่านมา

      Swali zuri sana hili na naona linahitaji jibu kutoka kwa wataalamu wenyewe. Ninaliwasilisha na nitarejea ama tutalijadili kwenye kipindi kijacho.

  • @aliakrabi8321
    @aliakrabi8321 26 วันที่ผ่านมา

    Watanzania wachache sana hata wasomi wanaipenda kazi anayopewa, ana initiative kuisukuma kazi iishe vizuri na kuiboresha kazi yake. innovative-finding ways kuiboresha kazi. wasiokuwa na excuses, wanaojali na kuogopa matokeo mabaya ya baadae. asiyekuwa na story nyingi wakati wa kazi, asiyekuwa na ufedhuli na majungu

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 26 วันที่ผ่านมา

      Ni kweli kabisa. Wako ila ni wachache sana.

    • @aliakrabi8321
      @aliakrabi8321 25 วันที่ผ่านมา

      Tunakwama kwenye malezi na maadili chuoni, utamaduni wetu wa kufichiana siri, kuoneana aibu, kutoambina ukweli kwa marafiki kama itakuwa mchungu au unamsema rafiki yako na kustahiana kusikofaa.

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 25 วันที่ผ่านมา

      @aliakrabi8321 Uko sahihi sana. Kwa sehemu kubwa tatizo linaanzia kwenye ukosefu wa malezi bora na maadili.

  • @andrews_kodeson
    @andrews_kodeson 27 วันที่ผ่านมา

    Hii ni uwongo mkubwa kusema kwamba maendeleo hayawezi kutenganishwa na siasa na serikali. Mifano wazi ya hili ni mataifa ya Marekani na Mexico, Korea Kusini na Kaskazini, na Msumbiji na Afrika Kusini. Nchi hizi zinaonyesha kwa njia isiyo na shaka jinsi vile sera za serikali, miundombinu, na usaidizi wa kisiasa vina mchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Msaada kutoka kwa serikali katika nyanja kama elimu, afya, usalama, na miundombinu huunda mazingira ya kukuza ukuaji endelevu na unaojumuisha. Maendeleo hayafanyiki kwa kujitegemea, bila ushiriki wa moja kwa moja wa serikali. Inafaa kufikiria kuhusu hili, hasa tunapona watu wengi, ikiwa ni pamoja na wewe, ambao waliondoka nchi yao kuenda kuishi Ulaya, ambapo kwa sehemu kubwa, ni hizi sera za serikali na miundombinu bora ambazo zinahakikisha kiwango cha juu cha maisha na maendeleo. Maendeleo yangekuwaje bila mikakati ya kisera na serikali inayojitolea kwa ustawi wa wote?

  • @johnmremi
    @johnmremi 29 วันที่ผ่านมา

    Thanks brother keeps it UP

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 29 วันที่ผ่านมา

    Ahsante kwenye ulev mtu akinywa pombe nyingi unajikuta anajissifu na jamii ina msifu Kadhalika Hata Wanaume Malaya akiwa na wanawake wengi anaoshiriki nao ngono jamii fulani ina msifu kama ni mwamba kumbe ndio ina mpotosha

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 29 วันที่ผ่านมา

      Kabisa. Hii ndio inasaidia kuzuia maendeleo ya Mtanzania.

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 29 วันที่ผ่านมา

    Heko Sana Kama vile Nasemwa mimi

  • @GilliardMmary
    @GilliardMmary หลายเดือนก่อน

    Mh Ezekiel Kuhoga shukrani sana kwa somo la leo nimekuelewa vizuri sana, BLESSED

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      Ahsante sana kwa mrejesho kiongozi🙏🙏🙏

  • @LatifaIddi-e8n
    @LatifaIddi-e8n หลายเดือนก่อน

    Unisaidie 400,000000/- baada ya miaka 16 nipigie hesabu nijue

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      Katika tovuti ya UTT Amis kuna kikokotozi ambacho kinakusaidia kupata mahesabu kwa urahisi zaidi. Nitatengeneza video nyingine kukuonesha unawezaje kukitumia.

  • @ShebbeMeja-hn8ed
    @ShebbeMeja-hn8ed หลายเดือนก่อน

    Much love ❤ thank you bro

  • @AmosLugatangya
    @AmosLugatangya หลายเดือนก่อน

    Vipi kuhusu Inuka Fund ya orbit securities bado tu hawajatengeneza Application ili kutuwezesha kuingia moja kwa moja kuangalia uwekezaji wetu ?

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      @@AmosLugatangya Kwa taarifa nilizonazo, App ilishapatikana. Ila nitafuatilia kujua taarifa zaidi kisha nitawa julisha kwa sasa hali ikoje.

  • @bigboys016
    @bigboys016 หลายเดือนก่อน

    Hakuna kingereza cha switability bwana,we sema kwamba mifuko yote iko bora ila inategemeana na matakwa ya mtu binafsi😢

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      Sawa sawa mkuu! Umesomeka vizuri. Neno 'suitability' ambalo nililitafsiri kama 'ufaaji' ni tofauti na matakwa ya mtu. Hutokea mfuko fulani ukawa una nafasi nzuri zaidi ya kuwa na faida zaidi kwa mtu fulani kuliko mfuko mwingine. Na hii ni tofauti na mtu kutaka mfuko mmoja au mwingine. Ili kuweza kujua huo mfuko ambao unafaa zaidi (more suitable), basi mwekezaji anapaswa apitie maelezo vizuri kwenye website ya UTT Amis..

    • @edgerlema2976
      @edgerlema2976 หลายเดือนก่อน

      Almanisha suitability...yenye maana ya kitu kinachokufaa zaidi

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      @edgerlema2976 Ahsante sana kwa uelewa wako mzuri.

  • @kabhikachambala3392
    @kabhikachambala3392 หลายเดือนก่อน

    Echeni kuchanganya Kiswahili na Kiingereza

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      Shukrani sana kiongozi kwa comment zuri. Kwa kweli imebidi ni record video kujibu comment yako. Ni ya msingi sana. th-cam.com/video/NihHVkDW5Vc/w-d-xo.htmlsi=YDI4zXp3ByhKZtkC

  • @GilliardMmary
    @GilliardMmary หลายเดือนก่อน

    mfuko gani ndio mzuri kuwekeza?

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      Hello Gilliard. Ahsante kwa kufuatilia na kwa swali muhimu sana. Hili swali limeulizwa na watu kadhaa tayari na hivi karibuni nitatengenezea video ili kutoa maelezo vizuri.

    • @GilliardMmary
      @GilliardMmary หลายเดือนก่อน

      @@mindsettinginitiative Nakushukuru sna kwa majibu ya haraka sasa nitaomba unitag siku hio video ikitoka maana nataka kweli kuwekeza. Asante sana

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      ✨ Unatafuta Mfuko Bora wa Kuwekeza UTT-Amis? 💸 Tumia Njia Hizi 5 za Dhahabu: 1️⃣ Pitia Sera ya Mfuko 📜 2️⃣ Sifa za Mfuko 📊 3️⃣ Hakikisha Malengo ya Mfuko yanaendana na yako 🎯 4️⃣ Kagua Thamani ya Vipande 💎 5️⃣ Linganisha na Bajeti yako ya Uwekezaji 💵 Jifunze Hapa: th-cam.com/video/vaO5ry0vWfA/w-d-xo.html 💡 Wekeza kwa maarifa, fanikiwa kwa uhakika! 🚀 #UwekezajiSmart #UTTAMIS #FedhaZako #ThamaniYaVipande #SafariYaUfanisi

    • @GilliardMmary
      @GilliardMmary หลายเดือนก่อน

      @@mindsettinginitiative shukrani sana sana nimekuelewa vizuri sana, God bless you.

  • @aikachuwa6956
    @aikachuwa6956 หลายเดือนก่อน

    Somo zurii sanaa sanaa

  • @thomasjmollel
    @thomasjmollel หลายเดือนก่อน

    NAITWA THOMAS JEREMIAH MOLLEL, NILINUNUA VIPANDE WAKATI WA KUANZISHWA MFUKO 2005, NILIKUWA NIKIPATA TAARIFA ZA MAENDELEO NA UKUAJI WA VIPANDE VYANGU MARA KWA MARA, LAKINI BAADAE NIKAWA SIPATI TENA TAARIFA YEYOTE, JE NIFANYEJE KUWEZA KUJUA BALANCE YANGU?

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative หลายเดือนก่อน

      Ahsante Thomas kwa ujumbe. Tafadhali nitafute kwa nambari +358417578763 (WhatsApp) ili tuone tunalifuatiliaje suala lako.

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 2 หลายเดือนก่อน

    Hongera Ezekieli Kwa ubunifu Wa Uanzishwa Wa Session hii

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 2 หลายเดือนก่อน

      Shukrani sana Mr. Rubeni. Pole haukuweza kuungana na sisi. Tujaribu tena wakati ujao.

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 2 หลายเดือนก่อน

    🎉

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 2 หลายเดือนก่อน

    Usomaji Wa vitabu Je Ni Vtabu Vya Aina Gani Hasa Tuna Soma Kwa Faida Ya Wengine

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 2 หลายเดือนก่อน

      Tuna uwanja mpana wa vitabu vya kusoma. Hii ni kuanzia ujasiriamali, uongozi, mahusiano, falsafa na saikolojia za mafanikio, na kadhalika. Hatusomi vitabu vya shuleni (academic books), hatusomi riwaya, hatusomi vitabu vya dini, hatusomi vitabu vya siasa.

  • @rubenMbokwa-b3o
    @rubenMbokwa-b3o 2 หลายเดือนก่อน

    Hongera sana Unajitahidi Sana Kutoa Elimu Ya Msingi Sana Ila WatunHata Ku like tunWanaona Gharama

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 2 หลายเดือนก่อน

      Shukrani sana Mr. Ruben. Umekuwa supporter mkubwa sana wa Mindsetting Initiative na kwa hilo nashukuru sana.

  • @robert.joseph
    @robert.joseph 2 หลายเดือนก่อน

    Nice interview keep it up

  • @asheriobadiah
    @asheriobadiah 2 หลายเดือนก่อน

    Hongereni orbit kwa ushindi

  • @sarahsengerema8660
    @sarahsengerema8660 2 หลายเดือนก่อน

    Google link sijaiona

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 2 หลายเดือนก่อน

      Pole sana Sarah. Jaribu hapa: drive.google.com/file/d/1BPcGFj4mFxpXhBwW9KwQJOvFzXAMtHSN/view?usp=drivesdk

  • @ngasalagambi6585
    @ngasalagambi6585 2 หลายเดือนก่อน

    Ni njia zipi naweza nikawekeza katka soko la hisa na upatikanaji wak😊

    • @mindsettinginitiative
      @mindsettinginitiative 2 หลายเดือนก่อน

      Njia kubwa za kuwekeza katika soko la hisa ni tatu. 1. Kununua hisa za kampuni moja kwa moja. 2. Kuwekeza kupitia mifuko ya wazi ya uwekezaji wa pamoja, kama UTT, Inuka Fund 3. Kuwekeza kupitia mifuko ya uwekezaji wa pamoja ambayo haiko wazi, kama NICOL. Ili kujua namna ya kuwekeza, tafadhali wasiliana na broker akupe ufafanuzi vizuri. Wako broker wengi, ila ninaopendekeza kwako ni Orbit Securities. Watafute kwa namba hii. +255 747 138 101 (Ammi Julian).

    • @shammhagama2527
      @shammhagama2527 11 วันที่ผ่านมา

      Je nikiwa na laki tano naweza kuanza kununua Hisa moja kwa moja??​@@mindsettinginitiative